Uchaguzi 2020 Jinsi ACT-Wazalendo na CHADEMA vitavyoangukia pua katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Siasa sio uadui na siasa ni suala muhimu kwenye ustawi wa jamii.Lakini pale mwanasiasa au Chama cha siasa kinapoitumia vibaya siasa huwa na matokeo mabaya sana.

Sisi bahati nzuri Chama tawala kimekuwa makini sana katika kuwashughulikia wanasiasa na vyama ambavyo vimekuwa na mbaya juu ya Taifa letu.

Act wazalendo na kiongozi wao walidiriki kuandika WB barua eti nchi yetu isipewe mkopo wa kuboresha elimu hapa nchini kwetu. Kwa akili ya kawaida tu hawa ni wazalendo kama wanavyojiita? Wanadai kuna ubaguzi katika utoaji elimu. Kisa serikali haitaki kuruhusu wanafunzi wanaondekeza ngono na kupata mimba kuendelea na shule.

Hao hao Act wazalendo walizunguka kwa mabeberu na kusema kuna uminywaji mkubwa wa demokrasia hapa nchini. Kama kuna uminywaji hicho chama kingekuwepo?

Limekuja Janga la Covid-19. Wakaungana na Chadema na kushinikiza serikali iweke lockdown. Na kila kaya ipewe laki tatu. Hili jambo linawezekana? Mbaya zaidi waliungana na kuichafua nchi yetu na kusema inapika data eti watu kwa maelfu wamekufa na wanazikwa usiku.

Kama makosa kama hayo yalitokea walipaswa kuongea na vyombo kama ITV au TBC na sio kwenda Aljazeera na Bbc kuichafua nchi yetu.

Kwa hiyo Act wazalendo fake na Chadema wapiga madili. Wananchi wamechukia sana. Maana hamna umoja na taifa letu. Nia yenu ni kuleta mpasuko na mgawanyiko. Hivyo Oktoba mtapata mlichokipanda.

Nawaambia mtavuna mlichopanda.
 
We si bwege usiejua kitu kazi yako kutetea upuuzi.
 
Ni mapimbi kama ww ndo wataipa ccm kura..lkn wenye akili timamu hawataipa ccm kura...sukari tu imewashinda alaf mnajinasibu kuwa mnaweza...mnaweza kuteka na kutesa wapinzani baaasi
 
Kwenye hili janga la COVID-19 Mbowe Mugabe amefadhili utengenezaji wa majeneza, kuyapiga picha na kuyaweka mtandao ili kueneza taaruki kwamba watu wanakufa wengi mitaani lakini kwa nguvu za Allah mpango huo umefeli!
 
Ni mapimbi kama ww ndo wataipa ccm kura..lkn wenye akili timamu hawataipa ccm kura...sukari tu imewashinda alaf mnajinasibu kuwa mnaweza...mnaweza kuteka na kutesa wapinzani baaasi
Tumia asali kama sukari imeisha!
 
Ni mapimbi kama ww ndo wataipa ccm kura..lkn wenye akili timamu hawataipa ccm kura...sukari tu imewashinda alaf mnajinasibu kuwa mnaweza...mnaweza kuteka na kutesa wapinzani baaasi
Tatizo la sukari limeshakwisha. Hapa hoja ni uzalendo. Chadema na Act wazalendo hamfai. Hamlitakii mema taifa letu.
 
Kwenye hili janga la COVID-19 Mbowe Mugabe amefadhili utengenezaji wa majeneza, kuyapiga picha na kuyaweka mtandao ili kueneza taaruki kwamba watu wanakufa wengi mitaani lakini kwa nguvu za Allah mpango huo umefeli!
Sasa ndio watanzania wachague Chadema? Labda tunaumwa akili.
 
Back
Top Bottom