Jihadhari na wizi mpya

Kaliua urambo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2009
Posts
603
Reaction score
127
[h=6]umezuka wimbi jipya la uhalifu. Unakuta mfuko wa nylon (maarufu kama mifuko ya condom, rambo, plastic) barabarani . Ukiukanyaga tu lazima utapata puncher maana ndani yake kuna kibao kilichopigiliwa misumari zaidi ya unavyofikiria wewe. Ukishuka garini kuangalia kulikoni wimbi la vibaka linakuvamia na hakuna utakachobakia nacho zaidi ya gari maana litakuwa halina upepo baadhi ya Magurudumu.Tujihadhari hasa usiku usipite barabara ambazo haziko busy sana[/h]
 
Ahsante kwa taarıfa. Ila nı vızurı ungeandıka "tahadharı kwa wenye magarı" ınawezekana ıngesomwa zaıdı.
 
Ahsante mkuu kwa taarifa, wengine tumezoea kurudi majumbani usiku sasa tubadili ratiba ili kuokoa maisha na mali
 
Duh!!!wezi wanazidi kuwa wabunifu!!!
Shukrani mkuu!!!
 
ugumu wa maisha ndo unao wafanya kila siku waje na mbinu mpya
asante sana kwa taarifa mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…