Jihadhari na design hii ya ma house girl | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jihadhari na design hii ya ma house girl

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by washwa washwa, Sep 7, 2012.

 1. washwa washwa

  washwa washwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 1,522
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Here comes the story part I.

  Jana 21.08.2012 nlipotoka job, wife alinipa taarifa kuwa mdogo wangu wa kike (mwenye salon ya kike kimanga) alimpigia simu kuwa amepata msichana na atakuja nae home jioni akifunga saluni.
  Ikabidi nimpigie simu mdogo wangu ili anipe full information.
  Mdogo wangu akanimbia majira ya jioni uyo msichana alifika Saluni kwake akidai anatafuta kazi za ndani. Uyo msichana akasema yeye alikuwa anfanya kazi morogoro but ametoroka kwani alikuwa anateswa na mama mwenye nyumba.uyo msichana akizidi kuongeza kuwa yeye hana mawasiliano ya ndugu yeyote ila baba yake anishi mwanza but hanjui mama yake. Basi mdogo wangu akamuonea huruma akamkaribisha saluni ilia je nae home jioni na nifanye nae mahojiano ya kina.

  Jana majira ya saa 3 usiku baada ya wao kurejea home na kula chakula ikabidi nianze kumhoji yule binti.

  Akanitajia jina lake na umri wake 15yrs, na nia yake ni kufanya kazi za ndani na akipata pesa ataenda kwao kusalimia then angerudi tena kuendelea na kazi yake.
  Ni binti mdogo na nilitamani kumsaidia.
  Baada ya kupata maelezo kutoka kwake; nilimuambia kwa sababu hatumfahamu ni lazima tukatoe report kwa balozi/mjumbe kabla hajaenda kulala na alikubali.
  Nikaenda kwa mjumbe akawa ameshalala; ikabidi nimwambie wife kesho asubuhi (yaani leo) wakiamka waende kwa balozi/mjumbe kutoa taarifa na kuandikishana.

  Leo asubuhi najiandaa kwenda kazini; kumbe yule binti ametoroka mapema asubuhi after mlango na geti kufunguliwa.
  Majirani wakasema walimuona katoka na viatu mkononi wakazani anaenda kutupa taka coz alikuwa anafagiafagia nje. Kuangalia vitu sebuleni na chumbani kwa kina dada ikaonekana everything is OK.
  Basi nikawmambia mdogo wangu na kijana flani wa jirani wamfuatilie then mimi nikaondoka zangu kuelekea job.


  Here comes the story part II.

  Majira ya saa 4 asubuhi nikiwa job nilimpigia simu mdogo wangu anitaarifu yaliyojiri:

  Akaniambia yule binti walimuona na akakimbilia nursery school flani karibia na barakuda na kwa msaada wa raia wengine walimkamata.
  Walimpiga kidogo na kumsachi. Walimkuta na elfu 90 na alikiri kuwa aliziiba ktk wallet ya mdogo wangu.

  Ikabidi mdogo wangu achukue bodaboda wakaenda nae hadi saluni kwake kimanga ili akamhoji zaidi.
  Yule binti akasema kuwa alitudanganya hajatokea morogoro but anaishi na bibi ake mbagala na ule ndo mchezo wake yeye na bibi yake.
  Akasema kuwa bib ake ni mchawi na huwa anamtumaga kwa nyumba za watu kwa mbinu ya kuomba kazi but baadae wanaiba na kuchukua watoto wadogo kimazingara.
  Akaongeza kuwa hao watoto wadogo huwa wanawachukua misukule na wengine wakiwa wakubwa wanatumwa kama alivyotumwa yeye.
  Yote hayo aliyasema bila woga huku watu wakiwa wamemzunguka pale saluni.
  Akasema kuwa jana alipoingia getini bibi ake alikuja kimazingara but ghafla macho yake yalianza kumuwasha na hakuwa na amani. Kuona vile bibi ake akaondoka.
  Ilipofika muda wa kulala alienda kuoga but aliporudi chumbani alimkuta mdogo wangu anasali ndipo alipigwa na miale ya blue na nyekundu akakimbia kurudi sebuleni.
  Aliporudi sebuleni alimkuta wife anachek TV nae wife akashtuka kumuona yule binti hana amani.
  Baade yule binti akaenda kulala ndipo wife akachukua maji ya Baraka akanyunyiza pale mlangoni na sebuleni kisha akaenda kulala.
  Yule binti akazidi kuelezea kuwa usiku hakulala kwani aliteseka sana na kuweweseka na bibi ake alipokuja kimazingara hawakuweza kuchukua watoto ikabidi aondoke na kumuacha yule binti kwani alikuwa kaishiwa nguvu.
  Akasema tangu aanze iyo kazi hajawahi kukamatwa na akmeshangaa sisi tumeweza kumkamata na kueleza siri zake. Akasema bibi ake alimjia kimazingara na akamwambia asirudi kwake kwani ametoa siri.
  Alionesha CHALI alizochanjwa na bibi ake kama kinga na alipokuwa anapigwa hakusikia maumivu yoyote.

  Alielezea mambo mengi ambayo mdogo wangu hakuweza kunielezea ktk simu kwani nae alikuwa anatetemeka kutoamini yaliyoukuwa yanatokea. Walimuachia akaondoka zake.

  I felt so sorry for my twins but I thank GOD wamebaki salama.

  Tuwe makini sana na wasichana wa kazi ndugu zangu; you may share it to your relatives and beloved.
   
 2. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Hayo mambo ya kishirikina yametawala sana mji huu .................
  :spy:
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  copy & paste....we sniff around u kno.....
   
 4. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,129
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  We Preta wewe!!!
   
 5. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna style nyingi tu ambazo hawa wanaojiita ma-house girl kumbe wana mambo yao ya ajabu sana....! tukumbuke kusali pia kunasaidia sana
   
 6. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Wife alinyunyiza ile annoiting water ya TB JOSHUA nini?
   
 7. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Poleni sana mkuu.
   
 8. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  jana tarehe 21?mbona kuna giza sana hapa?
   
 9. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  jana tarehe 21?mbona kuna giza sana hapa?
   
 10. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Poleni sana,Mungu atunusuru.
   
 11. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Dah, pole sana. Nimepatwa na incidents 2 za ma-house girls walozi. Wa tatu alikaribia kuvunja ndoa yangu in three days only! Warning, you better watch your back!
   
 12. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,078
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  Yanapatikana Parokiani au wwaweza mpelekea Padre/mchungaji ayabariki..
   
 13. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,078
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  Aisee pole sana hawa wadada wa kazi tunatakiwa kuwa nao makini sana...
   
 14. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hayo yalishamkuta mama yangu (nae anakaa kimanga). Mdogo wangu alikutana na binti akajieleza kuwa anatafuta kazi na story kibao...kwa huruma mdogo wangu akampeleka kwa mama. Kesho yake kamwibia mama vitenge na nguo zake za thamani. Mpaka kesho mama anamlaumu mdogo wangu kwa kumuokota binti njiani in the name of huruma. But ni siku nyingi sana hawezi kuwa huyu, ni more than 5 years a go.

  Sasa hayo ya uchawi inawezekana binti alishindwa maana mama yangu anasali kupita maelezo; mwamsho yeye, moyo yeye, anfunga kuliko waislamu; harogeki,

  Hii ni serious aisee. Msiokote mabinti barabarani.
   
 15. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mi ninachofanya nikipata Binti nampeleka kwa mama yangu ampeleke kwenye maombi ili kama ana sijuhi majini; sijuhi misukule tumjue; it works. Hivyo probation kwa mamaaaa.
   
Loading...