Alagwa
Member
- May 30, 2012
- 95
- 85
Tuelewane kidogo... Ishu sio bei ya tv au ukubwa wa tv yako bali gharama ya tv yako kwenye Maisha yako nikubwa sana kiuchumi kama utapiga Mahesabu vizuri.
Tunanunua kwa gharama sana ili kujiburudisha lakini sio gharama hiyo tuu pia tunatumia muda mwingi kuangalia tv hiyo ambapo muda huo tungeutumia kufikiria au kufanya shughuli itakayokuingizia kipato zaidi kama unaona shughuli hakuna basi tenga hata muda kidogo wa kutafakari Maisha yako na mishe mishe zako alafu ndio peleka macho yako kwenye tv baada ya kutumia muda kujiwekezea mwenyewe binafsi kwa kujitafakari.
Sisemi tv ni mbaya ila isichukue muda mwingi kwenye maisha yako kiasi cha kukosa muda na familia hapa nimeitaja familia kwakuwa wengi tunafikiri muda tunaoangalia tv na familia ndio muda wa familia hapana muda wa kuangalia tv hata kama familia nzima ipo ila ni muda wa tv lakini sio muda mnao utumia kuongea na kujadili mambo ya familia.
Leo nimeandika kwa kifupi tuu. Je wewe unaonaje hili?