Jihadhali na mdudu hatari nzi

Jihadhali na mdudu hatari nzi

Pol Paul

Member
Joined
Apr 15, 2018
Posts
66
Reaction score
55
Kuna wadudu wengi wanaotuzunguka, wengine tunaishi nao majumbani hata kama hatuwapendi.

Inzi (housefly or scientifically musca domestica), ni mdudu wa kawaida kabisa kwa wengi wetu mwenye madhara mengi kuliko faida kwa mwanadamu.

Wengi hatujakaa tukajifunza angalau kidogo kuhusu mdudu huyu. Leo naomba nikuhabarishe kidogo tu kuhusu jamaa huyu “mtoto wa nyumbani” ambaye twafahamu hasikii hata kama ukimfukuza vipi atapenda kurudi na kutua sehemu ambazo wengi hatupendi.

Inzi hana meno hivyo hula chakula cha majimaji tu ambacho ni pamoja na kinyesi (feces), vitu vilivyooza (moist, decaying organic matters), vidonda (open sores), na vitu vingine vilivyoharibika na kuoza.

Inzi ana ulimi ulio kama mrija ambao huutumia kufyoza chakula chake. Akiona chakula kigumu, hukitemea mate au kukitapikia ili kilainike kisha hukifyonza. Inzi hucheua chakula kisicholainika sawasawa na baadaye kukila tena kikishalainika.

Inzi ana mabawa mawili na miguu sita ambayo pia huitumia kuonjea chakula. Miguu ya nzi ina uwezo wa kuonja sukari mara milioni 10 haraka zaidi ya ulimi wa mwanadamu!!. Inzi hutumia milingoti (antenae) yake kunusia. Ingawa inzi ana lensi 4000 ndani ya macho yake, lakini huona vizuri umbali wa inchi 24 hadi 36.

Sehemu nzuri za inzi kutagia mayai ni zenye unyevunyevu mchafu, wenye joto na vitu vilivyooza kama vyooni hasa vya shimo, jalalani, n.k. Mama inzi mmoja mwenye afya nzuri anaweza kutaga mayai 50 mpaka 75 kwa mtago mmoja hadi mayai 500 – 1000 kwa maisha yake yote.

Kukupa tu wazo jinsi inzi wanavyoongezeka kwa haraka, kulingana na hekima za mtaalamu wa wadudu (entomologist) mmoja aitwaye Hodges: wakiwepo inzi wawili (baba na mama) wenye afya nzuri, wakianza kazi Aprili; ifikapo Augosti, inzi hawa watakuwa wametengeneza jeshi la inzi wengine wapatao 191, 010, 000, 000, 000, 000, 000!!!. Hebu Angalia inzi wakifanya vitu vyao hapa:

 
Nzi ni mdudu ambaye anakupiga huku anakulamba......ni hatar kinoma
 
Back
Top Bottom