Jikumbushe umakini wako ulipoanzia

Jikumbushe umakini wako ulipoanzia

Jayspeed

Senior Member
Joined
Feb 23, 2014
Posts
156
Reaction score
169
Jifunze kushikilia vitu, watu au hata maslahi unayoyapenda kwa umakini zaidi sababu sio kuwa unavipoteza kwa kukosa umakini hapana umakini unao sana ila hukumbuki ulianzia wapi umakini wako kabla hujasahau.

Ngoja nikukumbushe...umakini wako ulianza pale ulipokuwa unatumwa chupa ya chai na mama yako na wala huangushi chupa hiyo kwa kuhofia vifinyo au fimbo zisizo na idadi..

Hapo ndipo umakini wako ulipoanzia sema unasahau hilo jikumbushe na tathimini sana hilo kisha shikilia kila unachokipenda kwa umakini kama chupa ya chai uliyotumuwa na mama kwani ukikipoteza au kukiangusha maumivu yake ni sawa ya zile fimbo za mama au vifinyo au hata maneno yake yanayoumiza moyo ambayo wengi husema bora fimbo tu kuliko maneno
 
Kitu cha kwanza nilichokua naogopa nikifanya kosa wakat nipo mdg kwanza ni mamna nitakavyoonekana, mikanda na most kind of brutal punishments kutoka kwa baba a.k.a mkolon nilishazoea nikawa sugu, akabadilisha trick akawa aniita anatumia maneno na ndo kilicho nishape mpk leo, kat ya watu ambao tungepotea maishan kama wazazi wangeamua kuchoka kwa kutosikia kwetu basi mimi ningeshapotea for sure
 
Umakini wangu unapotea pale napofanya kitu cha kijinga huku nabaki najilaumu sana.

Kuna siku niliwahi kupasua chupa ya chai, nikapasua dishi, siku hiyo hiyo nilianguka bafuni wakati nikiwa naoga. Hivyo umakini wangu ulipotea nilipovunja chupa
 
Lakini wakati m
Umakini wangu unapotea pale napofanya kitu cha kijinga huku nabaki najilaumu sana.

Kuna siku niliwahi kupasua chupa ya chai, nikapasua dishi, siku hiyo hiyo nilianguka bafuni wakati nikiwa naoga. Hivyo umakini wangu ulipotea nilipovunja chupa
Lakini wakati mwingine unaposhika chupa ile unaishika kwa makini zaidi ili iwe salama ndivyo maisha yalivyo wakati unapasua chupa ni sawa na wakati ambao umefeli kwenye maisha utalaumu kila kitu utajiona hufai lakini unapopata nafasi nyingine huwezi ichezea kwa uzembe kama mwanzo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom