Jini mahaba linavyonitesa

Haya ndio mawazo ya busara na si kujiua. Pamoja na maombezi, usiache kwenda clinic pia watakushauri hasa hapo kwenye red siku hizi inawezekana. Pole sana kijana.

Aksante ndugu yangu nitajitahidi na kufuata ushauri wako
 
Wewe acha kumpotosha mwezio kwa waarabu ataambulia mapepo na majini mengi zaidi. Migisha usiende popote uponyaji wako uko kwa Yesu tu

Nami naamini katika yeye awezaye.
 

Naamini katika hilo bro na nimempokea yesu awe bwana na mwokozi wangu. Huwa nasali kila siku kabla ya kulala japo kwa wakati huo kabla ya kwenda safina nilichanganyikiwa na kutokuamini katika mungu japo nimekulia na kulelewa katika familia na malezi ya kikristu.
 

Aksante na ninashukuru kwa ushauri wako ndugu yangu
 

Ni kweli ndugu niliyavunja but kuna kipindi nilishindwa kusimama katika imani pia kila nikijitahidi kuomba huwa napata usingizi mzito ghafla na wakati mwingine huwa nachanganya maneno ila sasa nimerudi kwenye mwanga na huwa nasali pamoja na tb joshua na wise men kupitia emanuel tv. ya
 
Pole sana kwa masaibu hayo je ulisha washirikisha wazee wa kimila juu ya matatizo yako vipi wazazi wanasemaje? majaribu ni ni sehemu ya maisha hata Mungu anasema ukiona umepta jaribu ujue ni saizi yako ndiyo maana limekupata so endelea kwa sala tafuta njia ikupasayo epuka makanisa ya kitapeli kwani mara nyingi hayo ndiyo yatakuongezea matatizo zaidi.
 

Amen nashukuru kwa maneno yako ya faraja.
 

Ni heri kuwa moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu! Wacha Kuchanganya Mungu na hizo altiti na shubiri nyeusi! Bwana Mungu si Mungu wa mizaha.
 

Hapana sijashirikisha wazee wa kimila wala wazazi wangu. Naamini siku 1 yataisha na kuanza maisha mapya.
 
Ni kweli mzee mzizi mkavu hadi kwa umri huu sijaoa japo nimeshajijenga kidogo pia sina hata niliyepanga nae future.
Nilikuwa ni mtu wa mikosi, hasira, kunyanyasa, kuchukiwa, mgomvi, malaya niliyepitiliza. Kwa hali niliyonayo sihitaji mwenza japo nahitaji kuwa na mtoto. Nimekuwa nikilia pindi nikumbukapo wanangu hao wawili. Huumia pindi nionapo mtoto mdogo. Sina jinsi namuachia mungu na nipo tayari kwa lolote.
 
pole ndugu rudi safina uendele kuombewa huku wewe mwenyewe ukiendelea kuoma na kuishi kwa kuamini.... baada ya imani yako kulegalega yamerudi na nguvu mpya
 
Pole sana kijana.Ni kweli una mapepo ila naomba nikueleze kwamba wachungaji wengi wa kipentekosti huwa hawatoi mapepo bali wanayatuliza then wanakupa ya mapepo yao na ndio maana ukiacha kwenda kwenye makanisa yao mapepo yanarudi,wanatumiaga mapepo kufanya miujiza ya uongo.NAKUSHAURI uwe unasoma ZABURI 51 yote kisha Zaburi 35 nayo yote usiku kabla ya kulala.Funga siku 7 kwa maombi unakula usiku tu.Uache maovu unapofunga mbele za Bwana.Hili jambo litaisha ndani ya siku 3 tu.Nakuomba kama uko Dar uje nitakuombea sitaki hata mia.Ila kama uko mbali nenda kanisa lolote la waadventist wasabato waambie nao watakusaidia.
 
Ningependa kusikia ushauri wa watu wasioamini uwepo wa wachawi na majini. Kama Kiranga na NyaniNgabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…