Jimboni kwa Lissu: Wananchi wako naye,wanasonga mbele

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
'Mchochezi' Tundu Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki. Ni Mbunge wa pekee wa upinzani wa jimbo kutoka Singida. Niko jimboni mwake kwa siku ya tatu leo. Najionea na kusikia.

Kwa kifupi,wana-Singida Mashariki wako na Mbunge wao. Wako pamoja na maono na mawazo yake. Wanatembea naye bega kwa bega. Wanafurahi na kusikitika naye.Maendeleo yanapiga hodi ya kasi. Yanawafunika wanajimbo na kuwapa faraja. Wananchi wana fikra mpya.

Cha kipekee kwa Lissu ni alivyojipanga jimboni kwake. Ana timu ya hamu na timamu. Ana wapokea malalamiko;wasikilizaji na wawasilishaji. Uwepo wake hapa,hukamilisha tu mfumo wa mfano alioujenga. Mfumo wake ni wa kupigiwa mfano.

Wana-Singida Mashariki wanafaidi demokrasia ya vyama vingi. Wanaonja changamoto za demokrasia na zinawakomaza kwa kusonga mbele. Najionea ya ndoto zangu za kinchi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Singida)
 
Mpwa usije ukaacha jeshi letu takatifu likaelekeza nguvu huko kuwa kuwa kuna intelijensia inaonyesha kuwa kutakua na Magaidi huko hahahahaa na ukasikia baadae tumeyaua magaidi 12, 27, 36 20 wakati wakurushiana risasi na Askari wetu watiifu
 
'Mchochezi' Tundu Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki. Ni Mbunge wa pekee wa upinzani wa jimbo kutoka Singida. Niko jimboni mwake kwa siku ya tatu leo. Najionea na kusikia.

Kwa kifupi,wana-Singida Mashariki wako na Mbunge wao. Wako pamoja na maono na mawazo yake. Wanatembea naye bega kwa bega. Wanafurahi na kusikitika naye.Maendeleo yanapiga hodi ya kasi. Yanawafunika wanajimbo na kuwapa faraja. Wananchi wana fikra mpya.

Cha kipekee kwa Lissu ni alivyojipanga jimboni kwake. Ana timu ya hamu na timamu. Ana wapokea malalamiko;wasikilizaji na wawasilishaji. Uwepo wake hapa,hukamilisha tu mfumo wa mfano alioujenga. Mfumo wake ni wa kupigiwa mfano.

Wana-Singida Mashariki wanafaidi demokrasia ya vyama vingi. Wanaonja changamoto za demokrasia na zinawakomaza kwa kusonga mbele. Najionea ya ndoto zangu za kinchi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Singida)
Lete data za uchaguzi uone alivyochomoka kwa bahati. Kuna wabunge wa jimbo na wabunge wa media. Fikiri
 
Ukubalikaji wake ndani ya jimbo lake hakupimwi kwa ngonjera ama kusikia sikia.Kipimo kizuri ni ushindi anaoupata dhidi ya wenzake kipindi cha uchaguzi.

Kwenye uchaguzi uliopita Tundu Lisu alisha kwa ushindi mwembamba sana.Sikufanikiwa kuweka maandishi lakini kwa kumbukumbu yangu yakichwani ushindi wake haukuzidi kura 3000.Ushindi wa namna hii huwezi sema huyu mtu amejipanga kwani naamini kama CUF wangesimamisha mgombea tusingekua naye Bungeni.

Kifupi naweza sema huyu ni mbunge wa taifa sio jimboni wake kwani inaonesha kukubalika kitaifa zaidi kuliko jimboni.
 
Kijana usiitukane CCM kuwa hutegemea wapinzani wagawane kura

Mzee Tupatupa
 
Back
Top Bottom