GE2025 Jimbo Katoliki Bagamoyo latangaza kuwaombea marehemu pamoja na Majeruhi siku ya 13/11/2025, waliotokana na uchaguzi mkuu

GE2025 Jimbo Katoliki Bagamoyo latangaza kuwaombea marehemu pamoja na Majeruhi siku ya 13/11/2025, waliotokana na uchaguzi mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Kufuatia Vifo Vilivyotokea Wakati wa Kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025 nchini Tanzania
Mhashamu Stephano Lameck Musomba OSA, Askofu wa Jimbo Katoliki Bagamoyo Amewaomba na kuwaalika Mapadre, WATAWA, Waamini na Wote wenye Mapenzi Mema Tarehe 11/11/2025 Iwe ni Siku Maalumu ya Kuwaombea Marehemu wote waliofariki Katika Kipindi hiko cha Uchaguzi Mkuu.

Parokia zote za Jimbo la Bagamoyo, Jumuiya za Kitawa na Taasisi za Kanisa zimeombwa kuadhimisha Misa hiyo siku tajwa.

Aidha, Askofu Musomba Ameomba Tarehe 13/11/2025 Siku ya Alhamisi wakati wa kuabudu Ekaristi Takatifu tuweke nia hiyo hiyo ya kuwaombea Marehemu hao na Kuomba Uponyaji kwa wote walioumizwa siku hiyo.

Mwenyezi Mungu awe Faraja kwa Wote, na Marehemu wote Wapumzike kwa Amani.

SaveClip.App_574472270_18423460765119141_6366008245308401138_n.jpg
 
Hii ni ibada ya faraja kwa ndugu na jamaa zote waliopatwa na msiba huo
 
Mfanye maombi baada ya kutoka kula hela za sara ya uapisho, hii ni mbaya kwa kweli.
 
🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️ 🕯️
 
Back
Top Bottom