Jiji la Mbeya kama kijiji

Jiji la Mbeya kama kijiji

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,405
Reaction score
11,196
Ukisikia jiji la mbeya utafikiri bonge la jiji kumbe upuuzi mtupu. Sasa hapa kati nilipata safari ya mbeya nikakwea Fastjet ile kutua kwa kweli uwanja wa Songwe ni mzuri kiasi (pengine kwa sababu ya upya) sasa tukapanda shuttle kwenda mjini 10,000/= (bei ya kulangua) nikafika hoteli ambayo ndio wanaisifia ni classic (Mbeya hotel) duh ni kama nyumba ya makumbush.

Nikamuambia dereva nipeleke nyingine tukaenda Paradise Hotel (nayo ya kipuuzi pia) nikaenda nyingine (GR City) dah ndio nikajua kumbe zile sifa za Wanyakyusa hapo Dar kwao hamna lolote sasa sehemu ya kula ndio ishu yaani labda uende CITY PUB hakuna sehemu nzuri ya kupata varieties.

Poor Mbeya inastahili kuitwa KIJIJI CHA MBEYA si JIJI LA MBEYA mmekalia UCHAWI tu.

Changamkieni fursa ya Mipaka ya KASUMULU & TUNDUMA kufunguka kibiashara.

Cape 2 Cairo Road inayopita Mbeya nayo ni fursa za kiutalii lakini mmekalia kuzugia dini Jumapili mchana, USIKU kama kawa.

=====

Maoni ya wadau


Unakosea unapojadili utofauti wa miji negatively - inabidi uwe positive. ni kweli wewe ni mgeni mbeya lazima uone tofauti iliyopo na miji kama mwanza kwa mfano. Mambo uliyoyazungumza sikubaliani nayo yote hasa hili la uchawi ambalo tuliache kwanza.

mwanza nayo haikuwa hivi miaka kama 25 iliyopita - hoteli kumbwa sana za kujivunia ilikuwa Mwanza hotel na kidogo lake hotel. Pamba ilikuwa almost ni guest house ya hali ya juu. hizi hotel ndo ziko comaparable na hizi ulizozitaja za mbeya. na wakati wote wawekezaji wakuu wa mwanza wakitoka Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora - mzee Makinda RIP, baba yake spika Anne, amabaye alikuwa RC wa Tabora enzi hizo (1970s) aliwasihi waarabu na wahindi wa Tabora kwamba wasisahau kuinvest Tabora na kukimbilia Mwanza. hadi sasa kuna wafanya biashara toka Mbeya wame invest Mwanza.

Investment ya juu na haraka kwa Mwanza imekuja baada ya upandikizaji na uvunaji wa Sangara, uvunaji wa madini ya dhahabu Geita, Kahama, Tabora, Mara nk. Angalia Tanga - ulikuwa ndo mji wa pili kwa Dar shauri ya mkonge na wazungu matajiri wakiwa Lushoto etc - lakini baada ya hapo mji umedorora ingawa kwa mbali unarudi tena. Maana yangu hapa ni kuwa unlike Mbeya Mwanza ina utajiri wa maeneo jirani tajiri ambayo yanakwenda kuinvest kule. Ukija kwenye population Wasukuma tu pekee ni wengi kuliko kabila lolote Tanzania na ni matajiri na watumiaji wazuri, acha wana Kagera, Mara etc

Mbeya imejikaza kuwa katika hali hiyo mbele ya policies ambazo zimewatimua wafanya biashara kadhaa ambao wameelekea Dar, Mwanza na kwingineko. Policies za Mbeya kwa wawekezaji ni HARSH = kwa mfano kuna mtu alitaka kujenga 5-star hotel eneo la gymkana kati ya uwanja wa Sokoine na mbeya peak hotel alipigwa vita tena na viongozi wenyeji wa Mbeya - ubovu wa mji wa Mbeya unaletelezwa na aina ya uongozi walionao. watu wamekalia kula pesa - miaka ile world bank ilikuwa na master plan ya kui modernize the notorious Mwanjelwa - hakuna kilichofanyika imebaki ni the best squatter ya Tanzania!!

hii thread yako inafaa isomwe na viongozi wa Mbeya masikio na macho yazibuke.

Kuhusu uchawi sikubaliani nawe - ukitoka mbeya wanasema pwani wana majini. ukifika pwani ya dar wanasema unguja. ukifika unguja wanasema pemba. pemba wanasema tanga etc.
 

Attachments

  • nemi_wa_ireneuwoya8_20210203_221859_0.jpg
    nemi_wa_ireneuwoya8_20210203_221859_0.jpg
    49.5 KB · Views: 24
Umepanic wewe, yaani unalilia uzuri wa maeneo miaka ya leo! Wenzako tunaishi vijijini huku hata umeme hakuna but hatuna wasiwasi. Kuanza kujadili uzuri ama ubaya wa maeneo ni UTOTO wa hali ya juu. Jitafakari
 
Mkuu pole sana inaonekana wamekuboa sana hapo Mbeya...

Kwenye suala la hotels nakubaliana na wewe, the last time nimeenda hapo biz trip nililala Beaco ambayo ndo walikuwa wanasema ni iko juu,, but ni kawaida sana. Anyway kwa kuwa ndio wamefunguka angani recently labda zitajengwa standard hotels maana hiyo Paradise vyumba vidogo kama gesti hausi
 
andreakalima,
Mimi hii post yako nairipoti lakini nakushauri ifute utapata shida wadau wakiingia humu wapo wengi kichizi. Hujui hao unaowaita Wachawi ndio wanaolisha familia yako!? mimi nimekaa hapo mbeya kwa miezi 6 mfululizo. Huwezi kufananisha na mkoa mwingine wowote kwa mahitaji muhimu, chakula, hewa safi, utulivu, watu wastaarabu yaani mimi huwa naliita jiji la mbeya StressFree City.
 
Mbeya ni mji wa kipuuz kama alivyosema mtoa mada. wao wanapenda sifa za kijinga tu lakini opportunities zipo ukizingatia upo njia panda ya MALAWI, ZAMBIA/ZIMBABWE/CONGO DR lakin kinachoiangusha mbeya ni UCHAWI narudia tena UCHAWI halafu ukiwakuta jumapili wanajazana makanisani utafikiri kweli wacha Mungu kumbe sanaa tu.
 
andreakalima,

Mara yangu ya kwanza kufika Mbeya ilikuwa usiku,miaka 10 iliyopita-nililala maeneo ya stand kuu hapo.kulivokucha niliamka nikaoga then nikatoka nje ili nione mandhari ya mji(wakati huo) wa Mbeya.nilishangaa kweli,but nikajua stand ipo mbali na mji,kwa kuwa nilikuwa nataka nifike ofisi za serikali nilimuuliza mhudumu pale gharama za kufika mjini kwa tax,kwanza alicheka then akaniambia hapa ndo mjini kaka....kwa kweli nilichoka.

Msamiati ,umeshawahi fika Kilimanjaro,Arusha,Iringa,Tanga,huwezi fananisha hiyo miji na wa mbeya in term of comfortability,mbeya ni mji wenye vumbi sijapata ona sehemu ina vumbi kuliko mbeya,house arrangement and some other important services like hospiatal etc
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa nje ya Dar majiji ni Arusha na Mwanza tu.................Arusha na Mwanza hutoboreka.....kumechangamka......sehemu classic na kisasa kutembelea zipo kibao.....si mji unaitwa jiji unaomba kupelekwa hotel 1st class unapelekwa hotel za Temeke stereo nafuu..........:der:
 
kama mnaona wamelala kwanini msiitumie hiyo fursa kufungua HOTEL NA PUB za hadhi muitakayo?
Kama vp mtuache watu wa mbeya ,tumeridhika na mji wetu
uliyesema sisi wachawi , ni UCHAWI gani unaozungumzia hapa?..maana unafki kama wa mtoa thread nao ni UCHAWI pia!
Karibuni MBEYA muwekeze, ili iwe vile mnavyoiwazia
 
ukisikia jiji la mbeya utafikiri bonge la jiji kumbe upuuzi mtupu. sasa hapa kati nilipata safari ya mbeya nikakwepa fastjet ile kutua kwa kweli uwanja wa songwe ni mzuri kiasi (pengine kwa sababu ya upya) sasa tukapanda shuttle kwenda mjini 10,000/= (bei ya kulangua) nikafika hoteli ambayo ndio wanaisifia ni classic (Mbeya hotel) duuh ni kama nyumba ya makumbusho nikamuambia dereva nipeleke nyingine tukaenda Paradise Hotel (nayo ya kipuuzi pia) nikaenda nyingine (GR City) daah ndo nikajua kumbe zile sifa za wanyakyusa hapo Dar kwao hamna lolote sasa sehemu ya kula ndo ishu yaani labda uende CITY PUB hakuna sehemu nzuri ya kupata varieties. Poor Mbeya inastahili kuitwa KIJIJI CHA MBEYA si JIJI LA MBEYA mmekalia UCHAWI tu.

Du Wanyakyusa tena wametoka wapi na dharau zako hizo? wewe ni mkabila na uwezo wako wa kichwani mdogo sana! Wewe umetokea nchi gani? ni Tz hii hii tunayoijua? Kama umeona watu wa Mbeya ni watu wa hovyo tu kama ulivyoandika basi una heri wewe uliyotokea Jiji zuri tuachie kijiji chetu usitukane watu hapa na kuleta chuki zako za kijinga. Wewe kwenu wapi ambako ni kuzuri sana na hakuna wachawi? hata kama n kubaya sisi ni kwetu tu,hongera zako uliyotoka sehemu isiyo ya hovyo hapa Tanzania. Ama kweli jf imevamiwa na watu wenye akili ndogo!
 
ukisikia jiji la mbeya utafikiri bonge la jiji kumbe upuuzi mtupu. sasa hapa kati nilipata safari ya mbeya nikakwepa fastjet ile kutua kwa kweli uwanja wa songwe ni mzuri kiasi (pengine kwa sababu ya upya) sasa tukapanda shuttle kwenda mjini 10,000/= (bei ya kulangua) nikafika hoteli ambayo ndio wanaisifia ni classic (Mbeya hotel) duuh ni kama nyumba ya makumbusho nikamuambia dereva nipeleke nyingine tukaenda Paradise Hotel (nayo ya kipuuzi pia) nikaenda nyingine (GR City) daah ndo nikajua kumbe zile sifa za wanyakyusa hapo Dar kwao hamna lolote sasa sehemu ya kula ndo ishu yaani labda uende CITY PUB hakuna sehemu nzuri ya kupata varieties. Poor Mbeya inastahili kuitwa KIJIJI CHA MBEYA si JIJI LA MBEYA mmekalia UCHAWI tu.

Abusive language ndio kipimo cha uelewa wako. Nimewahi sikia kwamba ni rahisi kwa mchawi kumjua mchawi mwenzie na si vinginevyo sijui kwa upande wako likoje hili. Ila nahisi utakuwa ni walewale.

Me nilitegemea utatoa hoja ya mapungufu ya jiji la Mbeya tu, ila si kutukana wenyeji wa mji huo with general view. Inaonekana una hasira na mtu ila umeshindwa jinsi ya kumfikishia ujumbe mhusika.

Lakini pia nafikiri hujui vigezo vinavyotumika kuupa mji hadhi ya jiji. Ndio walewale mnaofikiria kwamba ili kuwe na jiji lazima kuwe na maghorofa kadhaa. Hata hivyo hizo hotel ulizozitaja ni kweli ni za kawaida ila si hizo pekee zilizopo.

Lakini pia tambua kuwa serikali inapopandisha hadhi miji kuwa manispaa, halimashauri, majiji inakuwa na lengo la kuharakisha maendeleo yafike haraka. Nchini Kenya huwezi fananisha jiji la Nairobi na Kisumu au uingereza London na Manchester.
 
Ukiwa nje ya Dar majiji ni Arusha na Mwanza tu.................Arusha na Mwanza hutoboreka....
.kumechangamka......sehemu classic na kisasa kutembelea zipo kibao.....si mji unaitwa jiji unaomba kupelekwa hotel 1st class unapelekwa hotel za Temeke stereo nafuu..........:der:

Mwanza gani unayoisema? hata Arusha ninayojua! Ndiyo maana tunadharauliwa na nchi za jirani! hivi ni wapi Tanzania hii ambapo mtu anaweza kuwacheka sehemu nyingin ya Tz,hebu acheni kuleta ujinga wenu hapa.
 
ukisikia jiji la mbeya utafikiri bonge la jiji kumbe upuuzi mtupu. sasa hapa kati nilipata safari ya mbeya nikakwepa fastjet ile kutua kwa kweli uwanja wa songwe ni mzuri kiasi (pengine kwa sababu ya upya) sasa tukapanda shuttle kwenda mjini 10,000/= (bei ya kulangua) nikafika hoteli ambayo ndio wanaisifia ni classic (Mbeya hotel) duuh ni kama nyumba ya makumbusho nikamuambia dereva nipeleke nyingine tukaenda Paradise Hotel (nayo ya kipuuzi pia) nikaenda nyingine (GR City) daah ndo nikajua kumbe zile sifa za wanyakyusa hapo Dar kwao hamna lolote sasa sehemu ya kula ndo ishu yaani labda uende CITY PUB hakuna sehemu nzuri ya kupata varieties. Poor Mbeya inastahili kuitwa KIJIJI CHA MBEYA si JIJI LA MBEYA mmekalia UCHAWI tu.

Karibu Arusha Jiji la Kimataifa..
 
Umepanic wewe,yani unalilia uzuri wa maeneo miaka ya leo!!! wenzako tunaishi vijijini huku hata umeme hakuna but hatuna wasiwasi.Kuanza kujadili uzur ama ubaya wa maeneo ni UTOTO wa hal ya juu.Jitafakari

Mkuu lakini si unajua Jiji lazima linakuwa na Hadhi fulani...??
 
Back
Top Bottom