Jina lako JF (ID) ina maana gani na kwanini umejiita?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,789
Hello members!! Nimekua nikisoma id za members kwa kweli zingine zinafurahisha, zinahuzunisha na kusisimua pia.
Nimeona kuanzia uzi huu maridhawa kabisa mwana jamii pita hapa tueleze maana na kwa Nini umejiita hivyo??

Naanza Mimi NALIA NGWENA
Hilo ni jina ambalo nilijiita baada ya kupita jkt, ipo hivi nalia ngwena ni wimbo ambao ulikua ukiimbwa ulikua na mateso makubwa ndani yake tunaita maovyo ovyo,
Ilifikia hatua huu wimbo tuliimba huku tunalia.

Maana afande aliyekuwa akiimbisha huu wimbo alitoa na mazoezi makali humo humo ndani yake.

Kiukweli katika vitu ambavyo sitoweza kusahau ni huu wimbo na ndiyo maana nikajiita NALIA NGWENA

Karibuni wakuu.
 
Named after lovely Zaramo City # nyumba ya amani#ukae kumwetu.
Polish_20230404_115742002.jpg
 
Katika kila kitu unachoonekana kufeli, basi anza upya ukiwa mwenye ujuzi na ubora zaidi na hakika utafanikiwa. As long as unakimaanisha unachokifanya, hakuna kitakachokushinda. Usikate tamaa.

Nikajiita Restart. Hiyo Dr ni baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom