Jiji la Mwanza mipango miji mko wapi?

Jiji la Mwanza mipango miji mko wapi?

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,727
Kila ninapona picha za jiji la Mza na jinsi vilima vyake vilivyovamiwa na makazi, najawa na hofu. Hofu ya kuupoteza hilo jiji, ikitokea hayo mawe yaliyo kwenye hivyo vilima, yatakapoporomoka kwa sababu za kiolojia au shughuli za binadamu zinazoendelea bila kuthibitiwa!

Je, ni wataalamu wa mipango miji au Mamlaka yenyewe ya jiji, ambayo iko usingizini! Kilichotokea Kagera, tunaomba kisitokee Jiji la Mwanza.

Ni wazo tu.
 
Ni kweli kabisa watu wamevamia milimani na kujenga kiholela. Ukiangalia jinsi mawe yalivyokaa ilitokeà yakapolomoka tutegemee maafa mkubwa sàna
 
Ni kweli kabisa watu wamevamia milimani na kujenga kiholela. Ukiangalia jinsi mawe yalivyokaa ilitokeà yakapolomoka tutegemee maafa mkubwa sàna
Nilishashuhudia maafa Mara moja jiwe lilipoangukia nyumba na kuua wanafamilia waliokuwemo ndani.
Lakini asilimia kubwa ya wanaojenga milimani ni wageni (hasa wakurya) na si wenyeji.
 
Nilishashuhudia maafa Mara moja jiwe lilipoangukia nyumba na kuua wanafamilia waliokuwemo ndani.
Lakini asilimia kubwa ya wanaojenga milimani ni wageni (hasa wakurya) na si wenyeji.
Mlima wa kabuhoro wamejaa wahaya watupu
 
Nilishasema hapa na narudia kusema tena,Mwanza sio Jiji bali ni mkoa ambao kwasasa unalingana kwa kila kitu na mkoa wa Kigoma.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Hahaa kwahiyo kila mlima na kabila lake hiyo kabuhoro ni wahaya,wakerewe,wakara ndio wengi

Yah....mabatini na bugarika ni wakurya wa kutosha, igogo waha....huku nyamanoro, pasiansi, ghana na mji mwema ndio kuna mchanganyiko wa makabila
Ila mwanza bana, hakuna mlima uliniuma watu kujenga kama ule mlima wa kitangiri, mlima ulikuwa green ule, walikoteaga hata sijui
 
Kinachotia wasiwasi wa jiji kupotea yakitokea ya kutokea ni ujenzi katika hivyo vilima, usiodhibitiwa, ukiendana na ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya nishati na ujenzi. Matokeo yake, kinga udongo ulioshikilia mawe makubwa, unamomonyoka kila mvua inaponyesha na kuacha ustawi wa mawe ukitikisika.

Yawezekana si leo, lakini itatokea. NEMC mko wapi, au tumbua tumbua ifike huko?
 
images-1-jpg.534179

Moja ya vilima vilivyojengwa na kuharibu uhai wa kilima chenyewe kuhimili mmonyoko wa udongo endapo mvua itanyesha kwa wingi
 
Back
Top Bottom