JIKO LA MKAA

JIKO LA MKAA

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,729
Nimeshawishika kuleta bandiko hili baada ya kuona na kusikia kutoka Star TV urahisi wa kutengeneza jokofu la kiasili lisilohitaji matumizi ya umeme lakini lenye uwezo wa kuhifadhi vyakula vibichi kama matunda na mbogamboga kama mwezi na bado vikawa na ubora wake wa asili. Yawezekana kuna walionayo na wanatumiaau wamekwisikia, kwa hao tunakumbushana tu.

Jokofu hilo lilibuniwa na Jkt na kuoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye Maonesho ya Nanenane ya mwaka 2013 Mkoani Dodoma (Nzuguni). Nakiri kusema teknolojia hii haijaweza kuenezwa japo tuna vituo vya VETA kila mkoa wakati wakulima wa mazao kama nyanya wanalia uharibifu kwa kukosa soko.

Isitoshe vijana wengi hawana ajira wakati teknolojia hii rahisi ingeweza kuwapatia kipato na wakati uleule wakulima wakaweza kuhifadhi mazao yao mabichi kwa muda wa majuma mawili hadi mwezi mmoja, wakati wakiendelea kutafuta masoko. Hakuna wadudu, pia mazao hayanyauki wala kupoteza ladha yake kwa kuwa ndani ya kibanda hicho (tazama picha - kutoka mtandaoni) kuna ubaridi wa kutosha.
JOKOFU.jpg

images.jpeg

Kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu, kibanda (jokofu) hicho hujengwa kwa:
i) Nguzo za miti ya kawaida ambayo inapatikana vijijini.
ii) Kuta za mkaa uliowekwa kwenye wavu. Mkaa huo ni wa kawaida utumikao kwa kupikia majumbani kwetu au mkaa wa mawe.
iii) Paa la nyasi zinazopatikana vijijini.

Ubaridi wake hutokana na unyevunyevu unaohifadhiwa na mkaa huku paa la nyasi likikinga joto la jua kuingia ndani ya kibanda. Mkaa unalowanishwa kwa maji kila siku au kama maji ni ya shida baada ya siku moja.

Jokofu la aina hii linaweza kutumika vijijini. Hivyo basi, nitowe wito kwetu sote kujitengenezea majokufu ya aina hii kwa kuhifadhi mazao mabichi na vinywaji, hasa vijijini ambako bei za majokovu na gharama za umeme zinaweza kuwa nje ya uwezo wao.

Wanamzingira watakuja na hoja ya uharibifu wa misitu, wakati nchi yetu ina hazina kubwa ya mkaa wa mawe. Isitoshe Serikali za vijiji hazijachakua hatua stahiki za kuhifadhi misitu kwa mfano "kata mti panda mti".

Uchumi wa viwanda ni pamoja na viwanda vya kutengeza vitu kwa teknolojia mbadala ya matumizi ya malighafi inayopatikana nchini ili kuongeza thamani ya maza yetu.
 
Back
Top Bottom