Jihadhari kukopesha ndugu fedha

Mkopo ni kiumbe mbaya sana nakumbuka kuna mama mmoja miaka michache iliyopita alikopa pesa kwenye taasisi moja ya fedha akawa hajalipa kwa mda unaotakiwa, wale jamaa wa benki walimtafuta nyumbani kwake hawampati mwisho wa siku wakaelezwa na majirani zake kwamba yule mama anashinda na kulala kanisani kwa kakobe Mwenge, basi bwana si wakaja kanisani kumtafuta walipofika getini wakajieleza vizuri yule mama kweli alikuwepo akaitwa na wahudumu getini ile kufika na kuwaona wadeni wake hiiiiiiiiiiiiiiiii hakujali kama yeye ni mama mlokole aisee acha weee kilichotokea ni kwamba mama yule alikurupuka na kuruka ukuta kurukia upande wa pili asikamatwe na wadeni wake nakwambia watu hawakuamini kilichotokea mbele ya macho yao, mama yule akapotea bila kuwekwa mikononi mwa wadeni wake, kwa hiyo ndugu yangu deni ni mzigo mzito sana unaondoa utu na hata thamani yako.
haijalishi wewe ni mlokole, tajiri, mchungaji, sheikhe au nani kama huwezi kurudisha mkopo acha kukopa vinginevyo fedheha na aibu itakupata ndugu!
 
Sikuizi kukopesha imezidi kua mbaya, kuna kipindi hua nacheka nikiona wadada wanadaiana hela za vikoba sijui mara imekuja mkokoteni unabeba vitu,mara imetoka Tv mara wamekodi watu,sasa wewe kudai hujui mkuu kukopesha unajua,
manake watu wa uswahilini mahodari wakudai,kwanza hiyo aibu yake atakavyo kuadhiri lazima hela yake urejeshe..
 
Mim elf 20 tu nilimkopa dogo mmoja analia alipe bili ya maji na umeme yan tang mwk jana mpk leo nkimdai anasema hela ndog iyo ndg yang unaidai km nin kuna mda naishiwa kat sent sin ndan nkimdai hapokei cm wana la sms hajibu apo aliomba 50 nkampa 20 ngempa 50 ngeumia zaida hela ya kutafuta mwenyew inauma sana hata km buku ni yako na jasho lako
 
kweli kabisa
kukopesha ni kujichimbia kaburi, tena mtaishia kugombana bure
bora umpe mtu ela ambayo hata asiporudisha,haitakukwamisha kitu
 
Jirani yetu nilimkopesha laki 400,000/= akawa ananizungusha ikapita miezi kama minne nikajiuliza pesa ya mwanaume hailiki bila jasho nikamvutia muda miezi mitatu tena kimya siku moja nikasubiri mwisho wa mwezi nikaenda nyumbani kwake nimevaa koti refu na sime kiunoni akanikaribisha ndani tukaongea akaanza kunizungusha mimi nikamwambia jamaa yangu pesa ya mwanaume mwenzio huwezi kuila bila kuitolea jasho sasa basi leo tunamalizana nikachomoa sime langu akahamaki akasema jirani tusifikie hatua ya kutoleana silaha pesa yako nakupa akazama ndani akanipa pesa yangu nikatoka hapo nikaenda polisi kuchukua RB kuwa kuna mtu ananitishia maisha maana nilijua nimeshalianzisha mpaka leo hii nikimkopa hela huwa anarudisha bila shuruti
 
Nimepoteza Mil 2 na lake Moja na kumi Alipewa ancle ili nikasome chuo kikuu huria badae Jina langu litatokea nikapata mkopo wa serikali ilikuwa 2009 wakati naondoka kwenda chuo nikamwambia naomba hela. Akaniambia atanilipa amekombolea gari bandarini hadi leo sijapata pesa na nimesamehe tu Sina namna
 
sasa wote mkikataa kukopesha sisi tutakopa wapi....hata wew unaekataa kukopesha kuna siku utataka kukopa...cha msingi ni kuweka mazingira rafiki ya kuipata pesa yako andikishiana na mtu ikizidi milioni awe na kitu ukishike kadi ya gar, pikipik or kiwanja ukifanya hivyo hela yako itaipata tu
 
Jamaa yangu alikwenda kudai pesa zake na hakupewa na aliporudi nyumbani akaugua ugwanjwa wa ajabu na akafa watu wakaseama amelogwa. Kuna mwandishi mmoja alikuwa anatafuta habari na akaenda kwa mganga kujifanya ana shida na akakutana na watu wamekuja kwa mganga kwa ajili ya kuloga watu waliowakopesha pesa zao. Nimeshawakopesha wengi na cha kusikitisha ni mmoja alikuwa akijiita mchungaji na ameishia na pesa zangu. Inakuwa vigumu saa nyingine kumnyima maana anakuwa ni rafiki yako lakini akishapata anaishia. Kwa ujumla ukikopesha jiambie mwenyewe umemsaidia.
 
jombaaa iyo kitu nouma xana deni linakera watu wakishasolve shida zao bac asivi akija mtu anataka mkopo mwambie aende bank uko
 

Dah, Ni ndugu umemsaidia.... Potezea bwana.... Sio ndugu wote wako hivyo.... Mi mtu akichelewa nilipa lakini anaonyesha concern namwelewa, mambo yanakuwaga tight wakati mwingine tunasaidiana. Dah ulikuwa una 8m, hiyo laki Sita Ni Fanya Ni malumbuko ukilalama hivi utakosa pesa na baraka
 
Pesa ya mwanaume hailiki bila kuitolea jasho nikikukopesha zangu utazirudisha tu
 
Pesa ya mwanaume hailiki bila kuitolea jasho nikikukopesha zangu utazirudisha tu
 
Nenda kwenye taasisi za mikopo,utaratibu huu wa kukopesha kishikaji ni Africa tu
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…