JINO Linaua Balaaa!!!

JINO Linaua Balaaa!!!

Jerhy

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
3,135
Reaction score
1,001
Naombeni kufahamishwa endapo kuna dawa au tiba kamili kwa jino nje ya kung'oa.
Ninagalagala sakafuni ile mbaya hino halitulii kabisa awali nilitumia DFP lakini maumivu yamechipuka tena. Ni jino la premolars upande wa juu kushoto, nahisi maumivu makali mpaka mishipa kichwani imenitoka alafu nimevimba vibaya sana, naombeni mnijulishe dawa au tiba halisi au mtaalamu wa meno anisaidie kwa sababu limetoboka na hata nikiswaki hamna damu inayotoka plse msaada ili nikatibiwe maana nateseka balaaa
 
Mi si mtaalam wa meno ila sayansi rahisi ni kwamba huwezi zuia 'decaying process or stopping it' tunachofanya ni kujikinga isianze kutokea. Hapo suluhisho la kudumu ni kung'oa jino lako au unaeza enda mbali zaidi kupandikiza (ila sikushauri hivyo).
Pole, nakutakia upone haraka.
 
Kuvimba ni dalili ya maambukizi. Wahi hospitali asubuhi utapewa dawa kwanza za kutibu. Halafu jino litashughulikiwa. Hakikisha umesafisha kinywa kila wakati.

Pole sana
 
Naombeni kufahamishwa endapo kuna dawa au tiba kamili kwa jino nje ya kung'oa.
Ninagalagala sakafuni ile mbaya hino halitulii kabisa awali nilitumia DFP lakini maumivu yamechipuka tena. Ni jino la premolars upande wa juu kushoto, nahisi maumivu makali mpaka mishipa kichwani imenitoka alafu nimevimba vibaya sana, naombeni mnijulishe dawa au tiba halisi au mtaalamu wa meno anisaidie kwa sababu limetoboka na hata nikiswaki hamna damu inayotoka plse msaada ili nikatibiwe maana nateseka balaaa

Jaribi kuweka mafuta ya karafuu! Utapata afadhali fasta! Lkn mwisho lzm uende ukamuone dentist!
 
Mkuu, nenda hospitali. Unaweza kuziba jino na likapona bila kung'oa. Kama uko dar unaweza kwenda pande za Pugu kuna daktari mzuri sana wa meno, hautapoteza jino lako. Just PM If utahitaji directions
 
Asante kwa ushauri mwema bila shaka itanilazimu kuwajibika haraka kuweza kupata suluhu mapema. Labda tu niulize hospitali ipi ina wataalamu wazuri wa meno kwa sababu nakumbuka docta mmoja aliwahi kumng'oa jino rafiki yangu siku hiyo mie ndo nilimpa kampani kwenda basi jamaa akazimia kabisa hali iliyonifanya niogope utoaji wa meno, lakini sasa ndo hivo hamna jinsi
 
Pole sana mkuu, ingawa nimecheka sana, maumivu ya jino we acha tu!
 
Nenda Al hilal dispensary maeneo ya mitaa ya libya na jamhuri, kuna doctor mzuri sana wa meno
 
Pole sana mkuu, ingawa nimecheka sana, maumivu ya jino we acha tu!

Jamaa alizirai muda wa nusu saa hivi yaani mpk sasa akifika hospitali yoyote akiona mlango umeandikwa Dr Wa Meno basi hutimua mbio kabisa na

Akisikia mtu analalamika jino jamaa hulia machozi na kulaani sana madaktari wa meno, hivi sasa hana meno 3 na kwmba inampa sana shida hata kutabasamu, ndo hivo.

Hii nadhani docta alikosea na kuvunja mishipa ya fahamu hili linatokea kama mtu anahitsji upasuaji wa kichwa basi wanapasua goti itakuwaje kwa meno?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom