what do you think l am? i am also Catholic; lakini vitu vingine ni vya kiimani zaidi kuliko logic. Maana bado kidogo mtaanza kuita hata walio na vipaji vya Roho Mtakatifu kuwa ni Vichaa; na kwamba kama haiwezi kuwa explained na kueleweka katika viubongo vyetu then si kweli au tunadismiss.
Kuna story moja ya Mt. mmoja hivi ambaye alikuwa anatafakari kuhusu utatu mtakatifu; akawa anakaa ufukweni mwa bahari akijaribu kutafuta logical explaination ya Holy Trinity. siku moja akamuona mtoto mdogo amechimba kishimo chake kwenye shore, halafu anachukua maji kwenye kikopo kutoka baharini anajaza kishimo chake. Ameendelea hivyo kwa muda mwisho yule Mt. akamuuliza (huku akiwa annoyed kidogo) lengo lake hasa ni nini. Yule mtoto akasema kuwa, anataka kuyaamisha maji yote ya bahari yaende kwenye kishimo chake. Yule mt. akamwambia huoni udogo wa hicho kishimo na ukubwa wa hii endless bahari. mtoto naye akamwambia, ukubwa wa shimo hili ni sawa na akili zako, na ukubwa wa bahari ni sawa na fumbo la utatu mtakatifu, hivyo huwezi kulielewa kwa kutumia akili zako hizo na mtoto akapotea. So from that day, yule mt. akalikubali na kuliamini bila kutafuta hizo logical explainations ambazo kanisa la sasa linajaribu kutafuta.