D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,307
- 3,489
KUNA CHA KUJIFUNZA KWA PYTHAGORAS
Huenda hukusoma sana, lakini ulimaliza darasa la saba. Basi hiyo inatosha. Inatosha sana kwa wewe kukutana na kitu kinaitwa
" Pythagoras theorem"!! Hukumbuki? Je hii a²+b²=c² ushawahi kukutana nayo??! Kama umewahi kukutana nayo, hiyo ndiyo inaitwa “Pythagoras Theorem”.
Mwaka 569 BC, Pythagoras alizaliwa huko Samos, Ugiriki.
Kitu ambacho hukijui ni kuwa Pythagoras hakuwa tu Mathematician, ila alikuwa *Philosopher* mwenye msimamo wa kipekee. Japo Philosophers wengi walijikita katika kutafuta ukweli juu ya "Chimbuko la dunia", Pythagoras hakuwa na muda huo. Yeye aliamini tu kuwa dunia hii inatawaliwa na amani, na "mahusiano ya kihesabu" ndiyo yanayoweza kuelezea vizuri zaidi hii amani.
*Pythagoreans* ndiyo lilikuwa kundi lililoamini imani hii, wakaweka misingi yao "migumu" sana katika kutekeleza imani yao.
Moja kati ya mambo makubwa ni kuwa imani yao ilitawaliwa na usiri wa hali ya juu sana.
PYTHAGORAS alikataa kabisa mafundisho yake yasirekodiwe katika maandishi.
Kuna kitu kimenivutia zaidi kuhusu *PYTHAGORAS*ni pale alipokuwa na miaka 18, alipoamua kufunga safari hadi kwa Mathematician na Philosopher wa zama hizo aliyeitwa THALES, japo kipindi hiki alikuwa mzee sana na hakuwa anaweza tena kufundisha, lakini Pythagoras aliamua kwenda "kupata chochote".
Akafika na kuchota hekima na busara za kutosha sana zilizomjenga na kumfanya kuwa Mathematician mkubwa sana. Kabla THALES hajamkabidhi kwa mwanafunzi wake danistan ambapo hapa Pythagoras alisoma sana.
Hakuna mwenye ushahidi wa [HASHTAG]#proof[/HASHTAG] ya Pythagoras theorem, japo vitabu vingi vilijaribu namna ambazo "huenda" Pythagoras aliprove theorem yake hivyo. Lakini hadi sasa hakuna mwenye "uhakika", ila kwenye [HASHTAG]#RightAngledTriangle[/HASHTAG],
Pythagoras theorem (a²+b²=c²) haijawahi kuongopa.
NILIVYOJIFUNZA
1⃣ Pythagoras aliiona fursa ya kuzaliwa kipindi ambacho *Thales* yupo hai, akaitumia japo Thales alikuwa mzee sana na hakuwa anaweza kufundisha, lakini Pythagoras alipata makubwa sana.
2⃣ Pythagoras aliamua kuwa Philosopher mwenye mawazo tofauti na wenzie wote, lakini bado alikuwa sahihi na akapata kundi kubwa la watu waliomuunga mkono.
3⃣ Pythagoras hakutaka habari zake ziandikwe popote, lakini ziliandikwa na Pythagoras theorem (japo walioandika walimkosea) lakini imeisaidia jamii kiasi kikubwa sana.
4⃣ Pythagoras alizaliwa katika zama ngumu zaidi kimawasiliano lakini aliweza kusimamia alichokiamini na akapata wafuasi wengi sana.
5⃣ Pythagoras hakuridhika tu kuwa Philosopher akaamua kutafuta na taaluma nyingine ya Mathematics na ndiyo huyo mpaka leo tunamtaja.
Sasa turudi kwako wewe..
1. Una fursa ngapi zilizokuzunguka?
2. Una ugumu wowote wa kuwasiliana na mtu yeyote umtakaye duniani?
3. Una watu wangapi wanaofanya vizuri maeneo tofauti tofauti? Umewahi kuwafuata?
4. Umeshashirikishwa kwenye fursa ngapi na ukatoa visingizio?
5. Pythagoras hakutaka kuandikwa, ila dunia ilimbishia ikamwandika, je wewe hujatamani kuandikwa? Umefanya juhudi gani?
6. Unataka kizazi kijacho kikumbuke kwa namna gani??