Jihadharini na IML FOREX.

Jihadharini na IML FOREX.

Concerning hiyo AML wala sitaki kuiongelea.. Wacha wenye tamaa zao wapigwe tuu.. Maana kuna watu huwa wanapenda kuibiwa

Hiyo laki sita yako kwanini usitenge mwenzi mmoja wa kujisomea forex mwenyewe halafu uje uitumie kama mtaji?

Mi hata kama sikufahamu eti unaweka pesa yako kwenye kitu kama hicho sijui AML ama ujinga mngine wowote nakukata makofi kwanza maana hakuna namna
 
Mi naweza kukuambia tumia FXCM, XM, HOTFOREX, DUKASKOPY.. chagua yoyote and you are done..
Uko sahihi mkuu, mleta mada alisema broker wazuri ni wale wanatokea Israel tu na kama broker hatokei Israel basi huyo si mzuri!!!

Kwa lugha rahisi hata hao ulio wataja wote kwa mujibu wa mleta mada ni broker wabaya na wezi maana hawatokei Israel!!

Hapa ndipo utapoona maajabu ya watanzania!!
 
Hata ukisoma Harvard, kamari ni kamari tu; tufanye kazi za uzalishaji mali/huduma na tuache kupenda miteremko.
 
Hizo kitu FOREX nafsi yangu ilinifukuza kutoka kwenye mafunzo yao ambayo ukiingia tu lazima utoe madafu.
.....
Alafu ukimsikiliza huyo mtaalam unaona mwaka hauishi utakuwa umeukwaa UTAJIRI, ...!!
 
Hakuna pesa ya haraka haraka au kirahisi..
Ila kama kawaida yetu, kukicha tunalizwa na matapeli, tuko kama sikio la kufa, hutusikii wala kuambiwa kitu, ni kama matapeli wengine kama kina Masanja, Gwajima, kakobe, Lwakatare, Flora, Bushiri, TB Joshua, Upako, n.k. n.k.
Jamani zindukeni, mnaliwa hela zenu kiarahisi rahisi, mnatapeliwa...
 
Back
Top Bottom