Jina lako lina chapa mbili

Jina lako lina chapa mbili

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,527
Reaction score
830,085
Ni kitu ambacho hujawahi kukiwaza au kukisikia popote, lakini pia Inawezekana kabisa umeshakisikia tena mara nyingi tu lakini pengine kwa lugha tofauti.

Jina lako lina chapa mbili, chapa ya kuzimu na chapa ya mbinguni au kwa maana nyingine chapa ya nuru na chapa ya giza
Kawaida ya mwanadamu hupenda kubalance mambo kwa shetani kidogo kwa Mungu kidogo...kiasili jina lako huandikwa mbinguni tangu uumbaji na unapoingia duniani hufanya new registration ya kuzimu ambayo ndio huwa na nguvu zaidi ya kutawala maisha yako.

Pale unapoangaziwa , kwa imani yoyote ile na kuacha mabaya yote na kuamua kumrudia Mungu wako ni kipindi ambacho hutaka kufuta ule usajili wa kuzimu na kubaki na usajili wako wa asili, usajili wa mbinguni.

Hapa ndipo penye shida na ukisikia vita ya kiroho basi ujue ni hii . shetani hayuko tayari umkimbie kwakuwa usajili wake huweza kufutika tofauti na ule wa mbinguni au haufutiki milele, ni kipindi hiki ambapo shetani hukodi majeshi yake yoote kwa ajili ya kukurudisha kwenye himaya yake...hii ni vita ngumu mno vita ya kiroho vita ya mbingu.

Chunguza kwa makini huwezi kukosa mfano wa walao mtu mmoja unayemfahamu ambaye alikuwa ni mshika dini na mlokole hasa halafu akaanguka dhambini, huwa mbaya maradufu ya vile alivyokuwa mwanzoni na mtu wa namna hii ni ngumu kusimama na kumrudia tena Mungu.

Mtu wa namna hii anapoamua kusimama dede na kupambana kiroho, mbingu hutakisika, familia na jamii huingia katika mkanganyiko mkubwa mambo huharibika na hata vita yaweza kutokea katikati ya jamii hasa kama mlengwa alikuwa ni mtu mwenye nafasi ya kimamlaka na ushawishi katika jamii.

Tunaelekea kwenye uchaguzi ambao kwa namna moja au nyingine na kwa uroho wa madaraka na kutawala kuna baadhi ya washika dau wakaambiwa kuhusisha nguvu za giza lakini vilevile baadhi kwa mapenzi mema kabisa wakaamua kumhusisha Mungu moja kwa moja...hapa tutaingia kwenye uchaguzi wenye chapa mbili mbili uchaguzi wenye utusi tusi wenye vita ya kiroho kati ya ufalme wa nuru na ufalme wa giza.

Mungu pekeyake ndiye atakayeweza kutupitisha salama kwenye uchaguzi huu....tuuombee sana huku tukiikataa ile chapa ya pili chapa ya kuzimu
 
Asa mwanzo nilikusoma fresh nikakuelewa na nikavutiwa coz na mimi nahisi na chapa mbili ( ya kimungu na kuzimu) but ulivyoingiza siasa ukanipoteza mazima.....am truly hate politics!!

Yeah hata mimi nimeliona hilo na sikutaka kufika huko lakini nilijikuta naingia huko it was a kind of unresistable force...but still we can go back to the core of the topic
 
Yeah hata mimi nimeliona hilo na sikutaka kufika huko lakini nilijikuta naingia huko it was a kind of unresistable force...but still we can go back to the core of the topic

Kama ramli kwa mganga wa Kienyeji siyo?

This is what I meant 1445192504598.jpg Angalia mchoro huu vizuri utajikuta kote kote una ID
 
Kupanua mjadala huu usionakane ni wa dini au imani fulani tu, hata kwa wale wasioamini katika Mungu mkuu Mungu mmoja bado nako huko kuna chapa mbili, chapa ya wema na chama ya mabaya huko mbeleni tutakuja kuongelea habari za samsara hungry ghosts arahants wokovu nk nk...angalia mchoro picha huu 1445194210367.jpg
 
JESUS CHRIST is the way,the Truth and Life.Believe in HIM and call HIS NAME,you will be saved your eternal soul
javax kwa kulitaja tu jina la Kristo na kuamini kuwa yeye ndiye kweli na uzima, hakumfukuzi shetani naye akakimbia bali ndio unaingia kwenye mapambano halisi kwenye ulimwengu wa kiroho na kidunia pia
Hiki ni kipindi ambacho unafuta jina lako kuzimu na kutaka liandikwe upya mbinguni kwenye kitabu kile cha uzima wa milele, kwahiyo mapambano halisi na kuzimu/shetani huanza rasmi pale unapomkiri Kristo kwa kinywa na kwa roho yako na kujitoa kwake....

CC: christine ibrahim
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa hisani yako naomba kumkaribisha Mzee Mwakijiji asome huo ujumbe.Maana tuko wengi ametukwaza na programu yake ya Zinduka!

Mtag aje tu, namkaribisha kwa mikono miwili au mpelekee hukohuko aliko
 
Last edited by a moderator:
Mshana,
Umechambua vizuri,

Labda niongezee kidogo, Kibiblia, maandiko yako wazi kwamba unapozaliwa tu, unapewa mambo mawili uchague ama Uzima na Mema au Mauti na Mabaya, Kumb.30:15, Na hii chanzo chake ilianzia pale mwanzo baada ya Adamu na Hawa kukaidi maagizo, Tangu wakati huo, dunia ilitekwa na shetani akawa anaimiliki dunia kila kitu Kiroho na Kimwili na ili kuhakiki kuwa shetani (ibilisi) alikuwa anaitawala dunia angalia Luka 4:3-13, Ibilisi anamuonyesha Yesu Kristo milki yake na fahari ya dunia kuwa ni yake....Hii haikumpa Mungu Ukuu wake akatoa tahadhali kwa kila mtu awe na uchaguzi ama Mungu (Uzima na Mema) au shetani (Mauti na Mabaya), Kwahiyo kama Mshana alivyosema, unapozaliwa tu unakuwa na uchaguzi wa aidha umwelekee Mungu au shetani, Na ujue shetani njia zake ni za uongo, udhalimu, mabaya yote, yatendekayo duniani yeye ndiye mwanzilishi akijipanga kwenda Jehanamu. Wema, ukweli, uwazi, furaha, amani, upendo, kuvumiliana, kuchukuliana, afya na uzima tele ndo mfumo halisi wa Mungu anavyotaka tuishi
 
cc: NDUKI mose
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom