Jinsi kilimo kinavyowafilisi watu wa Bagamoyo

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,880
Katika kauchunguzi kangu kadogo nimegundua watu wengi wanalazimisha kilimo kwenye ardhi ya bagamoyo wakati sio rafiki kwa kilimo,watu wamesahau upande huu wa Mkuranga,Kimanzi na Rufiji ambapo pana ardhi bikra na pia bei ni chee.

Watu wengi wanakimbilia bagamoyo ambapo ardhi ni ghali na haina rutuba kama iliyopo kanda hii mfano jamaa yangu amenunua Bagamoyo na mimi nikanunua Kimanzi, amepanda ufuta na mimi nimepanda ufuta,wangu umetoka wote tena una rutuba vizuri,wake umetoka moja moja, amarudia lakini hali ni ile ile.

Mimi nachanja mbuga saizi nipo kwenye palizi yeye amekata tamaa,ukitaka utoke kwenye mashamba ya bagamoyo uwe na capital ya kutosha,hata nanasi ya kimanzi au rufiji na ya bagamoyo huwezi linganisha,bagamoyo ameiweza mkwere kwenye nanasi kwakuwa ana capital kubwa,hata shukuru kawambwa naona anahangaika tu, vijana wenzangu nawakaribisha kimanzi.
 
Kwa mfano nikitaka kununua shamba la ukibwa wa heka tano huko mkulanga itanigharimu shillingi ngapi kijana mwenzangu?
 
kule eka ni laki mbili tu,ila mimi siuzi wala sio dalali,kama umesikia sehemu inaitwa nyamato
 
Sometimes kilimo ni kama kamari usiwekeze hela yako yote kwenye kilimo mana unaweza kuja lia kilio cha kusaga meno..tenga. Kiasi kadhaa wekeza kwenye kilimo na kiasi kadhaa kwenye biashara yoyote hata kama ni ya mtaji mdogo huku ukisubiri kupata matokeo ya ulichopanda.
 
Wanajamii natoa angalizo.
Huyu ndugu yetu aliyeamua kwenda maeneo yenye bei hiyo inawezekana kajitoa muhanga. Maeneo kama hayo yapo ila tatizo na vijana akienda huku ameshika smartphone akakuta barabara haijulikani, TANESCO na DAWASCO hawapo, majirani wako km 2 kila upande n.k fasta unakimbia kurudi Dar eti ni maeneo hatarishi. Sasa hayo maeneo ndo yenye udongo wenye 'bikra' na ndo mheshimiwa anatualika twende huko. Wakenya wakiona maeneo kama hayo hawafanyi utani na mpaka uwashtukie tayari walishatengeneza hela ya kutosha.
 
Mbona mate yashaanza kunitoka kabla sijafahamu?

Nchi hii bado ardhi ni bei rahisi sana ila kwasababu watu tunataka kujazana Dar na tunalipenda joto la Dar basi ukipelekwa keingine unaona maisha ni magumu sana ila baada ya miaka 10 ijayo misoto itakuwa mikubwa na ndipo tutakapokumbuka huko tulipopaita Sigimbi ila napo patakuwa hapashikiki kwa bei za mashamba
 
Back
Top Bottom