Jimbo la Busega sasa CCM Kwaheri

Jimbo la Busega sasa CCM Kwaheri

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
7,452
Reaction score
3,073
Busega jimbo ambalo lilikwa wilaya ya Magu sasa ni wilaya kamili, DC Paul Mzindakaya, kijana wa CCM ambaye baba yake amekula nchi akashiba sasa ni zamu za watoto wa wakubwa kuanza kujengewa misingi ya kututawala milele. Jimbo la Busega kutoka kwa Chegeni hadi kwa binamu yake Kamani, sasa halitakuwa chini ya CCM tena. Sababu ni nyingi lakini moja ni kushindwa kufanya au kushawishi maendeleo kwa wanandugu hao wawili yaani Chegeni na Kamani. Nyingine ni ugomvi wote ambapo vile wanafahamiana sana na kujua sana wametiana madoa makubwa, tatu ni ukweli kwamba vijana wa nassa waliamka siku nyingi wakawapa wenyeviti wa kijiji wapinzani wengi sana Busega licha ya CDM kuwa juu hivi karibu, pia CUF and UDP wako katika hali ya kuwepo na sio goigoi. VIJANA wanaotaka mabadiliko wako wengi, Yuko Meya wa jiji la Mwanza Mabula, ambaye yeye ni wa CCM kitu ambacho kitampa wakati mgumu kuwashawishi wajanja wa nassa wampe jimbo, Yupo Meneja wa Telecentre ya Kwanza Tanzania Bwana LONGO, Yupo Moses Masunga Kijana machachali na mwandishi wa habari mkongwe sasa, wapo vijana wengi ambao kwa kweli nguvu wanazo na CHADEMA sasa iko juu kuliko wakati mwingine BUSEGA, Swali ni je Kamani na Paul Mzindakaya wataweza kuzuia nguvu za vijana wasomi ambao pia wanakubalika na wakazi wa Busega??? CCM BUSEGA BYE BYE.
 
jibu ni CCM izikwe popote TZ i hate ccm
 
... DC Paul Mzindakaya , kijana wa CCM ambaye baba yake amekula nchi akashiba sasa ni zamu za watoto wa wakubwa kuanza kujengewa misingi ya kututawala milele. ...
Huyo jamaa aliiba sana vocha za pembejeo kule S'wanga. Nashangaa Rizwan akalipeleka jina lake kwa mshua ili awe DC, na akawa!
 
siyo hayo tu no mengi mno maovu ya ccm jumbo LA busega,Luna Kijana machachari wa nyangili no mwanasheria nae analiwania jimbo hilo name morali uko
juu sana.
 
magamba yanapumua kwa msaada wa machine,hata huko nyumbani magu 2015 byebye
 
siyo hayo tu no mengi mno maovu ya ccm jumbo LA busega,Luna Kijana machachari wa nyangili no mwanasheria nae analiwania jimbo hilo name morali uko
juu sana.
 
Dah pale ni kwetu kama kuna mbunge aliyewah kuwa mbunge ni siye mkubali basi Chegeni hapana.....Ni kwel maendeleo bado
 
Wana BUSEGA tumpeni kampani ya kutosha kijana huyu kutoka Kijiji cha JISESA/NGASAMO ali maarufu kwa jina la NGEREJA aweze kupeperusha bendera ya CDM Mwaka 2015.Hii ni kwa mustakabali wa maendeleo ya jimbo la BUSEGA.Huyu jamaa ni mpigania haki wa kweli na si mchumia tumbo kama CHEGENI na mwenzake aliyepo sasa hivi.Kwa wale mliosoma pale UDSM kwenye miaka ya 2002 hadi 2005 mna weza mkawa mashuhuda wangu wazuri sana wa jinsi alivyokuwa machachari katika kupigania haki za wanachuo pale UDSM.
 
Hapana , mimi siungi mkono kuwatimua ccm nchi nzima , itawezekanaje cdm kuendesha nchi bila upinzani imara ?
 
Wewe Ntemi wa Nassa a.k.a WILLA utakuwa mwongo, maccm bado yana nguvu sana huko na yataendelea kutukung'uta mpaka tukome. Yana mpango wa kumsimamisha msomi m1 yuko TRA wa pale Nyakaboja! Naamini vijana wa Nassa wengi watamwunga mkono ukizingatia kwamba Nassa ya ukanda wa ziwani hawajawahi kutoa Mbunge! Sasa wanasema ni zamu yao!
 
Wewe Ntemi wa Nassa a.k.a WILLA utakuwa mwongo, maccm bado yana nguvu sana huko na yataendelea kutukung'uta mpaka tukome. Yana mpango wa kumsimamisha msomi m1 yuko TRA wa pale Nyakaboja! Naamini vijana wa Nassa wengi watamwunga mkono ukizingatia kwamba Nassa ya ukanda wa ziwani hawajawahi kutoa Mbunge! Sasa wanasema ni zamu yao!

itakuwa zamu yao kusimamisha mgombea, lakini itakuwa zamu ya CHADEMA kutupatia mbunge.
 
Hivi kuna mtu anafanyakazi TRA anaweza kuwa mwadilifu, Maana CDM sio kokolo hata kidogo, we can not replace what we have with what is what we have.
 
Mkuu fikirikwanza,
Naunga mkono hoja! Kiukweli jimbo la Busega na jirani yake Magu (kwa dr. Festus Limbu) yamekosa wawakilishi makini kwa miongo kadhaa sasa. Kibaya zaidi siasa za ndani ya ccm katika majimbo haya zimegubikwa na fitina, chuki, ushirikina na kutishiana maisha zaidi kuliko kuwatumikia wananchi waliowachagua. Kwa mara ya mwisho anglau majimbo hayo yalikuwa na wawakilishi wakati wa marehemu Ernest Kisumo Nyanda (Busega) na marehemu Malaki Levi Lupondije (Magu). Baada ya hapo kwa kweli, hatujawahi kupata wawakilishi bungeni.

Sasa ni wakati muafaka kwa wana Busega na Magu kufanya mabadiliko ya kweli kwa maendeleo ya majimbo haya, na Taifa kwa ujumla. Inasikitisha kuona rasilimali nyingi katika maeneo haya lakini wananchi wanaishi katika umaskini mkubwa huku huduma muhimu za jamii zikiwa katika hali mbaya sana. Wakati serikali inapeleka maji kutoka ziwa victoria kwenda miji ya shinyanga na kahama, wananchi wengi wa Magu na Busega hawana maji safi na salama katika vijiji vyao. Wengi wao wanakunywa na kufanya shughuli za usafi ziwani, kitu ambacho ni hatari kwa afya zao. Wakati wa kiangazi kuna wananchi wanaolazimika kutembea kilometa kadhaa kufuata ndoo moja ya maji ziwani na kufanya shughuli za usafi huko. Wabunge wetu wanaishi Dar es Salaam! Wakienda Dodoma wanadai walipwe laki 200 maana maisha yamepanda!

Uvuvi ambayo kwa miaka mingi ndiyo ilikuwa shughuli muhimu kwa vijana wa Magu na Busega, sasa sio shughuli halali tena kwa vijana hawa na imezaa msamiati mpya...wavuvi haramu!. Pamba ambayo kwa miongo kadhaa ndio lilikuwa zao kuu la biashara, sasa ni zao kuu la hasara. Kibaya zaidi mwenyekiti wa bodi ya pamba ni mbunge wa Magu (dr. Limbu) aliyesomeshwa kwa hela ya pamba kama ambavyo wengi wetu tulivyosomeshwa, lakini hajaonyesha juhudi zozote za kunusuru kilimo na soko la pamba kwa ujumla wake.

Natambua matatizo kama haya yanaikabili sehemu kubwa ya nchi yetu, ila hapa nimeaandika kizalendo zaidi kama mwananchi, mzaliwa, mpiga kura na mfuatiliaji wa karibu wa siasa za Busega na Magu, ambazo awali ilikuwa wilaya na jimbo moja la uchaguzi (Magu). Sina uhakika kama bw. Longo naye anapigia kugombea ubunge, ngoja nimtafute kwa habari zaidi.
 
NBi bora kama wameamka toka usingizini.CCM ni janga
 
Heli uwe mtumwa wa mzungu kuliko kuwa mtumwa wa CCm, maana CcM wana angamiza Taifa! Vijana kwa kukosa elimu bora na maisha bora, wamekuwa malofa wanaohongwa T-Shirt na kapelo wanasahau kuwa umasikini wao umesababishwa na CcM. Wanaogelea kwenye lindi la ujinga na umasikini, hawaelewi wajibu wa serikali kwao nini, wanahangaika kila siku kutafuta mkate wa kila siku kwa jasho na mbinu zao wenyewe. Ccm inatuma vijana waliowavalishwa nguo za migambo kuwa vuruga vijana wenzao wasitafute pesa bali waendelee kuwa malofa ili iwe rahisi kuwadhibiti. Nassa ni sehemu kavu sana, vijana wamekwama kimaisha, hawawezi kujikwamua kimaendeleo, wakiwa na njaa wanawaza vizuri lakini Ccm ikija na TOT na kofia na jero jero, wanasahau kila kitu wanasombwa na mabasi kama dagaa na mwisho wa siku wanapigia kura magamba! Njaa mbaya Nassa hamuwezi kujikomboa mpaka mjitambue na mbadilike wote!
 
Wewe Ntemi wa Nassa a.k.a WILLA utakuwa mwongo, maccm bado yana nguvu sana huko na yataendelea kutukung'uta mpaka tukome. Yana mpango wa kumsimamisha msomi m1 yuko TRA wa pale Nyakaboja! Naamini vijana wa Nassa wengi watamwunga mkono ukizingatia kwamba Nassa ya ukanda wa ziwani hawajawahi kutoa Mbunge! Sasa wanasema ni zamu yao!

Ebana yule jamaa mi nitampa kula anaitwa Kadashi si mchoyo ni mtu Safi maana hata hizi njaa njaa hana.
 
Chadema ichukue jimbo la busega? Chadema ipi hii ya wachaga wapenda majungu wauaji wa chacha zakayo na legia mtema wasiopenda kuona mwanasiasa anapendwa ndani ya chadeama kama siyo mchaga walioshindwa kufanya uchaguzi wa ndani wa chama, ambao wabunge wa viti maalumu ni watoto wa viongozi wa chadema, mahawara zao binamu zao au chadema nyingine itakayo toka mbinguni? Mtasubiri sana mtasema sana lakini subiri 2015 mtapata kilicho mpata Raila kenya mnachonga sana ila naamini mtanyamaza tu muda siyo mlefu,
 
Back
Top Bottom