Jifunze kuhusu Jimbo la Waziri wa Kilimo na Mifugo, Luhaga Mpina

masuka1

New Member
Dec 31, 2018
4
1
LIJUE KIMAENDELEOJIMBO INAOONGOZWA NA MH. MPINA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI....

Jimbo linaloongozwa na mh. mpina ni jimbo lenye jumla ya kata 13, na kila kata ina vijiji 3 hadi 5, leo nimependa nikujuze kidogo juu ya jimbo linaloongozwa na mpambanaji huyu.... *Mpina ni mbunge* Tangu mwaka 2005

1. *Sekta ya afya* jimbo la mh mpina (kisesa) lina jumla ya kata 13. kuna kituo kimoja tu cha afya( *mwandoya health centre* ) ambacho ndicho kinachohudumia kata zote 13(yaani zaidi ya watu elfu 60 wanahudumiwa na kituo kimoja cha afya), Aidha mpina ni mmoja wa wabunge wachache waliokaa kwenye ubunge pasipo kuwa na mafanikio kwenye sekta hii nyeti katika jamii yetu, aidha hatua ambao bado anahangaikia ni kujenga zahanati kwa kila kijiji ingawa hata hii hajafanikiwa kuwa na zahanati kwa kila kijiji, sijajua tatizo ni nini? Labda pengine kuwashawishi wananchi ni changamoto kwake au ana majukumu mengine mengi makubwa zaidi....

2. *Sekta ya elimu* , katika sekta hii mpango wa kuwa na shule kila kata pia jimbo hili ulifanikiwa ambapo mpaka sasa karibia kila kata ina shule ya sekondari ingawa hakuna shule hata moja ambayo *angalau imefanikiwa kuwa na maabara* inayofanya kazi( *kama anabisha akanushe)* Aidha sekta hii ya elimu bado imegubikwa na changamoto kubwa sana zikiwemo ukosefu na uchakavu wa vyumba madarasa, nyumba za walimu na kutokuwa na shule za msingi kwenye baadhi ya vijiji.....

3. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mh. mpina amefanikiwa kuchimbwa kwa kisima ambacho kinasaidia upatikanaji wa maji kwenye kijiji cha mwandoya( *makao makuu ya jimbo* ) ingawa inafikia muda maji yanaisha kwenye visima hivyo, aidha changamoto ya maji bado ni tatizo kwenye jimbo hili la mh. waziri...sema anasema amejitahidi kuleta umeme wa REA na barabara za vumbi zilizotengenezwa na kijiko cha halmashauri pamoja na zile za TASSAF anawambia wananchi amezileta yeye kuongoza jamii ambayo wasomi ni wachache au hawapo kabisa ni raha sana......

4. Kilimo, mifugo na uvuvi, hapa kilichobadilika ni mabadiliko ya movement permit kabla ya yy kuwa waziri hapakuwepo na movement permit ya mifugo ndani ya wilaya mtu akiwa anapeleka mifugo ya kutoka sehemu moja hadi nyingine kulikuwa hakuna hiyo tozo(movement permit) lakini alivyoshika madaraka ya kuwa waziri hizi tozo zimerudishwa mara moja naona huu ndio walichokipa wananchi wa jimbo la kisesa kutoka kwa mbunge wao.....aidha alivyoona uchaguzi umekaribia ameamua kwenda na mawaziri kadhaa jimboni kwake na kuwaahidi wananchi kuwa atawapatia eneo la malisho kutoka kwenye hifadhi ya maswa(sijui kama atatekeleza sisi tinasubiri).

My take

Mpina jitahidi kurudisha fadhila wa wananchi wako maendeleo ya jimboni hayafanani na muda ambao umeutumia ukiwa mbungu, wenzako wanatumia nafasi ya kuwa kwenye chama tawala kuishawishi serikali kupeleka maendeleo kwenye majimbo yao, mfano wakina Endrew chenge lakini kwa nini kisesa inaendelea kuwa na hali duni namna hii kimaendeleo?, mwishowe tutakuchoka kama kila baada ya miaka mitano hakuna hatua ambayo tunasogea kimaendeleo......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom