Jifunze kuzipumzisha hisia zako

Jifunze kuzipumzisha hisia zako

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,450
Reaction score
5,127
Habari wana MMU,

Kuna wakati unafika mtu unakua umeumizwa kihisia sana,umeachwa au umesalitiwa na mpenzi wako na kujikuta unaona kama dunia si mahala salama pa kuishi, unapoteza ladha ya maisha kabisa. Unaanza kujihukumu au unajiona hufai na hukustahili kupitia maumivu makali hayo unayopitia.

Na katika hatua hii watu huchukua maamuzi mabaya au kutafuta wenza wa haraka ili kujaribu eidha kulipa kisasi au kutuliza maumivu, na kwa kua unaanzisha uhusiano wa ghafla bila kufafakari mara nyingi huwa unajikuta umeingia katika matatizo mengine zaidi.

Hivyo unapoona umeumizwa kimapenzi njia nzuri si kutafuta mbadala kwa haraka bali unatakiwa kukaa karibu na marafiki au washauri ili waweze kukuondolea upweke na mawazo hayo.

Tafuta kitu ambacho kitakufanya uwe na muda mchache wa kukaa bila kujishughulisha ili mawazo yasije kukurudisha kule .Ili uchukue muda mrefu bila kuwa na mahusiano.

Hivyo hisia zako zipumzike na moyo wako upunguze maumivu ndipo utaweza kua na uchaguzi sahihi wa mwenza mwinginekama utakua unahitaji kuwa nae.



1574171328891.png
 
Back
Top Bottom