Bora hata Voda wanatoa magari hayo tunaona watu wanapata. Tigo wanadai wanatoa milioni 2 na simu kila siku, milioni tano kila wiki lakini hata mara moja hakuna ushahidi kama kweli maneno hayo. Mbona ya kujisajili walikuwa wanaonyesha? Kujikoki nadhani kweli ni wizi. Nilienda nao kujikoki nikashituka dili lao nikaachana nao, lakini ni baada ya kuliwa pesa nyingi sana. Kuna usiri usio wa kawaida katika michezo yao. Voda kla siku wanaonyesha, ukikosa ni bhati isiyo yako. Kujikoki wanafika wakati wanadai unaongoza kwa mbali sana endelea kujikoki, ukiwa unajiweka sawa wanaanza kupunguza points kwa kila 360 wanayokukata, ghafla wanakuambia usijiamini kuna watu wamegundua mbinu zako wanakusogelea. Kisha wananyamaza au wanakuambia usijali ukikosa leo utapata kesho.
Ujinga wetu ndio unaotutafuna. Labda umasikini wetu ndio chanzo cha mahangaiko yote haya. Mnagombania gri moja la milioni 100 kwa miezi zaidi ya mitatu na kama ukipiga hesabu ya makisio ya haraka haraka unakuta wanakusanya faida kubwa mno! Tigo sio rahisi, ni wajanja zaidi wakiegemea kwa walalahoi wanaodanganyika kirahisi.
Yawezekana kuna watu wanapata, lakini kama milioni 2 zinatoka kila siku kwa mtanzania yeyote kwelikweli inaweza kuinua walio wengi sana. Usiri wa zoezi zima una utata. Ina maana mtu anaweza kupata milioni 2 kila siku kwa kijirudiarudia, maana kama umepata ya kwanza si unawekeza kwa mchezo huo tu kiwango kikubwa? asiyewahi kupata ataweza vipi kushindana katika hali hiyo? Twaongopeana, ni DECI nyingine hiyo.