Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,578
- 28,698
Mkuu haya uliyoayaandika umeyaandikwa kwa misingi ya Biblia??asigwa;
Leo umetoa mpya. Bado weye unaenda kwa hao wapiga ramli chonganishi. Ati pepo linakemewa na kutaja lilikotoka. Neno la Mungu linasema, Shetani asemapo lolote ni uongo kwani yeye ni baba wa huo uongo wala kweli haimo ndani yake. Asemapo huo uongo ndiyo kweli yake hiyo. Sasa weye wasema ati anataja aliko toka. Huo ni uchonganishi wala sio kweli. Siku nyingine atakupiga mwara, ati; Mamako mzazi kanituma nije muua huyu mwanao, si tiyari chuki kati yako na mamako?? Alikuja ili; aibe, aue na kuharibu. Hilo ndio ujio wake kwenye hiyo familia. Umuue mamako, umchinje na kuharibu mahusiano yenu.
Kamwe, usimsikilize aliyepagawa.
Kwa ajili ya mada; Kuna maambukizi yaletwayo na majini. Hii ndiyo kweli. Kama wachawi wanatembea na wake au waume za watu ni rahisi majini pia
Yesu alipowatoa wale pepo kwa yule Mgerasi hakuwauliza jina lao wakasema wao ni jeshi??
Yesu hakuwa na huo uelewa kuwa Shetani ni muongo na baba wa uongo??
Vipi wale vijana wawili wa Skewa wakati wa mtume Paulo walipojaribu kumtoa pepo pepo akatakaa kutoka na akasema Paulo tunamjua na Yesu tunamjua??
Huo ulikua uongo??
Pepo akiwa chini ya kibano cha jina la Yesu huwa hadanganyi....