Jiko la umeme

Jiko la umeme

Tarakilishi

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2013
Posts
2,180
Reaction score
2,454
Jamani naomba kuuliza aina nzuri ya jiko la umeme(two plates) ambalo ni imara. Nimetumia Singsung lakini limekufa haraka(miezi mitano tu). Natanguliza shukrani
 
Tafuta majiko used from Uk etc. Haya mapya yote ni majanga. Kama unahitaji ushauri zaidi twanga 0787577755.
 
Kaka nashukuru kwa comment yako. Nitapiga hiyo namba
 
Tafuta majiko used from Uk etc. Haya mapya yote ni majanga.
Haiwezekani jiko zee likawa bora kuliko jipya, all else being equal. Haya maelezo hayajaenda shule. Ndio maana sisi ni wa mwisho east Africa kibiashara, hatujui kutangaza biashara, hatujui kujieleza, hatujenda shule.
 
We naye nani aliyekwambia tunafanya biashara hapa?
 
We naye nani aliyekwambia tunafanya biashara hapa?
Unafanya biashara au hufanyi ushauri wako ni famba, jiko zee haliwezi kuwa bora kuliko jipya, all else being equal.
 
Jaribu kutafuta yanayotoka UK ambayo mengi ni used. lipo la TANALEC na linafanya kazi vizuri, lina hali nzuri. ukiitaji kuliona, piga; 0762193767
 
Tafuta majiko used from Uk etc. Haya mapya yote ni majanga. Kama unahitaji ushauri zaidi twanga 0787577755.

Bongo tutaishi kwa kutegemea used mpaka lini?
 
kama upo Dar es salaamm jipange nenda game pale mlimani city kuna majiko yanaitwa logik ni mazuri sana kuanzia heat controlling ( yanapika/chemsha haraka), energy efficient na pia ni imara sana. Mie nina langu tangu 2009 linapiga mzigo bila ya kutega na pia wanakupa na warant ya mwaka 1. nenda kajaribu mkuu
 
Back
Top Bottom