Jimbo la Dr.Slaa baada ya Uchaguzi wa Mitaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jimbo la Dr.Slaa baada ya Uchaguzi wa Mitaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Nov 5, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuna mwanachama kaja hapa na kubeza kazi ya Slaa na kusema yeye mwenyewe katangaza kwamba hajapata serikali ya mtaa hata moja kwenye jimbo lake . Habari hizi ni za uongo mkubwa . Mimi naongea tokea Arusha na katika matokeo ya hayo Karatu iko Mkoa wa Arusha .Matokeo sahihi yanaonyesha kwamba jimbo zima CCM walipaata viti 6 pekee na Slaa aliendelea kuwamaliza pamoja na camps zao na wakubwa na mapesa kumwagiga . Mkija na hoja za kipuuzi muwe mnachuja maana hapa ni JF jamani .

  nawakilisha .
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mambo haya kiongozi ndo yananitamanisha nijiondoe humu JF ni ujinga mtupu
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kigogo usijiondoe ila ujue kwamba JF imevamiwa baada ya CCM kuona kwamba JF ina sent agenda .Kazi yetu sisi ni kuonyesha ukweli kila mara . Kuna kibao baada ya watu kuvamia hala lakini we will not be swayed tutasimama na kuwapa ukweli . Mtu anaongopa eti Jimbo la Slaa hajapata kiti hata kimoja . Ujinga mtupu . Muulizeni Makamba ama aliaga wakati anaondoka . Ngoma ilikuwa kama tarime .
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lunyungu

  What is your point here? Mbunge wa Karatu ni Dr Slaa huna haja ya kutoa mshipa wa shingo kuthibitisha hilo.
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..na wewe njoo na Data kamili sio roborobo hizo ambazo zinaonyesha habari nzima ni majungu tuu,tuambie CCM ni viti vingapi na sehemu wanazoshikiria na upinzania ni viti vingapi na wapi wanaposhikiria na majina ya hao madiwani kama inawezekana na utuambie before/after number zimebadilika vipi...hope hii sio ngumu sana maana kama unajua hizo ndio info za mtu anayejua la sivyo potea na usituletee robo habari zako zisizoeleweka!
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Unaweza kuchangamsha akili nawe ukapata habari hizi si kazi ngumu nilicho kifanya mimi ni kukata uongo mweupe juu ya Slaa na kupoteza mitaa yote jimboni kwake . Nimesema CCM wana mitaa 6 pekee na huu ndiyo ukweli mengine unaweza kuyatafuta .

  Masatu ume miss point mkuu kasome tena nimesema nini juu kabla ya kunirukia kaka .
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Lunyungu,bado uanturudisha kulekule kwa mtoa habari wa awali.Cha msingi leta Data kamili,tuambie katika wilaya ya Karatu CHADEMA wamepata kura kadhaa,CCM kura kadhaa,CUF kura kadhaa nk.Unaweza ukawa upo Arusha lakini ukawa huna Data kamili za huko Karatu.Cha msingi tuletee Data zilizo kamilika badala ya kusema tu kwamba CCM wamepata mitaa 6(na CaHADEMA je,wamepata vingapi??)...Yule mtoa habari wa kwanza alionesha wazi kakurupuka(sababu ana mahaba na CCM) naw wewe isije ukaonekana unajibu mapigo(sababu una mahaba na CHADEMA?)...Ni hayo tu mkuu wangu..Pa1
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  CHADEMA yawa kisiki cha mpingo kwa CCM Karatu

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu, Arusha​
  Oktoba 28, 2009 [​IMG] [​IMG]Wananchi wahoji: Kama Karatu yawezekana, vipi kwingineko?
  HATIMAYE pazia la uchaguzi wa serikali za mitaa lilifungwa Jumapili iliyopita baada ya kampeni za uchaguzi huo zilizochukua siku 10 kuhitimishwa siku ya Jumamosi ya Oktoba 24.
  Kama ilivyotarajiwa na wengi, pamoja na idadi ndogo ya watu waliojitokeza na kujiandikisha kupiga kura, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na ushindi mkubwa kwa kuzoa viti vingi vya ngazi ya vitongoji, mitaa na vijiji kutokana na kusimamisha wagombea wake kwa karibu asilimia 100.
  Vyama vya upinzani vyenye majina makubwa kama NCCR Mageuzi, CHADEMA, CUF na TLP kwa ujumla wao vilishindwa kabisa kusimamisha wagombea wao katika maeneo mengi na kufanya wagombea wengi wa CCM kupita bila kupingwa.
  Ni Katika wilaya ya Karatu pekee ambapo CHADEMA kilisimamisha wagombea katika vitongoji vyote 138 na vijiji 44 vya wilaya hiyo vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria.
  Na hata macho ya Watanzania wengi yalielekezwa katika wilaya hiyo baada ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya CCM na CHADEMA kwenda kupiga kampeni katika wilaya hiyo kuwanadi wagombea wao.
  Kwa upande wa CCM kampeni yake iliongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Yusuf Makamba akisaidiana na Katibu wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda na wale wa wilaya ya Karatu wakati CHADEMA kampeni yake iliongozwa na Katibu Mkuu wake Dk.Wilbroad Slaa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Karatu.
  [​IMG]

  Mbunge wa Karatu, Dk. Wilibroad Slaa
  CHADEMA pia ilitumia helikopta mpya ya Mbunge wa Moshi vijijini, Philemon Ndesamburo kuwavuta wapiga kura katika siku ya mwisho ambapo walifanya mikutano ya kampeni katika vijiji zaidi ya 20.
  Mikutano hiyo ilifanyika katika wilaya za Hai, Moshi mjini, Mwanga, Same na Karatu huku viongozi wakuu wa chama hicho, Freeman Mbowe, Ndesamburo na Dk.Slaa wakihutubia kuwanadi wagombea wao.
  Katika wilaya ya Karatu ambapo CCM huchukuliwa kama cha upinzani baada ya CHADEMA kutawala na kuongoza jimbo hilo kwa takaribani miaka 14 sasa, uchaguzi huo ulikuwa unachukuliwa kama kipima joto cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
  Hadi juzi Jumatatu usiku wakati habari hizi zikiandaliwa, kwa mujibu wa matokeo yasiyo rasmi, CHADEMA kilikuwa kimeibuka na ushindi mkubwa katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Karatu kwa kuibuka na ushindi katika mitaa 21 kati ya mitaa 28 huku CCM ikiambulia mitaa 6 na NCCR-Mageuzi ikiibuka mshindi wa mtaa mmoja.
  Matokeo hayo ya Mamlaka ya Mji wa Karatu ni salamu tosha kwa CCM kuhusu mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa mwakani na ni wazi kuwa chama hicho kikongwe bado hakijapata tiba au dawa ya uhakika ya kuishinda CHADEMA katika wilaya ya Karatu.
  "Hadi hapa unaponipigia simu ni kwamba CHADEMA wameshinda mitaa 21 ya Mamlaka ya Mji wa Karatu huku CCM ikipata viti 6 na NCCR-Mageuzi kiti kimoja…lakini bado tunakusanya matokeo kutoka vijiji vingine vilivyoko nje ya mji na matokeo ya jumla yatangazwa kesho (Jumanne) saa nne asubuhi", alisema mmoja wa wasimamizi wasadizi wa uchaguzi huo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
  Msimamizi huyo alieleza kuwa matokeo hayo yamechelewa kutokana na jiografia ya wilaya hiyo ambapo baadhi ya vijiji viko mbali sana na makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya na pia zoezi la kuhesabu kura katika vijiji kadhaa limechelewa kutokana na ugumu katika kujumlisha kura za wajumbe wa halmashauri za vijiji.
  "Kuna tatizo kubwa katika zoezi la kuhesabu kura za wajumbe wa serikali za vijiji kutokana na upigaji kura kuendeshwa na kwa wapiga kura kuandika majina ya wagombea wanaowapigia badala ya utaratibu uliozoeleka wa wapiga kura kuweka alama ya vema kwa mtu anayempigia kura", alisema msimamizi huyo.
  [​IMG]

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Massay
  Akizungumza juzi jioni, mmoja wa maafisa na mratibu wa shughuli za uchaguzi kwa upande wa CHADEMA, Lazaro Massay alieleza kuwa hadi jana jioni chama chake kilikuwa kinaelekea kushinda katika maeneo mengi.
  "Tumezoa asilimia 90 ya viti katika Halmashauri ya Mji wa Karatu na katika vijiji vingine tunaongoza kwa kura nyingi ingawa kumekuwa na matatizo katika zoezi la kuhesabu kura kutokana na utaratibu mbovu wa uchaguzi huu", alisema.
  Massay, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, alisema kwa ujumla uchaguzi huo uligubikwa na dosari nyingi na chama chake kimepata viti hivyo katika mazingira magumu sana.
  Alisema miongoni mwa dosari hizo ni vitisho kutoka kwa viongozi wa CCM kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo wakiwataka kukisadia chama hicho tawala kwa hali na mali; vinginevyo wangechukuliwa hatua za kinidhamu.
  "Viongozi wa CCM wamekuwa wanapita katika vituo vya kupigia kura wakati zoezi la upigaji kura likiendelea na wamekuwa wanawatisha wasimamzi kuwa waisadie la sivyo watahamishwa katika maeneo ya kazi kama walivyofanya kwa Mkurugenzi wa Halmashauri", alieleza Massay.
  Alisema dosari nyingine ni utaratibu wa kupiga kura kwa kuandika majina 12 ya wajumbe wa serikali ya mtaa na kundika pia ya mgombea unayempigia kura; hivyo kuwachanganya wapiga kura hasa wale ambao hawajui kusoma na kuandika.
  "Kwa kweli moja ya dosari ambayo imechangia sana kuvuruga zoezi la upigaji kura ni utaratibu huo ambao ulikuwa mgumu sana kwa baadhi ya wapiga kura na mawakala wa CCM walitumia udhaifu huo kuwashawishi wapiga kura wakati zoezi la upigaji likiendelea", alisema.
  Alisema kuwa utaratibu huo ni mpya na ulikuwa haufahamiki miongoni mwa wapiga kura na ingekuwa vizuri ukatumika ule wa zamani wa kuweka alama ya vema chini ya jina la mgombea anayepigiwa kura.
  Alisema dosari nyingine ni mbinu chafu za CCM ambapo siku moja kabla ya uchaguzi huo walisambaza vikaratasi vilivyokuwa vinaeleza kuwa wagombea wetu wengi wamejitoa katika uchaguzi huo hivyo kuwachanganya wapiga kura.
  Juzi Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Wilbroad Slaa alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa uchaguzi huo unafanyika bila kufuata kanuni na sheria zinazotawala sheria za uchaguzi na waliokiuka taratibu hizo walikuwa na lengo la kuhujumu uchaguzi ili kukinufaisha Chama Cha Mapinduzi.
  "Kwa kweli sheria zimekiukwa na wagombea wameenguliwa bila sababu katika maeneo mengi nchini….hapa jimboni kwangu Mkurugenzi wa Halmashauri amehamishwa bila sababu na waziri mwenye dhamana (Celina Kombani) ambaye alipiga simu wilayani mwenyewe ikiwa siku moja tu kabla ya uchagzuzi. Sasa maana yake ni nini?", alihoji Dk.Slaa.
  Habari zisizothibitishwa zilieleza kuwa Mkurugenzi huyo aliondolewa baada ya viongozi wa CCM wa ngazi ya wilaya na mkoa kumlalamikia Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba kuwa hana "msaada" kwao na mara nyingi ameshindwa kutekeleza yale anayoagizwa na viongozi hao.
  [​IMG]

  Waziri wa TAMISEMI, Celina Kombani
  Baada ya "zengwe" alichofanya Makamba ni kuwasiliana na Waziri wa TAMISEMI, Celina Kombani ambaye alipiga simu na kutoa agizo la kuhamishwa mara moja kwa Mkurugenzi huyo ili kupisha uchaguzi ufanyike.
  Hata hivyo, Waziri Kombani amekana Mkurugenzi huyo kuhamishwa kwa sababu za uchaguzi na ameeleza kuwa uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida kutokana na mtumishi huyo kusumbuliwa na matatizo ya afya kutokana na kuugua mara kwa mara.
  Viongozi wa CCM mkoa wa Arusha na wale wa wilaya ya Karatu jana walishindwa kupatikana kueleza uchaguzi huo kwa upande wao ambapo habari zilizopatikana zilieleza kuwa hawakutegemea matokeo ya mitaa ya Mamlaka ya Mji wa Karatu kuwa mabaya kwao kiasi hicho.
  Raia Mwema ilipowasiliana na Katibu wa Mkoa kwa simu yake ya mkononi ilikuwa imefungwa muda wote wakati Katibu Msaidizi, Bilal Omar alieleza kuwa hakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia uchaguzi huo.
  "Wacha tu tusubiri matokea ya jumla. Mimi sina hakika ya vijiji na vitongoji tulivyoshinda na kushindwa", alisema Bilal kwa mkato.
  Chaguzi zote katika wilaya hiyo ya Karatu zimekuwa na ushindani mkali tangu mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1995 na kwa kipindi chote CHADEMA imekuwa ikiishinda CCM katika chaguzi hizo ingawa chama hicho tawala kimekuwa kikifanya jitihada na mbinu mbalimbali kulikomboa jimbo hilo lakini bila mafanikio.
  Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa mkoa wa Arusha waliohojiwa na gazeti hili kuhusu matokeo hayo, walihoji ni kwa vipi ni wilaya ya Karatu tu ndiyo inayoweza kuikabili ipasavyo CCM katgika chaguzi nchini.
  "Kama wilaya ya Karatu wanaweza kuitingisha CCM kiasi hicho, ni kwa nini wilaya nyingine nchini zisiweze? Ni kwa nini wasijifunze kutoka Karatu?", aliuliza Israel Akunay wa mjini Arusha.

  [​IMG]
   
 9. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utaondoka lini mkuu? Unataka nauli?
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yaani umemchoka kiasi hicho?
   
Loading...