Jinsi Consistency prayers inavyofanya Mungu atatue shida yako

Jinsi Consistency prayers inavyofanya Mungu atatue shida yako

The Chosen Liberator

Senior Member
Joined
Jun 21, 2025
Posts
123
Reaction score
66
Habari yako wewe unayesoma uzi huu muda huu.
Leo ni siku nyingine Bwana Mungu ametupa nguvu ili tuendelee kupambana kuutafuta Uzima wake na kupata amani ya kweli ndani ya mioyo yetu.
Hatuna budi kumshukuru Mungu kwa neema hiyo.

Leo ningependa kuzungumza kuhusiana na fundisho hili la kiroho tunalolipata kutoka kwa Yesu kupitia Luka 11:5–8.

Wengi tunapojikuta katika shida, mara nyingi huwa tunaomba mara moja kisha tunasubiria matokeo ya tulichokiomba na tukiona maombi yetu hayajibiwi tunaanza kufikiria Mungu hasikii au pengine anabariki kwa upendeleo lakini si kweli.

Je, Tuombe kwa mtindo upi?

Yesu alitoa mfano katika luka 11:2 ya kwamba mfano ukimuendea Rafiki yako wa kweli usiku wa manane, ukamwambia “Rafiki yangu, nisaidie mikate mitatu nina rafiki yangu amefika nataka nimuandalie chochote kitu” Rafiki huyo akajibu — “Usinisumbue, mlango umefungwa, nimekwisha lala na watoto wangu", Lakini ukaendelea kumuomba na kuomba kwa uthabiti, Je, rafiki yako hata amka na kukupa kwa kadiri ya haja yako?
Lazima ataamka na kukupa tu.

Unapomuonyesha Mungu hali halisi ya shida yako hata kama inaonekana hakuna suluhisho, uendelevu wa maombi bila kuchoka wala kukata tamaa humfanya Mungu kuona ya kwamba unamtegemea yeye kwa 100% kwa situation hiyo unayopitia.

Unapoonyesha kutokukata tamaa ya kuomba, unamuonyesha Mungu ya kwamba huna kimbilio lingine zaidi yake.

Kama ukimuomba rafiki yako mara moja kisha akakujibu kuwa ameshalala hawezi kuamka na kisha wewe ukaamua kuondoka zako kwa hasira, Je, utapata mkate kwa ajili ya rafiki yako huyo mgeni?
Jibu ni Hapana huwezi kuupata.

Kama rafiki yako ataamka na kukupa kwasababu utandelea kumuomba bila kuchoka na kwa uthabiti, Je, si kwamba Mungu aliye mbinguni atakupa zaidi kwa kadiri ya haja yako?

Maombi endelevu na thabiti si maneno tu, bali kuonyesha ukweli wa moyo wako kwamba yeye ndiye kimbilio la mwisho na kukazana uomba bila kuchoka haswa pale unapoanza kuhisi kama haujibiwi.

Unapoonyesha hali ya kukata tamaa na kuanza kujaribu kutafuta msaada kwa wanadamu, Shetani kupitia Roho waovu anaweza akakupa matokeo madogo yatayokufariji kwa muda mfupi ili uzidi kuona Mungu si msaada lakini mwisho wake huwa ni mchungu zaidi.
Shetani hawezi kukupa Uzima na Amani ambao yeye mwenyewe amekwisha upoteza tayari.

Hili ni somo kubwa sana analotufundisha Yesu kuhusiana na consistency prayers, anatufundisha kuendelea kuomba, bila kuacha.

Maombi ya aina yeyote ile, Maombi ya kufunguliwa, Kuponywa, kuomba msamaha, Shukurani, Uzima, Riziki ya kila siku na kuokolewa na yule mwovu yanahitaji moyo safi na uendelevu wa kila siku.

Kumbuka Yesu baada ya kutoa mfano huo akatusihi akisema katika Luka 11:9 kwamba — "Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa.".

Kuendelea kuomba ni ishara ya ukweli na unyenyekevu. Hata pale tunapoona hali ngumu, Mungu anaona hali yetu ya kweli na hatimaye hufanya kadiri ya haja yetu.

Kwa hivyo mtumishi wa Mungu usikate tamaa katika maombi yako, endelea kuomba, endelea kuomba, endelea kuomba na Mungu atakupa kwa kadiri ya haja zako.

Kumbuka maombi ya kweli ni yale yaliyoambatana na matendo mema hivyo lazima ukubali kuachikia matendo yote ya kimwili yasiyofaa ili nafasi ya roho ya Mungu ipate kukaa ndani yako.

Ukisoma ile wagalatia 5:19 imeeleza kwa uzuri zaidi;

19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya: uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo mengine yanayofanana na hayo.

22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.


Kama umefanikiwa kusoma uzi huu mpaka mwisho Mshukuru Yesu kwa neema hiyo.

Ubarikiwe mtumishi wa Mungu.
 
Yesu ni njia , kweli na uzima
Asante sana mtumishi, umenibariki sana. Nina jambo langu ninaomba kwa Mungu anitendee,nikachoka, hata nikaona Mungu hana msaada tena, nikajiingiza kwenye njia fupi fupi za kutafuta faraja ya muda mfupi, naona hii njia si nzuri, ni heri kumrudia Bwana. Mungu muweza wa yote aniongoze, azisikia haja za moyo wangu. Asante sana kwa somo zuri The Chosen Liberator
 
Back
Top Bottom