Jifunze kwa Aliko Dangote

Martini Am

Member
Mar 7, 2016
9
6
Moja ya siri zinazoweza kukusaidia kufanikiwa katika biashara ni kuweza kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara Waliofanikiwa. Ni busara na vyema sana kuangalia waliofanikiwa katika biashara walipitia njia gani ili na wewe uweze kuzifuata njia hizo, na kama zina makosa uweze kuziepuka.


Unapozungumzia watu waliofanikiwa katika biashara kwa hapa Afrika, huwezi kuacha kumtaja Alhaji Aliko Dangote. Dangote ni mfanyabiashra aliefanikiwa zaidi katika Biashara, na uliwengu unamtambua kutokana na utajiri wake unaofikia Dola za kimarekani bilioni 18.6!

Dangote amewekeza sana katika biashara ya Seluji, unga na sukari. Hivi sasa anasambaza kwa kasi biashara yake ya Seluji kwani amejenga viwanda katika mataifa mbalimbali ya Afrika , Tanzania ikiwemo.


Leo nataka nikuibie kwa uchache tu, njia alizopitia Alhaji Aliko Dangote hadi kuweza kuwa Muafrika tajiri zaidi.

Cha kwanza unachopaswa kufahamu ni kwamba Alhaji Aliko Dangote nae aliwahi kuajiriwa. Alhaji Dangote, alianza harakati za maisha kwa kufanya kazi kwa mjomba wake , Bwana Sani Dangote.

Kwa kuwa alifanya kazi kwa uamifu mkubwa, Dangote hakupata tabu alipomuendea muajiri wake kumuomba Mkopo wa biashara. Mwaka 1977 , Aliko Dangote alipewa mkopo na mjomba wake ambae ndie alikuwa bosi wake kwa wakati huo. Aliko Dangote alirudisha Mkopo huo ndani ya miezi mitatu kama walivyokuwa wamekubaliana na mjomba wake.

Aliko Dangote alipambana na kusimama imara katika Biashara ya bidhaa kama mafuta ya kupikia, cocoa, pamba, mtama, mchele na chumvi.

Kwa kuwa alikuwa akiingiza bidhaa hizo nchini Nigeria kutoka katika mataifa mbalimbali, Aliko Dangote alijitahidi sana kutengeneza mtandao wa kibiashara ambao ulimsaidia kusambaza bidhaa zake. Huwezi kufanikiwa katika biashara bila kutengeneza mfumo mzuri wa kibiashara kuhakikisha bidhaa zinawafikia wateja wa chini kabisa.

Baada ya kufanya biashara ya kuingiza bidhaa toka nje ya nchi yake kwa muda mrefu, baadae Dangote aliamua kuzalisha bidhaa alizokuwa anaagiza. Hapo ndipo alifungua viwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zile zile alizokuwa akiagiza kutoka nje.

Licha ya utajiri mkubwa alio nao, Dangote anafanya kazi kwa bidii sana na Daima haachi kumtegemea Mungu.

Inaaminika kwamba Dangote analala saa 8 usiku na kuamka saa 11 kamili kila siku. HEbu jiulize wewe Mtanzania mwenzangu. Unalala saa ngapi na kuamka saa ngapi? Ukichelewa kulala unakuwa unafanya kazi au unakesha ukila Ujana?


Nakuacha na hii Stori ya Dangote kupata Baraka kutoka Mtumishi wa Mungu. Ilikuwa ni mwaka 1977, Mchungaji mmoja aitwaye Benson Idahosa, aliwasindikiza wageni wake kwenda Airpot. Wageni hao walikuwa Watumishi wa Mungu waliokuwa wamekwenda Nigeria kuhubiri, lakini siku waliyohitaji kusafiri kurudi Marekani walikuta ndege imejaa. KWA KUWA ILIKUWA WASAFIRI SIKU HIYO, Mchungaji Benson Idahosa, aliingia kwenye ndege moja na kuwaomba abiria wawape siti watumishi wa Mungu. Hiyo ina maana kwamba, ilihatajika abiria wawili mmoja mwenye Roho ya utu, waahirishe safari ya kwenda ughaibuni watoe siti kwa ajili watumishi wa MUNGU. Abiria walionekana kupuuzia ombi hilo. Ghafla, Mchungaji alimuoana kijana mmoja mdogo akisimama kutoka siti za nyuma, na kunyoosha kidole kwa abiria mwingine akimuambia “ Wewe shuka, tutasafiri kesho”. Kasha abiria hao wakanza kushuka kwenye ndege na kutoa nafasi mbili katika ndege hiyo kwa ajili ya Wahubiri.

Mchungaji Ben Idahosa, alimsimamisha kijana Yule aliyemuamuru mwenzake washuke, na kisha akaamuliza jina lake.

Kijana alijibu, “Jina langu ni Aliko DANGOTE, NA huyu nilieshuka nae ni msaidizi wangu’


Mchungaji alishikwa na Butwaa, ana akatamka maneno ya Baraka kwa kumuambia Dangote “ Mungu wangu atakubariki wewe, na bishara yako itavuka mipaka ya Afrika, na kuvuka vipimo vyote”


Wakati huo Dangote alikuwa kijana wa miaka 20 tu ; leo hii dua ya mchungaji huyo imetimia. DAngote ni tajiri namba moja Afrika. Changamoto kwako Mtanzania mwenzangu, amabe hata huwezi hata kumpisha Mzee akaeti kwenye siti ya Daladala.
 
Utaratibu wa kupanda ndege miaka hiyo ulikua wa ajabu

Ndege mnaombana kuachiana seat kama daladala za mwisho wa lami machimbo lumo

Ahsante kwa kushare mkuu,hata kama sio kweli ila ujumbe umefika
 
moja kati ya watu wanao ni motivate naye yupo DANGOTE vijana tufollow nyayo zake sio watu ambao hawana maana huko isntagram
 
moja kati ya watu wanao ni motivate naye yupo DANGOTE vijana tufollow nyayo zake sio watu ambao hawana maana huko isntagram

Biasharasio rocket science,do things which makes you happy...kama umewahi seat na hutaki kushuka,no need ku-feel guilty eti kuna mchungaji ameomba,kama umeamua kutoka rohoni kushuka kama Aliko ni vema na haki,ilmradi usiwe mnafiki tu...

Sio baraka wala lucky Aliko hapo alipo,ni blood tears na out of this world efforts na smartness,tusianze kutisha watu na wachungaji na baraka sijui nini na nini,ilimradi hujamdhulumu au kumsababishia mtu maumivu,napinga kabisa hizi technique za kuwafanya watu wa-feel guilty eti sababu tu wewe ni mchungaji wakati ni haki ya yule bwana...

Biashara is a game,Aliko plays it like Michael Jordan,game over my nigga...stop link his prowess na yule mchungaji alie msaidia kiti,no relationship at all!
 
Dangote utajiri wake umetokana na ushikaji wake na Sani Abacha wakati huo. Akapewa haki ya kuingiza bidhaa nyingi peke yake (Monopoly ) mfano sukari, Mchele nk
 
Copy kutoka wikipedia...alizaliwa kwenye family yenye cinnection ila amezitumia vizuri na kufanikiwa.
Dangote hails from a very prominent business family. He is the great grand son of Alhaji Alhassan Dantata, the richest African at the time of his death in 1955. Aliko Dangote, an ethnic Muslim Hausa[7] from Kano State, was born on 10 April 1957 into a wealthy Muslim family.
 
Kumbe alikuwa na msingi tayari- wa fedha pamoja na uzoefu.

Si ajabu hata amesomea business administration, kwa business ya aina hiyo huendeshi kwa rehema ya Mungu tu, nguvu ya kujituma na mipango thabiti vinahitajika ili uweze kupeleka biashara mbele.
 
Utaratibu wa kupanda ndege miaka hiyo ulikua wa ajabu

Ndege mnaombana kuachiana seat kama daladala za mwisho wa lami machimbo lumo

Ahsante kwa kushare mkuu,hata kama sio kweli ila ujumbe umefika

Hiyo ya kushuka mtu sijui kama ni kweli ndege zinautaratibu wake sio kama daladala niliwahi kuachwa na ndege kwa sababu tu ruban kashafunga mlango
 
babu yake dangote tu... baba wa mama yake mzee datanta alishawai kuwa tajiri kuliko wote nigera kabla ya dangote hajazaliwa..

kama babu tu tajiri.. mjomba tajiri.. why na yeye asiwe tajiri..

dangote sio self made.. alikuwa anakopeshwa hela kwa wajomba zake na hadaiwi hata akishindwa kuzilipa wanampa nyingine na hapo hakuna riba.

so hakuwa na uoga wa kupata hasara akifeli biashara anarudia tena na tena bila wasi wasi maana hela zipo.

sasa wewe nenda kakope bank na mariba kibao uisome namba
 
Moja ya siri zinazoweza kukusaidia kufanikiwa katika biashara ni kuweza kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara Waliofanikiwa. Ni busara na vyema sana kuangalia waliofanikiwa katika biashara walipitia njia gani ili na wewe uweze kuzifuata njia hizo, na kama zina makosa uweze kuziepuka.....

Sana sana labda nijifunze jinsi ya kuibia serikali duniani kwa KUTOLIPA KODI WAKATI UWEZO UPO!
 
Back
Top Bottom