Jifunze Lugha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jifunze Lugha

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by engmtolera, Nov 5, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2]Maana ya lugha[/h]Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye kubeba maana, zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.
  [h=3]ni sauti za nasibu kwa sababu:-[/h]
  1. Zilizuka tu bila makubaliano maalum ya jamii kwamba zilikuwepo na hakuna jamii iliyofanya kikao kukubaliana juu ya kuunda lugha na matumizi yake.
  2. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kifungu sauti .Ndio maana kitu kimoja kilekile kinaweza kuitwa kwa maneno tofauti katika lugha tofauti
  3. lugha ndiyo nyezo kuu ya mawasiliano baina ya binadamu.
   Binadamu hutumia lugha kukidhi mahitaji yake ya kila siku.
   Baadhi ya matumizi ya lugha ni:
   kupashana habari
   kubadilisha mawazo

   [h=2]MUUNDO WA LUGHA[/h]- Lugha hujengwa kwa maneno.
   -Msingi wa maneno ni sauti moja moja
   -Sauti hizo ambazo hujenga maneno huitwa vitamkwa
   -Vitamkwa hivyo huwa katika mpangilio maalum unaolipatia neno maana.   MWENDELEZO WAKE SIKU IJAYO

   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=4]Mfano wa vitamkwa-ch,k,a,l,u na o.[/h][h=3]vitamkwa[/h]- Ni muanisho wa sauti zitumikazo katika lugha.
  - vitamkwa hivyohuwasilishwa na herufi za alfabeti.
  - alfabeti zimegawanyika katika konsonanti na Irabu
  - Irabu za kiswahili zipo 5 nazo ni:-
  a, e, i, 0 na u
  - Konsonanti za kiswahili zipo 19 nazo ni:-
  b,c,d,f,g,h,j,k,l,m,n,p,r,s,t,v,w,x,y na z.
  -Jumla kuna alfabeti: 24 za lugha ya kiswahili.
  -mawasiliano ya kutumia ishara si lugha kwani hayatumiii sauti wala maneno.
  -kwahiyo mawasiliano baina ya wanyama hayawezi kuitwa lugha.


  Tuonane kesho jamani
   
Loading...