Jikumbushe 'moments' ngumu kwa kupitia harufu

Centia2

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,018
1,621
Japo siyo vema kukumbuka 'misoto' ila sometimes inabidi ili liwe funzo la kurekebisha/kubadili mwelekeo wa maisha.
Binafsi kuna harufu mpaka leo hazitoki kwenye hisia zangu kwani niliziishi kipindi mambo siyo mambo.

1. Harufu ya nyasi zilizofyekwa na kuchomwa
Hii inanikumbusha kipindi ni mdogo, unatengewa kipande cha kulima na wadogo/kaka zako katika shamba la familia, ole wako usimalize!

2. Harufu ya pafyum flani (sikuipata jina) ilitumiwa sana kuwapulizia marehemu ili kuzuia harufu kabla ya maziko
Nakumbuka enzi hizo ilikuwa maarufu sana. Hii inanikumbusha ticha flani wa hesabu Darasa la 7 mkali kweli, alafu ubaoni akianza kushuka madude mnaona suruali ndo inapepea tu. Yeye hakujali kama mnaelewa ama vipi. Mwisho anataka upate zote. Kipondo chake ni bora ubebeshwe gunia la misumari (niliumia sana hisia kwa kushindwa kumuelewa)

3. Harufu ya magimbi yaliyochemshwa na dagaa chukuchuku
Hii mpaka leo hata iwe mita mia nitakwambia ni nini. Njaa ilipiga sana kijijini, kwakuwa magimbi hustahimili ukame basi hiki kilikuwa chakula cha kuamkia, kushindia na kulalia. Ole wako useme "Sili, nimeshiba", nadhani mnayakumbuka malezi ya enzi hizo.

4. Harufu ya mbilimbi
Hii nilikutana nayo baada ya kuhamia jijini, mwenyeji wangu ni maisha saizi ya chini, kila chakula anasindikiza na kachumbali/chachandu lenye hayo madude.

5. Harufu ya Makande, maharage chukuchuku, ugali na wali ulioungulia
Hapa ni kipindi nipo chuo cha kati (mkoani). Wale wapishi sijui ilikuwa makusudi ama nini. Kila chakula lazima kiungue na mafuta ya kula wanachepusha/wanapewa kidogo sana.kichefuchefu&kiungulia kwa miaka3 mfululizo (hapa sina hata buku la canteen) Daa mpaka leo hizi harufu nikizkuta nyumbani narudi kwanza.

6. Harufu ya vilosheni mshenzi (Arovella, Skalamen, Lemon and alike)
Daa, nakumbuka masela wangu kule Magereza nikiwa mahabusu kwa siku kumi. Mpaka leo kama sina pesa ya losheni (lotion) ya kueleweka bora nipake sabuni.

7. Harufu ya vumbi (la barabarani)
Hapa nakumbuka nivokuwa nasafiri kigumugumu kwenda na kurudi chuoni. Huna hata buku la kupozea koo, hofu kibao ikiwa usafiri utasumbua, huku ukitamanishwa na wasafiri wengine wanavyojijali na mazaga. Barabara mwendo wa vumbi kilomita za kutosha. Linapenya (magari ovyo) mpaka unafika hamu huna tena.

8. Harufu ya Eva (sabun maarufu za g/house)
Hizi sijui ni makubaliano ya wamiliki wa hizo sehemu. Basi nakumbuka nimeripoti kwa mwajiri ili anaipangie eneo la kazi. Nimekaa G/house kwa wiki nzima posho bado. Mimi na Eva, Eva na mimi. Mpaka leo nikijua naenda kulala huko nabeba sabuni yangu.

Mambo ni mengi, muda mchache. Tuongezee zaidi wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UmaskinI mjinga sana, yani huwaadhibu hata watoto wadogo wasojua chochote kuhusu dunia, si hata ungekuwa unasubiri unakua!!
 
Harufu ya udongo ukiloana na mvua nilikua natamani nigare gare chini niubwie, Moshi hiyo
 
Ripe banana's Wayback moshi, kipindi nimeasi nyumbani , , , tupo Mtaa na washkaji zangu Adb, Hzk, Mvm, Ems, Sms, Atm,

Pure love Body spray Naisikia harufu yake hata Nusu km Reminds me of you You xoxoxo , , , uliondoka bila kusema kwaheri

Harufu ya ugali unaoungua wayback pale MHs, Saa sita na nusu tukisikia tuu hiyo Harufu tunajua ubondo tayari,

Harufu ya mpera mbichi nakumbuka stiki nilizokuwa na kula Kutoka kwa bibi mixa mkaratusi dah nikiionaga nawish nitravel back in times nikafix hiyo miti isiwepo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom