Jifunze Utengenezaji Sabuni Ya Mche Bila Kutumia Mashine

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
Wajasiriamali House tumekuwa kwa zaidi ya miaka 10. tukiwasaidia Watanzania walio na mitaji isiyozidi laki 5 ,mbinu za kuanzisha au kuboresha bidhaa zao sambamba na mbinu za mauzo ya bidhaa zao. Kwa leo tutaangalia jinsi ya kuwa na kiwanda kidogo nyumbani cha utengenezaji sabuni bila kuhitaji mashine.

Tukizungumzia sabuni , Ni bidhaa inayopatikana baada ya kuchanganya asidi na alkali kwa ratio maalum

Kwa Tanzania, Kuna asidi inayopatikana kwenye mafuta ya wanyama na asidi inayopatikana kwenye mbegu za mimea

Ukitumia mafuta ya wanyama ,kwa kuwa yanaganda, utahitaji kuyeyusha, hivyo utatumia Moto ,tunaita heat process

Ukitumia mafuta ya mbegu za mimea Kama mbegu za mawese, mafuta yake huitwa mise kwa watu wa kigoma au mbosa kwa watu wa kyela

Sisi tunatumia cold process

Ukisha pata mafuta ya mise a.k.a mbosa, unahitaji alkali. Hapo tunatumia materials yaitwayo caustic soda kwa jina la dukani. ( Kwa jina la darasani tunaita sodium hydroxide, NaOH)

Kwa hiyo ili kupata sabuni , Ni lazima ratio yako ifikie point tunaita saponification value. Kwa hesabu rahisi kabisa, kila lita moja ya mise, tunachanganya mls 160 za caustic soda



Hapo utachanganya kwa mwiko au mashine ya kukorogea mpaka uchanganyike kabisa na rangi kubadilika



Hatua inayofuata Ni kubadili mchanganyiko wetu huu kuwa sabuni tuitakayo

Utafanya Kama ifuatavyo:

Gawa mchanganyiko wako kwenye vyombo kadhaa, na kila chombo utaongeza additive materials upendayo

Kama utaongeza natural clay, kijiko kimoja, sabuni yako itakuwa ya ngozi

Kama utaongeza rangi ya Blue, sabuni yako itakuwa ya mawingu

Kama utaweka aloevera,itakuwa ya mualovera (Nimeweka video ya utangulizi)





Nimeandaa kozi ya video na text, anayehitaji link za kui- access atalipia elf 10 tu, kwani tutamuongoza mkono kwa mkono mpaka atengeneze sabuni yake mwenyewe.Humo tumeelekeza maduka ya nayouza malighafi kwa bei nafuu zaidi, masoko ya sabuni na vitendea kazi kama mold au mikorogeo ya umeme. Pia kwa wanaohitaji ana kwa ana kwa ana ,mafunzo haya tuwasiliane kwa 0713-039 875
 

Attachments

  • Sabuni Bila Mashine.mp4
    11 MB
Back
Top Bottom