Jimbo la Mtama Nape hali mbaya

Jimbo la Mtama Nape hali mbaya

Mkuu;

Kwa jinsi ninavyoelewa mimi, lile jimbo la Mtama mwenye mvuto mkubwa ni Mathew. Huyu alikuwa Diwani wa kata ya Vijibweni kigamboni kwa CCM, mwaka huu akaamua kwenda kugombea ubunge huko kwao Mtama. CCM wakamkata jina lake na kumpitisha Nape ambaye si mzawa wa Mtama. Hivyo wananchi walikuwa wanamtaka Mathew agombee kwa tiketi ya CCM, lakini baadaya matokeo ya kura za maoni. Wananchi wakamwambia mathew ajiunge na chama chochote nao watampigia kura huko. ndipo Mathew akajiunga na CHADEMA kisha wananchi walirudisha kadi za CCM zaidi ya wanachama 700.

Hivyo huko Mtama nape pamojana mgombea wa CUF wanajisumbua kwani mwenye mvuto kwa wananchi ni Mathew.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

mkuu huyu selemani Mathew aliwahi kucheza soka?
 
[h=3]CHADEMA NA UKAWA WABEBA WATU NA MALORI KUTOKA MIKOANI KWENDA DAR[/h]

11896043_439280776273482_620534892077090478_n.jpg

Hii nihatarisha Usalama wa Wananchi walio bebwa kwenye lori

11243638_1619925658277540_6823470039063086561_n.jpg

11951165_1619925731610866_2564080418381561796_n.jpg

Wana UKAWA wakisafirishwa kutoka Mikoani kwenda Dar

11904732_1619925878277518_193624351232439322_n.jpg

11954765_1619926598277446_7250682606156853672_n.jpg

Mkuu!!!!!!!!

Hivi magari ya matangazo ya mikutano unategemea wapande SISIMIZI au VIROBOTO!!!!!!

Tofautisha gari la matangazo na haya:-
 
Heshima wanajamvi.

Hali ya kisiasa ya mjumbe wa halmashauri kuu ambae pia ni MC aka msema chochote wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ni mbaya sana.Taarifa toka jimbo la Mtama zinadokeza Seleman Methew anaongoza kwa mbali sana huku Nape akiachwa nyuma sana.

Kura ya maoni iliyoendeshwa kwa mtindo wa Kariakoo style zimebaisha Seleman Methew anaongoza kwa 89% huku Nape akiambulia 7.5% tu.Tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni Nape amekuwa akisomba watu kutoka maeneo mengine kwa kuhofia mikutano yake kosa watu kabisa.

Tayari Nape amejindaa kwa maisha mapya nje ya siasa,anatarajiwa kujikita zaidi katika biashara hasa za uvuvi,sanaa atakiomba chama chake achukue mikoba ya Late Capt Komba na ushonaji wa sare za CCM chama kinachotarajiwa kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi mkuu 25/10/2015.

Nawasilisha.
mkuu umenichekesha,"msema chochote"hahahhahahaha, pamoja na mambo mengne mengi ila nepi, mwigulu na mzee wa pumba aka kigwangala ni moja yq watu wanaosababisha nisiikubali ccm hata kidogo
 
Mkuu Mnazi mmoja ipo Manispaa kwa hiyo no sehemu ya jimbo la Lindi mjini, Kiwalala mgombea wa CUF ndg Mchinjita ana nguvu, Mtama mgombea wa Chadema ndg Selemani ana nguvu na Nyangao & Nyengedi mgombea wa Ccm ndg Nape ana nguvu hizo ni sehemu za barabarani.
Shit! YOU'RE 100% RIGHT about Mnazi Mmoja... kwenye mgawanyo wa few years ago baadhi ya vijiji vya jimbo la Mchinga na Mtama viliingizwa Manispaa! Thank you.

Kuhusu nguvu za Mathew na Nape kwenye maeneo tajwa, nakubaliana na wewe na kiukweli, Mathew akikosa kura za kutosha hivi vijiji vya barabarani basi atakuwa na shida kubwa coz', mathalani ukitoka Nyengedi ukaingia ndani ndani... huko ndani unakuta vijiji zaidi ya vitano na vina wapiga kura wengi tu na ambako kimsingi ndiko asili ya Membe. Ukiacha hivi vijiji vya kuelekea nyumbani kwa Membe, kuna kata kama za Nyangamara,Mandwanga, Sudi,Nachunyu,Panagatena na zinginezo; ni ngumu sana hizi kuamini kwamba wameachana na maji ya bendera!
 
m 02:05 13th September 2015
Aliyekuwa mgombea wa CCM baada ya kukatwa kupitishwa Nape kinguvu, CCM ilibidi wavuruge kasi ya mgombea wa UKAWA kwa tiketi ya CUF Bw. Mchinjita kwa style ya kuhamia CHADEMA na kuchukua fomu za kugombea ubunge kwa lengo la kugawa kura "" imefahamika""wana Mtama zindukeni huu ni usanii.Tutaletewa Membe mwingine tukose maendeleo.tusipoteze muda na kampeni za CCM B.

kama kweli alitaka kuleta maendeleo Mtama asingehamia CHADEMA, wangeelewana na Bw Mchinjita iliwaunganishe nguvu sio kugawa watu halafu utegemee mabadiliko yatakuja.Tena UKAWA jimbo la Mtama wamelitoa kwa CUF sasa iweje mgombea wa CHADEMA kutoka CCM (baada ya kukatwa) achukue fomu kwa tiketi ya UKAWA CHADEMA.

Eti hoja ni wa cuf haaminiki anaweza uza jimbo acheni kutuchanganya. tunataka maendeleo. wana Mtama tusidanganyike.imegundulika jamaa baada ya kukatwa alionana na Pinda na CCM kupanga hiyo mbinu ya yeye kuhamia CHADEMA na kugombea lengo ni kugawa kura za upinzani ili Nape ashinde.hii imegundulika watafute ingine.Siasa ni mchezo mchafu Mchinjita piga kazi maendeleo kwanza majungu baadae. Mwaga sera za kuleta maendeleo wanamtama tupate kiongozi makini
Nape tunamtakia kila kheri aendelee kueneza CCM yake jimboni kunatakiwa maendeleo sio kuongea na waandishi.
kwani huyo Membe amefanya nn??
 
Jiulize kwanini CHADEMA WANABEBA WATU KUPELEKA KWENYE KAMPENI??

KAMA HUJUI
SOMA HAPO JUU

JUBEBA WATU NI STYLE YA CCM
STYLE YA KUSHINDWA SASA UNAKODI MAJESHI.

SASA
MATHEW IMEFAHAMIKA RASMI NI 'CCM B'.
LENGO KUGAWA KURA NAPE APITE.
LAKINI TUKO MAKINI

ISIHAKA MCHINJITA - MWALIMU MZOEFU.KIJANA SHUPAVU. MZAWA WA MTAMA.
MLETA MAENDELEO. ANAYEJALI WANANCHI. SIO MCHUMIA TUMBO

ANAKUBALIKAAAAAAAS NA TUTAMCHAGUA.

TAHADHARI: TUSIDANGANYIKE WANA MTAMA.
 
Heshima wanajamvi.

Hali ya kisiasa ya mjumbe wa halmashauri kuu ambae pia ni MC aka msema chochote wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ni mbaya sana.Taarifa toka jimbo la Mtama zinadokeza Seleman Methew anaongoza kwa mbali sana huku Nape akiachwa nyuma sana.

Kura ya maoni iliyoendeshwa kwa mtindo wa Kariakoo style zimebaisha Seleman Methew anaongoza kwa 89% huku Nape akiambulia 7.5% tu.Tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni Nape amekuwa akisomba watu kutoka maeneo mengine kwa kuhofia mikutano yake kosa watu kabisa.

Tayari Nape amejindaa kwa maisha mapya nje ya siasa,anatarajiwa kujikita zaidi katika biashara hasa za uvuvi,sanaa atakiomba chama chake achukue mikoba ya Late Capt Komba na ushonaji wa sare za CCM chama kinachotarajiwa kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi mkuu 25/10/2015.

Nawasilisha.

Huyu akatafute kazi za u mc kama wenzie akina MC pilipili na yeye atakuwa MC nape
 
Makubaliano safiiiiiiiiiiii

Sasa maendeleo tu
 
Ukweli upo au ni changa la mtandao.

Tuwe makini
 
Hatimaye wagombea ubunge Upinzani Mtama wamaliza tofauti zao

Na.Ahmad Mmow, Lindi.

Wagombea wa ubunge katika jimbo la Mtama, wilaya ya Lindi vijijini, kutoka katika vyama vilivyopo kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA), Isihaka Mchinjita(CUF) na Seleman Methew(CHADEMA) wamemaliza tofauti zao zilizotokana na mgogoro wa kugombea jimbo hilo.

Mgogoro ambao ulianza kuwagawa wafuasi wa wagombea hao kiasi cha pande hizo kutuhumiana kutumiwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Wakizungumza baada ya kikao kirefu cha ndani kilichofanyika katika kijiji cha Kiwalala kwenye ukumbi wa kanisa la Romani Katoliki, mbele ya wafuasi na wanachama wa vyama hivyo waliokuwa wanasubiri kusikia yaliyofikiwa kwenye kikao hicho.

Wagombea hao walisema wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kubaini mgogoro huo utakipa nafasi Chama Chama Mapinduzi kushinda uchaguzi katika jimbo hilo.

Isihaka Mchinjita alisema mgogoro huo ungekinufaisha CCM bila wao kujua kwamba wanakinufaisha chama hicho wakati wanasubiri tamko toka kwa viongozi wa juu wa vyama vyao la kumtangaza kati yao kuwa mgombea.

Alisema kwa kuwa wao ndio waathirika wa mgogoro huo, ndipo wakaamua kutafuta muafaka ambao utasaidia kupambana kwa pamoja kuiondoa CCM katika jimbo hilo, badala ya kuendelea kuhasimiana.

"Tuliyokubaliana ni mambo mazuri ambayo yamezingatia maslahi ya vyama vyote viwili, tamko rasmi la tuliyokubaliana tutalitoa kwapamoja kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 29 mwezi huu," alisema Mchinjita.

Selemani Methew, alisema "ilikulinusuru jimbo lisiangukie mikononi mwa CCM wameamua kufanya jambo ambalo litasababisha lichukuliwa na chama cha upinzani."

Hatuwezi kuendelea kugawanywa wakati lengo letu ni kudiliti CCM(kukifuta Chama Cha Mapinduzi), tulieni wananchi, tuliyokubaliana yanania mzuri mtayafurahia,"alisema Methew.

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Lindi vijijini, Chikawe Namkaa, alisema wamefikia uamuzi huo ili kurejesha amani katika jimbo hilo kutoka kwenye uhasama uliokuwa na pande tatu. Alisema hali ya usalama katika jimbo hilo imeanza kuwa tete kwa baadhi ya wanachama na wafuasi wa chama chake kuwindwa na kupigwa.

"Mahasimu walikuwa wanatumia mgogoro baina yetu kuwapiga wafuasi wetu nyakati za usiku wakijificha nyuma ya mgogoro huu,"alisema Namkaa.

Mwenyekiti huyo alisema watashirikiana na CUF kuweka ulinzi iliwafuasi wapande zote mbili wasidhuriwe na wafuasi wa vyama ambavyo wagombea wake waubunge wanajua hawatashinda na kuamua kukodi wahuni kwenda kuwapiga na kuwatisha wanachama wa chama hicho.

"Tumeondoa tofauti zetu, natutashirikiana katika suala zima la ulinzi, lakini pia makubaliano haya yamefungua mlango wa kutokea ccm kwenye madaraka katika jimbo hili," aliongeza kusema Namkaa.

Mazungumzo ya wagombea hao yaliongozwa na maofisa wa kutoka makao makuu. Ambapo kwa upande wa CUF uliwakilishwa na katibu mkuu wake wa jumuia ya wanawake, Fatma Kalembo, na CHADEMA kiliwakilishwa na Oliver Mwinuka. ambaye ni mratibu wa mikutano na misafara ya mgombea mwenza wa urais kupitia UKAWA, Juma Duni.

source. LindiYetu
 
m 02:05 13th September 2015
Aliyekuwa mgombea wa CCM baada ya kukatwa kupitishwa Nape kinguvu, CCM ilibidi wavuruge kasi ya mgombea wa UKAWA kwa tiketi ya CUF Bw. Mchinjita kwa style ya kuhamia CHADEMA na kuchukua fomu za kugombea ubunge kwa lengo la kugawa kura "" imefahamika""wana Mtama zindukeni huu ni usanii.Tutaletewa Membe mwingine tukose maendeleo.tusipoteze muda na kampeni za CCM B.

kama kweli alitaka kuleta maendeleo Mtama asingehamia CHADEMA, wangeelewana na Bw Mchinjita iliwaunganishe nguvu sio kugawa watu halafu utegemee mabadiliko yatakuja.Tena UKAWA jimbo la Mtama wamelitoa kwa CUF sasa iweje mgombea wa CHADEMA kutoka CCM (baada ya kukatwa) achukue fomu kwa tiketi ya UKAWA CHADEMA.

Eti hoja ni wa cuf haaminiki anaweza uza jimbo acheni kutuchanganya. tunataka maendeleo. wana Mtama tusidanganyike.imegundulika jamaa baada ya kukatwa alionana na Pinda na CCM kupanga hiyo mbinu ya yeye kuhamia CHADEMA na kugombea lengo ni kugawa kura za upinzani ili Nape ashinde.hii imegundulika watafute ingine.Siasa ni mchezo mchafu Mchinjita piga kazi maendeleo kwanza majungu baadae. Mwaga sera za kuleta maendeleo wanamtama tupate kiongozi makini
Nape tunamtakia kila kheri aendelee kueneza CCM yake jimboni kunatakiwa maendeleo sio kuongea na waandishi.
kwani huyo Membe amefanya nn??[/QUpo

pole gamba
 
Mnaandika lakin kwa alichokifanya jana Nape viwanja vya Sokoni..?
 
Kinachompunguzia Nape wasiwasi wa kishindwa ni kwasababu kuna wagombea wa Cuf na Chadema.
 
Back
Top Bottom