Jinsi Halotel wanavyowatapeli wateja kwa sasa

ukabu

JF-Expert Member
Dec 9, 2011
212
68
Wakuu nimeleta Uzi huu hapa kwa lengo la kutaka kuwaambia Kampuni ya Halotel kua wanachotufanyia wateja wao sio kabisa.

Yani nimewafuatilia kwa muda wa mwezi sasa ila nimegundua wanatuibia ....

Kwa kifupi ukijiunga na kifurushi chochote cha internet mfano ukapewa gb 1 sasa wao wanalikamua gb lako fasta hata we bila kutumia ...

Ukitaka kuprove hilo jiunge kifurush cha internet halaf download app yoyote ya kucount zile upload na nowloads unazofanya utaona umetumia mb 300 then unaambiwa umetumia mb 800..

Kwa waliotumia Halotel mwanzoni mpaka sasa nadhani mnataKubaliana na Mimi kua mb za Halotel kwa sasa zimeghubikwa na unyamganyi....

Wito wangu ni kwamba

Halotel rudishen tariff zile mlizokua mnatumia mwanzo ambazo mtu anajiunga mb zake na zinatumia sio mnazikata...

sio poa tuliwaamini sana na sasa mnachotufanyia tutawahama turudi zetu tulipokua...
 
Mkuu ulichosema ni kweli. Ukijiunga kifurushi cha halotel ukapata, kwa mfano, MB 500 na hapohapo ukadownload file lenye ukubwa wa MB 100, ukiangalia salio utakuta MB 320. Wanakuwa wamekuibia MB 80 mubashara. Wizi mwingine ni pale unapojiunga na kifurushi cha MB 600 halafu wanakigawanya kiwizi: (500 MB na 100 za usiku). Ukitazama salio la MB za usiku huzioni na hawasemi ni usiku wa kuanzia saa ngapi hadi saa ngapi (kama Vodacom). Halotel ni QUMER wa kutupwa! Ijapokuwa mitandao yote ni wezi lakini halotel wamezidi na wanaiba kitoto sana. Nimeamua kurejea vodacom kwa kuwa wizi wao ni wa kisayansi na hauumizi sana. Nawashangaa TCRA wapo kimya huku sisi tukiibiwa.
 
Hongera kurudi nyumbani.
Mitandao mingine sina imani nayo, juzi nimefanyiwa mbaya na Tigo Pesa japo nimeliwa jero tu.
 
Haloter wezi nazani hata mwenyewe wataona kwamba wanao tumia simat wengi tumewakimbia walitaka kunifirisi ukinunuwa gb 1 uki download move ya mb 700 haijai unambiwa mb zako zimeisha
 
miw juzi niliweka elf 2, sikujiunga na data nikazima, naamka asubuhi kuwasha simu, hee nataka kujiunga sasa naambiwa sina balance ya kutosha kwa hiyo elf 2, kutizama balance naambiwa 1940, nikaona ni kweli hawa jamaa kweli wanatukamia sana
 
ila kumbukeni kuwa mb unszokatwa sio za file unalo download tu, kama unatumia komputa, inavitu vingi kama ant-virus, app, browser na kathalika na kathalika, ambayo ina update kutumia mb hizo hizo.

Hata hivyo, unapaswa kutoa malalamiko ukiona ndivyo sivyo.
 
Wakuu nimeleta Uzi huu hapa kwa lengo la kutaka kuwaambia Kampuni ya Halotel kua wanachotufanyia wateja wao sio kabisa.

Yani nimewafuatilia kwa muda wa mwezi sasa ila nimegundua wanatuibia ....

Kwa kifupi ukijiunga na kifurushi chochote cha internet mfano ukapewa gb 1 sasa wao wanalikamua gb lako fasta hata we bila kutumia ...

Ukitaka kuprove hilo jiunge kifurush cha internet halaf download app yoyote ya kucount zile upload na nowloads unazofanya utaona umetumia mb 300 then unaambiwa umetumia mb 800..

Kwa waliotumia Halotel mwanzoni mpaka sasa nadhani mnataKubaliana na Mimi kua mb za Halotel kwa sasa zimeghubikwa na unyamganyi....

Wito wangu ni kwamba

Halotel rudishen tariff zile mlizokua mnatumia mwanzo ambazo mtu anajiunga mb zake na zinatumia sio mnazikata...

sio poa tuliwaamini sana na sasa mnachotufanyia tutawahama turudi zetu tulipokua...
Embu tusaidie iyo program ya kuesabu kiwango cha Megabytes zilizotumika
 
Mitandao yote ya Tanzania wanaiba MB kasoro TTCL. Nimenunua kifurushi cha GB 10 kwa wiki cha Airtel mara mbili lakini hizo GB 20 HAZIKUMALIZA HATA WIKI wakati internet yao ipo very slow.

Majuzi nilikuwa nchini India nilikuwa nanunua GB 2 kwenye platform ya 4G na ilikuwa inanichukua zaidi ya wiki 2 kuzimaliza. Tena kuna wakati zilimaliza mwezi zikabaki.

Sasa hapa TZ internet ipo slow kiasi kwamba live streaming siangalii na hata Youtube inasumbua na bado vigurushi vinaisha bila matumizi.
 
Uko sahihi Halotel kuna tatizo kubwa sana .nilimnunulia mtoto kifurushi cha chuo Mara kadha 1.2gb atulie kwa thl. Matumizi yake ni tofauti sana na hapo mwanzo ilikwisha mithili ya 200mb. Udhaifu mkubwa upo TCRA
 
Si bora nyie mnaibiwa MB tu..
Hakuna wezi Wa vocha na MB jamn kama TIGO...
Wanatuibia sana hela,imefika kipindi hukai na vocha kwenye simu mpaka pale unapotaka kujiunga.
 
Isije kuwa mmetumwa ...cjui..lakini kwangu matatizo hayapo kabisa...cku wakiniibia na mimi nitahama
 
Kwa sasa siwezi kuwaponda Halotel hata kidogo ila wakianza kuniibia tu utasikia ushahidi wangu hapa wananiweka hewani na 1500 wiki nzima madakika ya kutosha na mb za kutosha .

Waendelee hivyo hivyo maana hata Voda nilishaanza kuwasahau.
 
Back
Top Bottom