T Kaiza-Boshe
Member
- May 27, 2013
- 20
- 39
Wengine wanauita utapeli, kwa maana simu utaitoa wewe mwenyewe, na inandoka ukiiona.
Iko hivi, anakuja mtu unayemjua vizuri, na wakati mwingine humjui, anakuomba simu unampa; na anaweza kuchukua na ya mwingine, na ya mwingine. Nyote mtampa simu zenu! Manaweza kuuliza kwa nini, au ya nini, huyo mwizi atatoa jibu jepesi, na japo siyo jibu la kuridhisha, mtanyamaza. Akiishachukua, anaondoka. Mnakuja kushtuka baadaye kuwa kawaibia simu. Wizi huu umetokea madukani, kwenye fremu za biashara, ofisini, na msibani. Kwenye eneo moja Kawe, mwizi ametumia mazingira ya msiba kuiba simu zaidi ya kumi wahusika wakiangalia, huku akijihusisha na msiba usiomhusu.
Katika kimoja kati ya visa vinne vilivyotokea Kawe katika juma moja, mwizi ni msichana anayejulikana alikoiba kwa vile aliwahi kuishi hapo, na anapoishi kwa sasa siyo mbali na eneo la tukio. Aliingia kwenye fremu moja akamuomba dada mmoja simu janja yake akampa. Kiisha akavuka barabara ya mtaa akamuomba mwanamama mwingine simu yake. Alipokuwa amepata simu nyingine akaondoka. Sehemu hiyo ina maduka, magenge, na bucha, na biashara za vyakula sehemu za wazi, na ilikuwa saa za kazi. Hivyo huyo mwanadada alipochukua simu watu walimuona. Wenye simu walipomuona anaondoka wakajaribu kumuita lakini yeye akawa kama anapuuza na kuendelea na safari yake. Na hakuna aliyemkimbiza!
Nilipomhoji mmoja wa walioibiwa kwa nini hawakumfukuza na kupiga kelele akamatwe, alisema waliona vile wanamjua na wanajua kwao wangemfuata nyumbani. Walimfuata baadaye.
Nyumbani mwanadada huyo hakuwa na simu. Simu aliishakabidhi kwa waliomtuma, ikiwa pamoja nay a kwake mwenyewe, na waliomtuma hakuwajua! Na hawakumlipa kitu!
Alipopelekwa polisi ndipo “mchezo” ukagundulika. Kifupi, wahusika walikuwa wanawake wawili waliomwambia karogwa na kwamba wangemponyesha na pia angepata milioni 2. Alipokabidhi simu aliambiwa ili uponyaji ufanye kazi anapoondoka asiangalie nyuma. Alipokuja kuangalia nyuma hakukuta mtu. Aidha mwanadada huyo alipohojiwa ni jinsi gani aliweza kufanikisha wizi huo alisema alielekezwa na wale wanawake kuwa akichukua simu akiulizwa ateme mate chini; na alifanya hivyo. Aidha alieleza kuwa alikuwa pia amepewa kijiwe alichokiweka chini ya ziwa.
Angalizo/Ushauri: Wezi wa namna hii ni vigumu kuwakamata, na anayekamatwa siyo mwizi, ila na yeye katumiwa na kutapeliwa. Wezi wanatumia mambo mawili: Mosi, wanamtumia mtu unayemjua na kumwamini, hivyo ni vigumu kumshutukia haraka. Na hata asipojulikana anaweka mazingira ya kuaminika au udharura. Pili, wanatumia nguvu za giza. Hivyo naona kuna mambo matatu yatakayoweza kutusaidia kukabiliana na wizi wa namna hii:
1. Epuka kupeana simu. Hasa wanawake ndio wenye mtindo huu.
2. Kama una imani ya Mungu, omba wakati wote uwe na Ulinzi Wake. Hii ndiyo naiona kuwa mbinu itakayosaidia wengi, kwa vile wezi wanatumia nguvu za giza.
3. Ukiona mtu anachukuwa simu ya mwenzako nyumbani, kazini, popote; mshtue. Ama, ikiwezekana, mfuatilie mwizi kinyemela hadi anapopeleka simu na kupiga picha. Ikipatikana picha itasaidia kukamata wahusika. Maana inaelekea wezi wanakuwa ni watu wa karibu kiasi cha kujua mazingira na nyendo nyendo za mlengwa. Kwa hiyo picha yao ikipatikana inaweza kuwa rahisi kuwatambua, au hata kuwatafuta kipolisi.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx