Wateja wa Halotel kupiga simu pamoja na kutumia internet bila kikomo kwa shs 10,000/= tu kwa mwezi mzima

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
5,265
2,000
Source: Wateja wa Halotel kupiga simu, kutumia intaneti bila kikomo

Kampuni ya Simu ya Halotel imeanzisha huduma ya Royal Bundle ambayo itawawezesha wateja wake kupata huduma zisizo na kikomo

Huduma hizo ni kama vile kupiga bila kikomo simu za ndani na kimataifa, kutumia intaneti bila kikomo pamoja na kuunganishwa moja kwa moja pindi vifurushi vitakapokwisha. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung, alisema mbali na kuzingatia ubora na unafuu wa huduma zao, ubunifu ni silaha kubwa ambayo wanaitegemea katika kuwafikia wateja wa makundi yote katika kila kona ya nchi.
“Royal Bundle’ imekuja kukata kiu ya wateja ambao walikuwa wanatamani kutumia huduma zetu bila ya kupata bugudha ya aina yoyote zikiwamo salio kuisha au intaneti kukata.Tunatambua umuhimu wa sekta ya mawasiliano katika shughuli za kiuchumi, hivyo tusingependa kampuni yetu kuwa kikwazo katika kulifanikisha hilo.Ndiyo maana leo tunawatangazia Watanzania wote kuwa kwa shilingi 10,000 tu unaweza kupiga simu za ndani na kimataifa kama vile kwenda nchi za India, China, Canada na Marekani bila ya kikomo, kutumia intaneti bila ya kikomo, kutuma SMS bila ya kikomo, na kama haitoshi, mara tu muda wa kifurushi utakapokwisha tutakuunganisha mara kwa mara,” alisema Van.

Alisema faida ni nyingi za kujiunga na huduma hii. Kwa mfano, kwa shilingi hiyo hiyo 10,000 kwa mwezi mteja atajipatia muda wa maongezi wa dakika 520 kupiga simu mitandao yote, kifurushi cha intaneti yenye kasi cha GB 2, pamoja na kuwezeshwa SMS 500.

Endapo kifurushi hiki kitafikia ukomo, mteja ataweza kuwasiliana kwa gharama nafuu kabisa. Ataweza kupiga simu kwenda mitandao yote kwa shilingi 1 tu, atatumia shilingi 2 tu kwa sekunde kupiga simu kimataifa, atajipatia MB 1 kwa shilingi 5 tu, na kutuma SMS kwa shilingi 2 tu. Kiufupi ukiwa na ‘Royal Bundle’ hakuna huduma yenye ukomo,” alisisitiza Mkurugenzi wa Halotel nchini.

Aidha, mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuzindua huduma nyingine ya “Tomato Bundle” ambayo ni maalum kwa wateja wa Halotel nchi nzima, itakayowawezesha kupiga simu bure kwenda namba yoyote ya Halotel kwa dk 5 za mwanzo kwa kila simu pamoja na kupata salio la ziada la bure la Sh. 4,000 ambalo mteja atalitumia kwenye huduma nyingine za Halotel (kwa mwezi mzima). Wateja wa Halotel kupiga simu, kutumia intaneti bila kikomo
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,326
2,000
Wizi mtupu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,042
2,000
Yani 10 wanipe GB 2 kwa mwezi upuuzi mtupu ,watu wengine tunatumia Zaidi internet kuliko kupiga simu na hiyo mi-sms yao,kwa mfano mimi naongea na mama mtoto imezidi sana Dk 1:08 mchepuko huwa namtumia SMS tu 2 au 3 kwa siku ila muda mwingi nakua online kufanya mishe mbali mbali sasa kunipa GB 2 kwa 10 na hiyo vidakika vyenu naona ni wizi tu kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mufata

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
242
500
Unapanda gari kwa nauli kubwa alafu linatembea mwendo wa kilometa 30 kwa saa, alafu wanakwambia wakati wa kurudi hautalipa nauli watakupa ofa.Hawa halotel ni ovyo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom