Jihadhari na airtel money

Jihadhari na airtel money

Zestach

Member
Joined
Sep 3, 2011
Posts
17
Reaction score
5
Kama wewe ni mtumiaji wa hudumu za kutuma na kupokea hela kupitia mitandao yetu ya simu naomba nikutahadharishe kuhusiana na Airtel Money.Nilifungiwa akaunti yangu,nikaambiwa itafunguliwa baada ya masaa 72,baada ya muda huo kupita nikapiga simu na kuambiwa niwe mvumilivu kwani kuna watu akaunti zao zimewahi kufungwa zaidi ya mwezi.Nikawa nimekata tamaa na kuisahau kabisa,jana ambapo ni zaidi ya mwezi nikapiga simu, jibu nililopewa ni kwamba bado inashughulikiwa.Sasa jaribu kufikiria kama ndo umeweka fedha kwenye akaunti yako ambazo unataka kumtumia jamaa yako mwenye hitaji la haraka na kwa sababu zozote zile wakawa wamefunga akaunti yako na ufumbuzi wake haujulikani ndani ya mwezi mzima,je wadhani wanastahili kutoa huduma hiyo?.Hii si kwa yaliyo nitokea mimi tu, hata jamaa zangu wa karibu nimejarbu kuwaeleza hili na kwa bahati mbaya wengine wamekumbana na adha hii.JIHADHARI NA AIRTEL MONEY,maana ukisubiri yakupate wewe waweza hata kutupa sim card yao kabisa.
 
Mkuu, simu yangu 0784371116 imefungiwa kupokea muito/ujumbe tokea November 2011. Nisaga soli ya viatu kwenda kurekebisha mpaka nikawa naonekana kama ni mmoja wa wafanyakazi wake. Nilipochoka nikalifikisha suala hilo TCRA na waliniahidi kunisaidia lakini mpaka leo hakuna kitu, ila mimi napiga, natuma na kuongeza salio kama kawaida.
Halafu wanatupotosha kwa kutangaza AIRTEL YATOSHA!!!!!!!
 
si muwafate ofisini kwao afu mgome kuondoka mpaka kieleweke
 
airtel money ni hofyo kama mafi ptuuuuu! yani nami nilikumbana na tatizo hilo kila siku ahadi. ilinilazimu nitoke mkoani (mby) hadi kwenye ofis zao pale Morocco. nilirudi zaidi ya mara nne kila siku dana dana. naona walivamia business hawa
 
Ebana kumbe na nyie mmeshawashtukia hawa jamaa, siku moja nimepata tatizo na line yangu ya airtel nikawapigia simu za kila aina, aisee hawajamaa kwanza hawapokeagi simu ya mteja hata kwa dawa!!!!!!!!!!, eti wananiambia "bonyeza 1" kuacha tarifa yakupigiwa, eti watu wa airtel wanipigie mimi kwa kuwa muda huo wako bize, au nibonyeze sijui kidude gani, niache ujumbe wa sauti eti watanipigia badae, sasa ni mwezi mzima sijawahi kupigiwa na airtel kusikiliza shida yangu. hapohapo kuna jamaa yangu alikosea kutuma hela ikaenda kwa mtu mwingine, ashukuru ilikuwa kiasi kidogo cha TSH20,000 aliifatilia mpaka amekata tama, bahati mbaya kabisa ametupilia mbali simcard yao. Kwahali hii nimeshakuwa na tahadhari na airtel, pamoja na airtel money.hawataniona kamwe!!!!!!!!!!
 
airtel yatosha nyingine ya nini????????????????
 
Hili Ndio jawabu....tumezoea kuandamana na tuandamane kwa hili

hawa nikuwata na kuwapa mabanzi ya maana mpaka wa improve huduma ehh mnajifungia nao ndani aisee no body in no body out uone watanyoooka
 
hawajamaa ukipata tatizo hasa airtelmoney hamna msaada kabisa kwa mteja na customercare mbovu kama nini haina msaada wowote ni majanga
 
Mkuu, simu yangu 0784371116 imefungiwa kupokea muito/ujumbe tokea November 2011. Nisaga soli ya viatu kwenda kurekebisha mpaka nikawa naonekana kama ni mmoja wa wafanyakazi wake. Nilipochoka nikalifikisha suala hilo TCRA na waliniahidi kunisaidia lakini mpaka leo hakuna kitu, ila mimi napiga, natuma na kuongeza salio kama kawaida.
Halafu wanatupotosha kwa kutangaza AIRTEL YATOSHA!!!!!!!

Mimi namba yangu ya Airtel 0786848489 niliitupa mahali nisipopajua maana ilikuwa ukinitumia sms saizi itanifikia baada ya saa 60. Nimesugua soli kutaka irekebishwe mwishowe watu wa customer service walinikariri hadi jina..nikalitupilia mbali li line lao
 
Hahahaa! Tigo wezi, Zantel wazembe, Aitel wezi, Vodacom wezi, TTCL washakufa basi hamieni shirika la Posta Tanzania utawasiliana na ndugu jamaa kama kawaida ila msisahau ile ' hofu na mashaka ni kwenu mliombali na upeo wa macho yangu'.
 
Mie nilikosea kutuma pesa ikaenda kwenye namba ambayo haipo yaani ipo sokoni inauzwa wakagoma kunirudishia pesa yangu,halafu hii huduma yao ya miito ya simu hataukijitoa wanaendelea kukata pesa tu yaaani kweli airtel yachosha
 
Mimi namba yangu ya Airtel 0786848489 niliitupa mahali nisipopajua maana ilikuwa ukinitumia sms saizi itanifikia baada ya saa 60. Nimesugua soli kutaka irekebishwe mwishowe watu wa customer service walinikariri hadi jina..nikalitupilia mbali li line lao
Mkuu mie nimeshindwa kuitupa kwa sababu imesajiriwa kwa jina langu na ndio maana nikawataarifu TCRA.
 
Pana mjingamjinga mmoja humu JF kawasifia kwa kupunguza gharama wakati hilo ni agizo toka TCRA kwa kampuni zote za simu nchini.
 
Back
Top Bottom