Jino langu linauma sana usiku naomba msaada

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,967
6,463
Wakuu nawasalimu,

Kwakweli usiku umekuwa mgumu sana kwangu, jino, Wataalamu wa meno bado niliowaona bado hawana majibu zaidi ya kuling'oa,

Ina maana dactari wa meno wanasomea kung'oa tu meno na siyo kutibu? Kwa kifupi tuseme wadudu wa meno ni kati ya magonjwa sugu duniani sawa na HIV, n.k?
 
Pulpitis

Linaweza kufanyiwa Root canal ila itatagemea na ushauri wa mtaalamu husika kama root canal itafaa au litolewe tuuu

Ulikuwa wapi hadi jino lifikie katika hali hiyo au ulikuwa unasubiri maumiv yaongezeke
 
Nenda hospital kubwa huenda ukapata tiba pasipo kung'oa, ukienda kwenye vihospital vidogo watakung'oa tu ili isiwasumbua ..!!
 
Pulpitis

Linaweza kufanyiwa Root canal ila itatagemea na ushauri wa mtaalamu husika kama root canal itafaa au litolewe tuuu

Ulikuwa wapi hadi jino lifikie katika hali hiyo au ulikuwa unasubiri maumiv yaongezeke
Root canal ni nini mkuu?
 
Haya ni matibabu ambayo hutolewa kwa jino ambalo sehemu ya uhai wake imeharibika kiasi kwamba haliwezi kutibika kwa kuziba tu, kwa maneno mengine hii ndiyo njia mbadala ya kutibu jino bila kung’oa.

Matibabu uhusisha kutoboa jino hadi sehemu ya uhai wa jino yenye mishipa ya damu na ile ya fahamu na chembechembe za meno na kuviondoa nikimaanisha kuondoa mishipa ya fahamu, ya damu na chembe pamoja na ugonjwa na baadae kuijaza sehemu hii na vitu maalumu vinavyokubaliana na mwili (biocompatible).

Aina za matibabu ya mzizi wa jino
Kuna aina kuu mbili za matibabu ya mzizi wa jino
1. Njia ya kawaida ( conventional root canal treatment )
Njia hii ni kama nilivyoeleza hapo juu, kuingia kwenye kiini cha jino na kuondoa kila kitu kilichomo na kisha kujaza uwazi uliobaki na vitu maalumu vinavyokubaliana na mwili.

2. Matibabu ya mzizi wa jino yanayohusisha upasuaji
kwa njia hii mbali na kutumia njia ya kwanza, upasuaji hufanyika pia ili kondoa mfupa uliofunika ncha ya mzizi wa jino kusafisha eneo lililozunguka ncha ya mzizi na baadaye kukata ncha husika kisha kuziba kutokea kwa nyuma (retro grade filling ). Njia hii hutumika pale njia ya kawaida inaposhindwa kuondoa tatizo au inapoonekana kabisa kuwa haitaweza kuondoa tatizo. Huu ni upasuaji mdogo, unaofanyika kwa ganzi ndogo ya eneo husika (local anaesthesia ). Mafanikio ya matibabu haya ni makubwa sana.

Ni meno yapi yanahitaji matibabu hayo?
• Meno yaliyooza hadi uoza kufikia kiini cha jino (dental pulp ) - sehemu ya uhai wa jino.

• Meno yaliyopata ajali na kupasuka na kuacha kiini cha jino kikiwa wazi (traumatic pulp exposure ).

• Meno yaliyopata ajali na kusababisha mishipa ya damu kukatika au kupasuka na kuvunjika ndani ya jino, kitu ambacho hupelekea jino kufa (pulp necrosis) na baadaye kusabisha jipu au kubadilika rangi.

• Wakati mwingine japo ni mara chache, ni pale tunapokuwa tunataka kuliweka sawa jino/meno ambalo/ambayo hayapo kwenye mstari sawa ili yaendane na meno mengine.

• Pia wakati mwingine, tunapo lisaga jino ili liweze kubeba meno bandia ya daraja ( bridge ) huku tukiwa na mashaka na uhai wake.
Nini dalili zinazoashiria jino kuhitaji matibabu haya?

• Jino linalouma - kuuma kwa jino kunashiria ugonjwa kuwa umeingia ndani ya kiini cha jino na au hata kupitiliza na kuingia kwenye mfupa ulioshikilia jino.

• Jino lililooza na kusababisha uvimbe, liwe linauma au haliumi.

• Jino lililokatika na kupoteza zaidi ya nusu ya kichwa cha jino (crown ) kukatika kuwe kwa ajali au kuoza au vyote kwa pamoja.

• Jino linalobadilika rangi huku kukiwa na historia ya kuligonga mahali au kuchapwa ngumi usoni, hapa jino linaweza kuanza kubadilika rangi miezi sita tangu siku ya ajali mpaka wakati mwingine hadi miaka ishirini wakati mgonjwa alishasahau hata ajali yenyewe.
Meno yasiyofaa kwa matibabu haya.

• Meno yaliyoharibika vibaya kiasi kwamba hayatibiki tena japo ni machache, kwani hata kama jino limebaki mzizi tu, ukiwa bado imara twaweza fanya matibabu haya na baadae kujenga kichwa ( crown ).

• Meno yaliyolegea sana kutokana na magonjwa ya fizi ambayo hayawezi kuimarishwa tena.

• Magego ya mwisho (wisdom teeth ) kwa kawaida meno haya huwa yana maumbile yasiyotabirika kiasi kwamba hata mafanikio ya matibabu huwa hayatabiriki, hii ikiambatana na kuwa yako nyuma sana kiasi cha kuwa vigumu kuyafikia kwa ufasaha na vifaa vyetu na pia yana mchango kidogo kwa usagaji chakula (2%).

• Meno ambayo mifereji ya mizizi ambayo hupitisha mishipa ya fahamu na damu imeziba ( calcified root canals)
Mafanikio ya matibabu haya.

Kiwango cha mafanikio ya matibabu haya ni kati ya asilimia sabini na saba hadi tisini na nane (77-98%). Haya ni mafanikio ya hali ya juu kwa matibabu ya aina yeyote ile, mafanikio huongezeka zaidi pale tabibu anapotumia vifaa vya kumuongezea uwezo wa kuona kama dental loops na operating microscope. Kutokufanikiwa kwa matibabu haya Ziko sababu mbali mbali zinazoweza kusababisha matibabu haya yasifanikiwe, baadhi zikitokana na udhaifu wa tabibu na zingine kutokana na jino lenyewe lilivyo (internal tooth morphology ) .
Tabibu: Iwapo tabibu hakusafisha jino vizuri na kuliziba sawasawa upo uwezekano mkubwa wa matibabu haya kutokufanikiwa. Pia ikiwa tabibu hafahamu vizuri maumbile ya ndani ya jino, kuna uwezekano sehemu zingine kuachwa bila kusafishwa.

Meno: Meno mengine yana maumbile yasiyo ya kawaida, mfano katika hali ya kawaida meno ya mbele yana mfereji mmoja wa kupitisha mishipa ya fahamu na damu, lakini kuna jino lingine linakuwa na mifereji miwili au mitatu, hapa kwa mazoea na kwa kukosa vifaa vya kisasa ni rahisi kusafisha mfereji mmoja na kuacha mingine, vivyo hivyo kwa magego ambayo kwa kawaida yana mifereji mitatu hadi mine, lakini mengine mitano, sita, saba hata utafiti fulani huko China umegundua baadhi ya magego kuwa na matundu nane. Meno ya namna hii ni vigumu kufanikiwa.

Nini kifanyike ili kupunguza uwezekano wa matibabu kutofanikiwa? Tabibu lazima ajikumbushe maumbile ya ndani ya jino analotaka kulitibu kabla ya kuanza matibabu na pia ajue kwamba jino laweza kuwa na mifereji ya ziada hivyo ajitahidi kuitafuta. Matumizi ya vifaa vya kusaidia kuona ni muhimu na hata matumizi ya x-ray za kisasa kama 3-dimensional digital x-ray ili kuweza kuona pande tatu za jino .
Kwanini meno yanaendelea kutolewa wakati matibabu haya yapo?

• Matibabu haya ni gharama ukilinganisha na kung’oa jino hii ikiendana pamoja na umaskini wa wananchi walio wengi ambao hushindwa kugharamia na hivyo kuchagua kung’oa.

• Baadhi ya hospitali hazina wataalamu au vifaa vya matibabu haya au vyote kwa pamoja.

• Mwamko mdogo wa wananchi kuhusu matibabu ya meno, hii inachangiwa pia na tabibu wa meno kutokuelezea matibabu mbadala zaidi ya kung’oa. Tafiti zimeonesha baadhi ya tabibu wa meno hutoa maelezo kwa yale matibabu wanayoyaweza tu, badala ya kuwaeleza pia upatikanaji wa matibabu mbadala katika sehemu zingine.

• Watu kuchelewa kufika hospitalini, wakija baadhi yao matibabu pekee yanayokuwa yamebaki ni kung’oa tu, hapa napo kuna mchango wa umaskini na uelewa mdogo

• Imani potofu kuwa tiba ya kudumu ya jino ni kuling’oa.

• Uzoefu wa zamani, kwa mtu ambaye aliwahi kuziba jino na likauma tena, ukimwambia matibabu haya ni vigumu kuyakubali
Hitimisho.

• Jali meno yako kama unavyojali viungo vingine vya mwili wako.

• Kungoa jino kama tiba ya ugonjwa wa jino, ni pale tu ambapo jino hilo haliwezi tibika kwa njia mbadala kama hii ya mzizi wa jino au pale inapobainika kuwa jino husika kuendelea kubaki pale hata likiwa limetibika linaweza kuwa chanzo cha kuleta madhara makubwa mwilini kama uoto mpya n.k.

........Copied.......
 
Ujiandae kifedha pia angalau uwe na elfu 80 nk kama una bima kajaribu muhimbili pale
 
Ujiandae kifedha pia angalau uwe na elfu 80 nk kama una bima kajaribu muhimbili pale
Mkuu ushauri wako ni mkubwa sana maana kila nikienda wanapa option ya kung'oa adi nikajua hawa jamaa wanajifunzaga kung'o uko shule !!! Ntaenda mwumbili soon
 
mbere
Pole sana naomba nikupe dawa kama utatumia utaleta majibu hapa! Nina uhakika unaufahamu mti wa Mpera (guava tree) sasa kakate kale ka ncha.

Kateke teke namaanisha yale majani malaini ya mwisho kabisa kwenye tawi. Kisha tafuna hasa upande wenye tatizo kwa dk 10-15 asubuh na jioni kwa siku tatu.

Kabla hujang'oa ikidunda hii dawa njoo useme nikuwekeeni ingine!!
 
Ilo jinio ni la kung'oa tu. Litakuwa limeshaoza... Omba Mungu atakupa jino jingine. Hata mimi nilishawahi kuumwa na jino la gego, nikang'oa ila nilibahatika kuota jino jingine...
 
Kama hutaona usumbufu kwenda Moro nitakutafutia namba za askari mmoja mstaafu yupo eneo la 88 anatibu meno bila kung'oa nimeona wengi wameponea kwake, ni-pm J'tatu nitakuwa huko
Anaweza kutuma dawa?
 
Wakuu nawasalimu,

Kwakweli usiku umekuwa mgumu sana kwangu, jino, Wataalamu wa meno bado niliowaona bado hawana majibu zaidi ya kuling'oa,

Ina maana dactari wa meno wanasomea kung'oa tu meno na siyo kutibu?
Kwa kifupi tuseme wadudu wa meno ni kati ya magonjwa sugu duniani sawa na HIV, n.k?
Tumia mkojo kusukutulia jino.
 
Mkuu! Achana na gharama, achana na dawa za wazungu, ngoja nikupe dawa ya uhakika. Kojoa mkojo Wako asubuhi mkojo fresh, kwenye chombo kisafi, Kisha weka mdomoni sukutua mdomoni kama dakika 1, tema Kisha weka mwingine, fanya kama mwanzo Kisha tema, Mara ya tatu unaweza sukutua dakika 2 mpaka 3, fanya hivyo kwa siku 3....

Utakuja kunambia hapa, haitatibu tu hilo jina ila hakutakua tena na tatizo la jino, haina haja kung'oa. Kumbuka kila asubuhi unatakiwa mkojo fresh!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom