Jina la Yesu lilivyo na nguvu

Jina la Yesu lilivyo na nguvu

Pastor Silla

Senior Member
Joined
Sep 22, 2020
Posts
162
Reaction score
166
Mara nyingi nimesikia watu katika masimulizi yao walipokumbwa na ili za Shetani waliponiambia kwa jina Yesu walipata mpenyo .

Mfamo nakumbuka mwaka ya 2005 nikiwa nimelala ndotoni nilitokea mtu mmoja akiwa amekusudia mabaya juu yangu amenitaiti kweli kweli kila nikikukuruka ananishinda nguvu nilipotamka kwa jina la Yesu niahachie akaniachia nikamshinda.

Naomba na wewe share nasi namna jina la Yesu lilivyoweza kukupa ushindi katika ila zake Shetani.

Asante na karibuni...
 
Tangu 2000 nilipoota usiku wa manane kuwa "Ukristu ni mchongo" siamini tena mambo ya Yesu. Sina jibu ila mpaka sasa najiuliza "Mungu wa kweli atamtoa mwanae kafara kweli?" Afanye kama binadamu wanavyofanya? Nimerudi kwenye imani yangu ya jadi.
Huyo Shetani mkemee jomba , Yesu ndo binadamu maarufu zaidi kuwahi kuishi Duniani , na ndo taarifa zake zinatafutwa zaidi kuliko yyte Yule , huwez ukawa na hii sifa Kwa kubahatisha au Kwa kufikrika never...
 
Kuna waliomfata Yesu Kwa sababu za kibiashara hao wapo mpak Leo na ndo wengi , kuna waliomfata Yesu ili waonekane wapate sifa nao wapo mpak Leo , kuna waliomfata Yesu ili waokolewe wapo mpak Leo Ila ni wachache Sana .... Kwa Yesu kunalipa inategemea unataka nn
 
Kuna siku nipo guest na mdada tulilala toka jana,asubuhi anataka kuniaga nikamuomba tuagane kwa mechi kwanza.Sijui yule dada alikua kama na mashetani vile,baada ya kumaliza mechi nilijikuta nipo ulimwengu mwingine kabisa yaani nilijiona nimekufa.Kumbe yy alidhani nimelala tu. Akili ikanijia nikiwa huko huko sijui wapi sijui ahera ,nikatamka damu ya Yesu inanena mema kadiri nilivyo tamka nikajikuta nimeinuliwa juu sana baada kama ya nusu saa nikaamka .Yule dada alishangaa sana nilipo msimulia mpaka leo sijawahi mtafuta nikahisi atakua na jini la mauti.Kweli jina la Yesu na damu yake vina nguvu sana,ila wengi hawajui.
 
Hakika jina la Yesu na Damu yake vinanena mema mkuu. Vp bado unaendelea na uasherati/uzinzi au umeacha? Karibu kwa Yesu mkuu ya duniani yote ni ubatili mtupu na kujilisha upepo!!
 
Tangu 2000 nilipoota usiku wa manane kuwa "Ukristu ni mchongo" siamini tena mambo ya Yesu. Sina jibu ila mpaka sasa najiuliza "Mungu wa kweli atamtoa mwanae kafara kweli?" Afanye kama binadamu wanavyofanya? Nimerudi kwenye imani yangu ya jadi.

Unaota mara moja tu kwamba ukristo ni mchongo unaamka na kushika ndoto yako,ila ukiota umepakatwa unakuwa mkali na kuhakiki maungo yako kama yameathirika ukiamka.
 
Naona kama tu mchongo wa Wayahudi ambao wamefanikiwa kuuteka ulimwengu. Nyakati za mwisho Mungu wa kweli atakana kuwa hana mtoto wa jinsi hiyo. Watu wangu wanaangamia kwa kuamini vitu vya uwongo.
Exactly ndio maana baadhi yao walimkataa
 
Mimi sio mwanatheologia, ila tuseme hao Wazungu(ondoa neno Wayahudi) . Hivi Yesu alikuwa Myahudi? Ila kuna baadhi ya Wayahudi walimkubali Yesu.
 
Hakika jina la Yesu na Damu yake vinanena mema mkuu. Vp bado unaendelea na uasherati/uzinzi au umeacha? Karibu kwa Yesu mkuu ya duniani yote ni ubatili mtupu na kujilisha upepo!!
Nilisha acha mkuu nampenda Yesu.
 
Nilikuwa Zambia nakumbuka....naingia kulala mida ya 6 Usiku ilikuwa....nikarudisha mlango sikufunga na funguo....nijilaze kitandani ...Ile naegamia mto nikahisi natekenywa sijioni...niinuke kidogo mara naona mto unacheza...kitanda kinacheza nikashuka upesi kutazama kitanda naona godoro linakunjwa na kukunjuliwa...nipige kelele sauti haitoki...natetemeka nakakamaa Mwili nashindwa kumove kuelekea mlangoni....nikaanza kukemea rohoni...Yesu niokoe,Yesu nisaidie....maana kinywa hakifunguki kimefungwa.....nikaendelea kunena moyoni mwangu...Yesu nisaidie...mwisho kinywa kikafunguliwa....aisee....nilipita yoweee😭😭😭 mwacheni Mungu aitwe Mungu
 
Back
Top Bottom