Jimbo la Magu ni kama halina mwakilishi Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jimbo la Magu ni kama halina mwakilishi Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LULENGO, Mar 25, 2012.

 1. L

  LULENGO Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni takribani miaka miwili sasa tangu kufanyika uchaguzi mkuu wa Rais ,mbunge na diwani inchini,lakini huwezi amini Mtanzania, mbunge wa jimbo la Magu mkoani Mwanza CCM hajawahi kuchangia,kutoa mada,kuhoji,wala,kukumbushia mambo mbalimbali yanayohusu wanainchi na wapiga kura wake.kuna ahadi kibao aliahidi faatilia hakuna hata moja walau aliianzisha,ahadi ya ujenzi wa bwawa kubwa la maji kijiji cha Jinjimili,majengo mawili ya madarasa Jinjimili,Mradi wa umeme kutoka JIneri la Pamba Kasori kupita Kabila hadi Mahaha pia bei ya Pamba ilihari yeye ndiye Mwenyekiti wa Board hiyo na pia ujenzi wa Minara ya Simu maeneo mbalimbali ya JIMBO na upelekaji wa Maji mjini Magu. Wapi, Wapi Mbunge hata kuongea tu,hoi kazi kupiga makofi bungeni na kuunga mkono hoja za wengine, Mjadala wa katiba ulikuwa hot sana pale MJENGONI lakini jamaa kamwe hakuongea hata, kana kwamba katiba inayoundwa haiwagusi wakaazi wa JIMBO hilo,Hii ni Hasara nyingine kwa Jimbo la Magu.Ni Muda wa kutafakari uwepo wa Mbunge kama huyo na pia kuitumia fursa hii vizuri wakati ukifika,Siyo Kupokea kanga,sabuni,na vijisenti wakati mhimu kama wa uchaguzi unapofika.Nawasilisha Kamanda Kutoka JINJIMILI.
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kwa hiyooooooo?
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  mtoeni kama rais wa Tunisia. kwanini hamkuchagua wa CDM akawashe cheche bungeni? shauri yenu tena nataka alale mwaka mzima ilimkome kuchagua mtu kwa kanga na sukari ya siku moja halafu mnataabika miaka mitano
   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Card yako ya kupigia kura unayo? kama ndivyo basi itunze mwaka 2015 ntakufundisha cha kufanya kuliko huo upuuzi mlioufanya hapo 2010
   
 5. Guma Mlugaluga

  Guma Mlugaluga Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mtaje kwa jina kuliko kumuweka kwenye mabano
   
 6. Guma Mlugaluga

  Guma Mlugaluga Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli una hasira, badala ya kuandika Magu umeandika Mgu!
   
 7. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni dr festus limbu. kuna uzi mwingine unaomhusu hivi sasa humu jamvini. bora mods waziunganishe.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Binafsi sijawahi kuyachukulia majimbo yalo wachagua wabunge wao kupitia CCM kama wanao wawakilishi wa kutatua matatizo yao!!!!! na kuwawakilisha wapiga kura wao!!!!
   
 9. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mwingne anaitwa dr. Mahenge hamna tofauti na huyo sema huyu jimbo lake ni makete.
   
 10. M

  MWINUKA E Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Majimbo yote ambayo wagombea wa CCM walipita wananchi toka majimbo hayo hawana wawakilishi bungeni. Mfano jimbo linalopakana na Magu la Bunda utasema wana muwakilishi bungeni? lingine ni jimbo la mtera ni kama halina muwakilishi bungeni. Any way kwa sababu siku zote kuanza upya si ujinga, 2015 itabidi kuanza upya.
   
 11. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huyo jamaa waga ni zoba sana
   
Loading...