Jimbo la Singida Mjini, nani atusemee kero zetu bungeni?

Jimbo la Singida Mjini, nani atusemee kero zetu bungeni?

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Ndugu zangu mimi mzaliwa wa jimbo hili linaloongozwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji! Jamani mbona tunafanyiwa makusudi? huyu mbunge ana kazi gani bungeni? anamwakilisha nani?

Tuna matatizo lukuki..tatizo la Maji limekuwa sugu, yanatoka maeneo ya nyumba za vigogo tu! Hivi mpaka tutegemee wabunge wa viti maalum tuu ndo watusemee?

Kumbe kuna watu huomba ridhaa ya wananchi kufanikisha mambo yao ya kibiashara tu?Hili jimbo lipo kama vile limetelekezwa tu, wafanyabiashara TRA wanatusumbua wanakula rushwa muda wote hawataki kutusikiliza.
 
Hivi mlimchagua Dewji mkitegemea atakuwa na Muda wa ukaa bungeni? Aache kwenda kwene mikutano yake ya kumuingizia milions awasikilize nyie.
Endeleeni kuvaa kofia zenu na Kanga za CCM ambazo mumevaa miaka 5 bila kubadilishiwa. By the way anakuja tena mwaka huu na kofia Zaidi.
 
Sio huyo peke yake, Hata uku Mororgoro na Aboud wetu tumeshamchoka. Sijawahi kumsikia anaongea matatizo ya wananchi wake bungeni
 
Nyie miaka yote mnamchagua Dewji au sisiem na hali inakuwa hivyo.Atakuja tena kuwapa rushwa ya elfu 5 kwa 10 mtasahau hayo mtamchagua tena vumilieni mana mnafikiri mumekosa hizo huduma kwa mapenzi ya Mungu
 
Hivi mlimchagua Dewji mkitegemea atakuwa na Muda wa ukaa bungeni? Aache kwenda kwene mikutano yake ya kumuingizia milions awasikilize nyie.
Endeleeni kuvaa kofia zenu na Kanga za CCM ambazo mumevaa miaka 5 bila kubadilishiwa. By the way anakuja tena mwaka huu na kofia Zaidi.

Mkuu sio wote tulio mchagua yeye,Mimi niliyajua haya ndio maana sikupoteza kura yangu kwake.Katika maeneo ambayo upinzani uko kimya ni hapa Singida mjini.
 
mtalia machoz ya damu.
nyie mnamchagua billionea wa africa et awe mbunge wenu..
et aache kufuatilia mabilion yake akakalishe matako yake bungen kisa nyie mambululululaa.
 
Mkuu sio wote tulio mchagua yeye,Mimi niliyajua haya ndio maana sikupoteza kura yangu kwake.Katika maeneo ambayo upinzani uko kimya ni hapa Singida mjini.

Inawezekana wapinzani wameshawaona tatizo ndio maana wamewaachia huyo ili mjitambue kwanza.Hilo nalitarajia hata kwetu upinzani utakuja kututelekeza tujifunze kwa sababu ya unafiki wawatu wetu kuweka akiri mfukoni nakutumia matumbo zaidi.By the way nikupeni pole
 
Jiungeni pamoja kumtoa. Katiba ingeruhusu kumwajibisha mngefanya hivyo. Sasa kazi yenu ni kupigia hapana katiba pendekezwa
 
Alipokuwa anagawa sukari kg 2 na unga wa ngano pamoja na vjisenti watu wengi ( tena wale wa hali ya chini) walimshangilia sana Dewji wakidhani wamepata kumbe wamepatikana. Utajiri wa Dewji ni wake sio wa Singida mjini walitakiwa hilo walifahamu.
 
mtalia machoz ya damu.
nyie mnamchagua billionea wa africa et awe mbunge wenu..
et aache kufuatilia mabilion yake akakalishe matako yake bungen kisa nyie mambululululaa.
Mkuu huyu mfanyabiashara anabebwa sana na madiwani wake ambao anawakopesha hela, na wanajua akipotea watakosa ulaji.Hapa unakokosaea upinzani ni ngazi ya mitaa kukata mizizi yake ndo itakua dawa.
 
kamanda Vincent lissu anatosha singida mjini

Ndo nani huyo na chama gani mkuu? mbona hatumjui? Anatakiwa afanye mikutano tumjue asisubiri muda wa uchaguzi kama yule mwandishi wa Tanzania Daima!
 
alimradi anafanya yake hata mfanyaje kalaghabaho
 
Unauliza njaa Singida?? shauri yenu !! huku kwetu kuna bibi alipewa kanga mpya akapanda daladala tukamuuliza waliokupa hiyo kanga wanakusaidia nini ?? akasema amepata kanga na visenti vya kununua kaugoro akatuonyesha na ugoro ...tukamwambia dereva simama kuna mtu anakula ugoro anatemea watu humu ..tukamshusha
 
Waunganishe jimbo na lile la Lissu.Dewji siyo yule wa enzi za baba yao...hivi una habari hata kiswahili hajui siku hizi???
 
Ndugu zangu mimi mzaliwa wa jimbo hili linaloongozwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji! Jamani mbona tunafanyiwa makusudi? huyu mbunge ana kazi gani bungeni? anamwakilisha nani?

Mlichagua wenyewe na mkependa endeleeni kuchagua hivyo hivyo. Msitulalamikie kwa maamuzi yenu mabovu, badilikeni.


Tuna matatizo lukuki..tatizo la Maji limekuwa sugu, yanatoka maeneo ya nyumba za vigogo tu! Hivi mpaka tutegemee wabunge wa viti maalum tuu ndo watusemee?

Kumbe kuna watu huomba ridhaa ya wananchi kufanikisha mambo yao ya kibiashara tu?Hili jimbo lipo kama vile limetelekezwa tu, wafanyabiashara TRA wanatusumbua wanakula rushwa muda wote hawataki kutusikiliza.

Mlichagua wenyewe na mkipenda endeleeni kuchagua hivyo hivyo. Msitulalamikie kwa maamuzi yenu mabovu, BADILIKENI.
 
hameni mji ,karibuni kwenye majimbo ya wana mabadiliko mpate uwakilishi wa uhakika
 
Back
Top Bottom