Jifunze namna ya kuanzisha biashara

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
Kwenye thread hii nimeona wengi wamepost hoja ya kutaka ushauri wa kuanzisha biashara, na wengine wameenda mbali zaidi kwa kutaja kiwango cha pesa alicho nacho kwamba ni biashara gani itafaa. Lakini inaonyesha dalili kwamba waanzaji wengi wa biashara wanakimbilia kuanzisha biashara kabla ya kupanga mikakati ya utafiti kwa kutumia kigezo cha business plan. Ni dhahiri uanzishwaji wa biashara ambayo itasajiliwa serikalini na kulipia kodi ni tofauti na mfumo wa biashara za kimachinga ambao hununua na kuuza eneo analotaka na sipopata wateja huhamia eneo jingine.

Business Plan ni jambo la kwanza na la msingi katika uanzishwaji wa biashara yako. Mambo ya msingi unayotakiwa kufanya katika business plan yako ni kama ifuatavyo:
  • Aina ya biashara unayokusudia kuanza
  • Wateja walengwa kwa biashara yako wanaoishi maeneo hayo, wanaopita maeneo hayo nk.
  • Eneo la kufanyia biashara yako ukitilia maanani kuchunguza ushindani wa biashara uliopo katika eneo hilo.
  • Fanya utafiti na wafanyabiashra wengine ambao wana uzoefu na biashara hiyo ili kupata mwelekeo wa biashara yako.
  • Fanya utafiti wa source ya kupata bidhaa kutoka makampuni yanayouza na tafiti ni kampuni ipi yenye maslahi kwako.
  • Andaa mfumo wa makadirio ya gharama za uendeshaji wa biashara ikiwa ni pamoja na Mtaji wako,
  • Gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na gharama za uanzaji wa bishara, vitendea kazi, kulipia pango, tax, umeme, usafiri, simu, mishahara, nk. (Kumbuka wewe unalipwa mshahara pia na umeajiriwa na biashara yako).
  • Andaa jedwali la makadiri ya mapato na matumizi ya kila siku, juma mwezi hadi mwaka mmoja.
  • Kisha tathmini faida utakayopata baada ya gharama za uendeshaji na kumbuka biashara inasimama ambayo ina net profit, gross profit tu ni hasara.
Mtaji ulio nao usiuhesabu kama ndio kianzio cha biashara yako, maana kuna gharama za maandalizi ya mahali utakapoweka biashara yako, leseni za biashara pamoja na vitendea kazi vingine. Hivyo vyote uvifanyie mahesabu katika gharama za uanzishwaji wa biashara yako.
Hakikisha theluthi moja ya mtaji wako wa pesa umebaki kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako maana biashara hadi isimame na kuanza kujiendesha yenyewe huchukua wastani wa miezi 6 kama upo eneo lenye wateja wazuri.

Huu ni ushauri wangu binafsi, nategemea kuna wengi hapa wenye ushauri mzuri zaidi watajazia yaliyopungua.
 
Mkuu nashukuru ntafanyia kazi ushauri wako maana mimi ni mmojawapo wa wanaotafuta jinsi ya kukuza mtaji wangu mdogo kama wa m.7 hivi
kama unaweza nisaidia zaidi plz niambie niku-PM ili tuwasiliane zaidi. hii ni kwa yeyote anaehisi tunaweza kuunganisha nguvu tukafanya biashara. nipo huru kuja popote ulipo ili tuweke stratergies zaidi na hasa kuwa karibu kwa kila tulifanyalo
 
Mkuu nashukuru ntafanyia kazi ushauri wako maana mimi ni mmojawapo wa wanaotafuta jinsi ya kukuza mtaji wangu mdogo kama wa m.7 hivi
kama unaweza nisaidia zaidi plz niambie niku-PM ili tuwasiliane zaidi. hii ni kwa yeyote anaehisi tunaweza kuunganisha nguvu tukafanya biashara. nipo huru kuja popote ulipo ili tuweke stratergies zaidi na hasa kuwa karibu kwa kila tulifanyalo

Nimekupata, nitajitahidi baada ya weekend hii kujadiliana nawe maana dunia ya leo uchumi ni wa mfumo wa utandawazi, ushirikishi na mengineyo. Thanks again.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom