Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Aisee, hii sio stori bali ni tamthiliya, nadhani watu mlioishi Bondeni mkiungana na mkaunganisha visa vyenu mnaweza mkatoa filamu au series nzuri tu...

Mfano kisa chako kimejaa mapenzi, kuna jamaa aliweka uzi wake hapa namna alivyonusurika kuuawa na polisi...

Sababu ya kufariki kwa Khumbu ni gani?
 
Ndugu zetu Wangoni, si ndugu zao pia...

#TheNguniPeopleFromSouthAfrica
 
Bora ulivoisha mana umenipitisha kituo cha gari,pili unakuka sana muda wangu
 
Huu uzi unavoanza nilisoma kidogo ata episode sikumaliza nikaudharau ila now nimekua mtumwa

Ila fresh lote life
 

Hahhaa mda sio mrefu tunapelekwa telegram


Author wa Jf mpo fit balaa.

Haya bwana na wewe unataka buku au
 
Kwa hiyo ambao hawana starehe maisha yao hayana mwisho au umeandika kuharibu hali ya hewa?

Anyway tuachane na hayo uko NMB ya wapi mkuu?
 
Matukio yote nayasummarise hapa angalau nitoe lawama maana mnavyonishambulia si kitoto.

Baada ya Khumbu kuja na huo mkoko mpya nikamwuliza ameupataje. Akasema kanunua kwa mkopo. ...Baadae kupitia kwa yule demu wa mshikaji niliyewaambia alihamia, alinipa siri ya huo mkoko mpya wa Khumbu. Aliniambia hiyo ndinga kanununuliwa na Mayor wa Durban. Khumbe hata ile habari ya kuniambia kuwa kapata kazi bank hatutakuwa tunaonana mara kwa mara ilikuwa uongo tu. Alitengeneza mazingira ya mimi kutokuwa namuhitaji kila mara ili Mayor akimuhitaji awe anapatikana. Yaani mimi aniweke kando ili awe huru na Mayor. Hivyo hizo story za kuwa busy na kazi ilikuwa za uongo.

Siku niliyotaka kuingia mikononi mwa police:

Wale jamaa walianza kufungia mzigo humu ndani tulimokuwa tunaishi. Lile gheto la kule mwanzo ulikokuwa unafungiwa mzigo waliacha kulitumia. Hivyo mzigo ukaanza kupimwa humo humo getoni tunapoishi. Binafsi kukaa kwenye nyumba na hayo makitu kilikuwa ni kitu ambacho nilikuwa sikitaki kabisa. Baada ya mambo kuanza kufungiwa humo nikaanza mchakato wa kuhama maana niliona hapa naenda kuhatarisha maisha yangu ya chuo. Nilijua tu kuna siku tutavamiwa humu.

Kufunga hayo madude wanatumia hii mifuko ya plastic tuliyokuwa tunaiita ya rambo. Sasa kwenye kufunga lazima kuwe na vipande vipande vya hiyo miplastic kwenye kukatakata. Na hivyo viplastic ukikutwa navyo hata kama hawajakuta mzigo umekwisha maana wazee wanavijua hivyo vipande vya plastic huwa vinasababishwa na nini.
Sasa hawa jamaa kila wakifunga walikuwa wanavizoa tu hivyo vipande na kuvikusanya na kuviweka kwenye makabati. Walikuwa wanasubiria mpaka yawe mengi ndio wakatupe. Kitendo cha kuishi na hivyo vipande vya plastic kilikuwa kinaninyima amani kabisa, halafu ukiwaangalia hawa masela hata hawajali kabisa. Nilichokuwa nafanya ilikuwa kila asubuhi nikiwa naenda chuo navishindilia kwenye begi naenda kuvitupa mbele ya safari ili angalau tukivamiwa wasikute ushahidi wowote. Maana hawa jamaa zangu walikuwa hawajali kabisa.

Sasa siku moja ilikuwa Jumapili, na sikuwa na mpango wa kwenda kokote. Mule ndani kulikuwa na hivyo vipande vya viplastic. Nikaamua acha nikavitupe ili nishinde home kwa amani. Nikawa nimevishindilia kwenye begi langu la shule. Ila kama Mungu tu ameniambia, Konda msafi be careful. Japo nilikuwa natoka mara moja kwenda kuvitupa, niliamua kuvaa kama vile naenda mbali. Yaani sikutaka kutoka let's say nimevaa bukta na vest kwa sababu najua natoka mara moja na kurudi. Nilivaa nguo kama naenda mjini au chuo. Nikachukua kabisa na kitambulisho changu cha chuo. Nikaweka begi mgongoni, nikatoka ndani, nikashusha ngazi na kuanza kuelekea getini nikiwa na rimoti ya geti. Ile kufungua geti tu nakutoka nje ya geti, mara pah! Kipira cha wazee kimepiga break miguuni kwangu, dah! Roho ikalipuka pah! Nikasema hapa nimekwisha. Wakisema tu fungua hicho kibegi tuone ndani kuna nini nimekwisha. Nikawa naona sasa shule ndio imefikia mwisho. Kipira kimesimama miguuni kwangu. Walikuwa askari weusi. Wakashusha kioo cha gari upande niliokuwepo wakaniambia nisogee karibu. Nikasogea, jamaa walikuwa wawili, kama nilivyosema wote weusi wapo kwenye uniform. Nikawa najitahidi nisionyeshe wasiwasi wowote. Wakaniuliza, unakaa humu ndani? Maana nilikuwa ndio nimetoka tu hapo getini. Nikasema ndio nakaa humu. Wakaniuliza tena, humo kwenye begi kuna nini, nikasema kuna vitabu vya dini, naelekea kanisani kufundisha kipindi cha dini kwa ajili ya watoto. Halafu kile kitambulisho cha chuo nilikuwa nimeking'iniza kifuani. Wakaniuliza wewe ni mwanafunzi, nikasema ndio, nikawapa kile kitambulisho wakakiangalia harafu wakanirudishia. Kisha wakasema tulikuwa tunakusalimia tu, wahi kanisani ukamtumikie Mungu. Wakakanyaga mafuta wakasepa, dah! Aisee! Kwanza nilifikiria sijui nirudi ndani nisiendelee kwenda kuyatupa haya madude. Nikaona acha niendelee na safari ya kwenda kuyatupa maana wasije wakageuka wakaniona tena narudi ndani nikawapa wasiwasi, mbona huyu kasema anaenda kanisani halafu amerudi ndani tena? Basi nikaanza kutembea fasta, hapo naangalia kona yoyote nitakayokutana nayo nipige, nipotee kabisa kwenye hiyo barabara. Kona tu ya kwanza nilipoipata nikaikamata, nikatembea mbele kidogo tu, nikafungua begi na kuyatoa hayo madude fasta na kuyatupa. Nikatembea mbele kabisa huko kuzunguka ili nirudi nyumbani kutokea upande mwingine.

Itaendelea jamani.... nilisema nitasummarise ila nashindwa kusummarise. Huko mbele acha nijifunze kusummarise.
 
Sammarize kifo cha kumbuh
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…