Jifunze kitu kupitia ushuhuda huu!!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,489
Kwa faida ya wengine....

Ijumaa iliyopita, nilikuwa darasani nikiwafundisha wanafunzi wangu ndipo mwanafunzi mmoja wa kike akainua mkono kuuliza swali. Nilimruhusu na akauliza swali rahisi sana ambalo nilidhani anapaswa kujua jibu lake maana tayari nilikuwa nimezungumzia mada hiyo wiki iliyopita.

"Kaa chini, tafadhari! Na sura yako mbaya! Muone!" ndilo jibu pekee nililompa. Darasa zima liliangua kicheko na alionekana kufedheheka sana.

Niliendelea na somo langu lakini nilihisi kuwa na hatia kwa sababu ya kile nilichokuwa nimesema. Nilimaliza kipindi changu na kuondoka.

Siku ya Jumapili, nilienda Kanisani. Mhubiri alikuwa akiongea juu ya nguvu ya ulimi.

Alizungumza juu ya jinsi unavyoweza kuwavunja moyo, kuwakatisha tamaa na kuwaangusha kabisa wengine kwa kile unachosema. Nilikumbuka kile kilichotokea Ijumaa na nikajiona ni mwenye hatia zaidi. Niliapa kuwa nitaenda kumuomba msamaha Jumatatu nikifika darasani.

Jumatatu alasiri, nilienda darasani lakini sikumuona yule mwanafunzi. Nilimuulizia kwa wenzake lakini hawakuonekana kujua ni nani hasa niliyekuwa nikimzungumzia.

Ndipo nikasema "ninamtafuta mtu niliyemtukana Ijumaa".

"Aah, huyo ni Furaha, mwalimu! Hayuko darasani leo" walijibu.
Rafiki yake ni nani? Niliuliza.

"Aisha", walijibu. Lakini Aisha pia hayupo darasani.

Ghafla, msichana aliye na Hijab aliingia. "Mwalimu, huyo ni Aisha" wanafunzi wangu walinijulisha.

Yuko wapi rafiki yako? Nikamuuliza.
"Yupi?" Alijibu bila kunitazama usoni.
Furaha! Nilisema.

Yuko chumba cha kuhifadhia maiti. Alijibu.
Jibu hilo lilinishtua! Chumba cha kuhifadhia maiti ????? Kufanya nini hapo ?? Niliuliza.
"Alikufa Ijumaa" Aisha alijibu.
Imekuaje ?????? Niliuliza.

Baadaye niligundua kuwa baada ya kipindi changu Ijumaa, Furaha aligongwa na gari lililokuwa likienda kwa kasi. Alikuwa akivuka barabara bila tahadhari, labda kwa sababu ya kile nilichosema.

"Mazishi yake ni Jumamosi na umealikwa pia, mwalimu" Aisha aliendelea.

Wakati nilikuwa nimesimama nilijaribu kuudhibiti mshtuko niliokuwa nao, Aisha alisema huku akilia, "Mwalimu, umemuua rafiki yangu".

Alikuwa sahihi! Ninapaswa kuwa muuaji! Wasichana wengine darasani walikuwa tayari wanalia! Sikujua niseme nini, ikiwa ni kuomba msamaha kwa rafiki wa Furaha au kwa roho ya Furaha.

Niliwasilisha barua yangu ya kujiuzulu siku iliyofuata ikiwa na maneno haya: Wapendwa Wahadhiri na Walimu, tafadhali acheni kutukana wanafunzi wenu. Wako shuleni ili kujifunza kutoka kwenu. Ingekuwa tayari wanajua, wasingekuwa shuleni!

Tafadhali fikiria kile unachosema kwa watu wengine. Je! Maneno yako yanaleta uhai au kifo kwa wasikilizaji?

ZINGATIO: HADITHI HII NI LAZIMA ISOMWE NA HAIWAHUSU WALIMU TU BALI SISI WOTE TUNAPOKUWA TUNAWASILIANA NA BINADAMU WENZETU: WATEJA, WANAFUNZI, WAZAZI, WENZIO, MARAFIKI NA KADHARIKA

Yatupasa tuwe waangalifu sana juu ya jinsi tunavyosemezana.

Asante.
 
Ushuhuda wako unaskitisha na unafundisha pia. Mrudie Mungu kwa kufanya toba na uombe msamaha.

Mathayo 12:36-37
Basi, nawaambieni, siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaa wanalosema. Maana kwa maneno yako utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako utahukumiwa kuwa na hatia.

1Petro 3:10
Kwa maana atakaye kupenda maisha, na kuona siku njema, auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.

Nyingine hii, tunatoa baraka na kulaani kwa nguvu ya ulimi ni Yakobo 3:8-10
 
Juzi kuna maneno niliyatamka nikimuambia mama yangu mzazi moja ya maneno nilimuambia" mama una matatizo".....niliongea kwa hisia na kweli nilimkamata...
 
Ushuhuda wako unaskitisha na unafundisha pia. Mrudie Mungu kwa kufanya toba na uombe msamaha.

Mathayo 12:36-37
Basi, nawaambieni, siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaa wanalosema. Maana kwa maneno yako utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako utahukumiwa kuwa na hatia.

1Petro 3:10
Kwa maana atakaye kupenda maisha, na kuona siku njema, auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.

Nyingine hii, tunatoa baraka na kulaani kwa nguvu ya ulimi ni Yakobo 3:8-10
Hivi kwa wale waoga na watenda dhambi siku ya hukumu itakuwaje?? si watajinyea km siyo kufa kabisaa!!! kabla hawajamuona Mungu akifungua vitabu vyake??

Yaani wataomba isiwepo!! au ihairishwe…….. ...ila sasa Jamani Shetani ndo namhurumia kabisaaa!....kuna huyu mtu anaitwa Jiwee hayayayaaaa!! hee yule bana atakuafa mara tatu kabla hajafikia kiti cha HUkumu!!

Na hiyo hukumu si masihara ipooo!! na ipo kweli! yaani nyie mfanye mazoezi ya kwenda kumshawishi Mungu awapunguzie adhabuu!!…….
 
Hivi mnajua siku hiyo ya Hukumu itakuwaje?? ngoja niwape kwa kifupi sana msjie sema sikuwaambia sasa nisikilizeni

Mkisha ingia hivi kunakoo hukoohukumuni mtakalishwa chini wooote wakosefu huku mmenyoosha mikono yote miwili mbele ya magoti yenu ……….anaingia jamaa mkubwaaa anawaka moto kila upande;

huyu atawaamrisha kwa kutamka '''Hiiiiiii yAAAP!!!!!!! ………..nyie mtaitikia tena kwa sauti kubwaa …….. ''mojaaaaa!''.....mbili .....tatu mojaaaaa'' ukiwa na bidi utapunguziwa……..ongezeni mengine….
 
Hivi mnajua siku hiyo ya Hukumu itakuwaje?? ngoja niwape kwa kifupi sana msjie sema sikuwaambia sasa nisikilizeni

Mkisha ingia hivi kunakoo hukoohukumuni mtakalishwa chini wooote wakosefu huku mmenyoosha mikono yote miwili mbele ya magoti yenu ……….anaingia jamaa mkubwaaa anawaka moto kila upande;

huyu atawaamrisha kwa kutamka '''Hiiiiiii yAAAP!!!!!!! ………..nyie mtaitikia tena kwa sauti kubwaa …….. ''mojaaaaa!''.....mbili .....tatu mojaaaaa'' ukiwa na bidi utapunguziwa……..ongezeni mengine….
 
Kwa faida ya wengine....

Ijumaa iliyopita, nilikuwa darasani nikiwafundisha wanafunzi wangu ndipo mwanafunzi mmoja wa kike akainua mkono kuuliza swali. Nilimruhusu na akauliza swali rahisi sana ambalo nilidhani anapaswa kujua jibu lake maana tayari nilikuwa nimezungumzia mada hiyo wiki iliyopita.

"Kaa chini, tafadhari! Na sura yako mbaya! Muone!" ndilo jibu pekee nililompa. Darasa zima liliangua kicheko na alionekana kufedheheka sana.

Niliendelea na somo langu lakini nilihisi kuwa na hatia kwa sababu ya kile nilichokuwa nimesema. Nilimaliza kipindi changu na kuondoka.

Siku ya Jumapili, nilienda Kanisani. Mhubiri alikuwa akiongea juu ya nguvu ya ulimi.

Alizungumza juu ya jinsi unavyoweza kuwavunja moyo, kuwakatisha tamaa na kuwaangusha kabisa wengine kwa kile unachosema. Nilikumbuka kile kilichotokea Ijumaa na nikajiona ni mwenye hatia zaidi. Niliapa kuwa nitaenda kumuomba msamaha Jumatatu nikifika darasani.

Jumatatu alasiri, nilienda darasani lakini sikumuona yule mwanafunzi. Nilimuulizia kwa wenzake lakini hawakuonekana kujua ni nani hasa niliyekuwa nikimzungumzia.

Ndipo nikasema "ninamtafuta mtu niliyemtukana Ijumaa".

"Aah, huyo ni Furaha, mwalimu! Hayuko darasani leo"
walijibu.
Rafiki yake ni nani? Niliuliza.

"Aisha", walijibu. Lakini Aisha pia hayupo darasani.

Ghafla, msichana aliye na Hijab aliingia. "Mwalimu, huyo ni Aisha" wanafunzi wangu walinijulisha.

Yuko wapi rafiki yako? Nikamuuliza.
"Yupi?" Alijibu bila kunitazama usoni.
Furaha! Nilisema.

Yuko chumba cha kuhifadhia maiti. Alijibu.
Jibu hilo lilinishtua! Chumba cha kuhifadhia maiti ????? Kufanya nini hapo ?? Niliuliza.
"Alikufa Ijumaa" Aisha alijibu.
Imekuaje ?????? Niliuliza.

Baadaye niligundua kuwa baada ya kipindi changu Ijumaa, Furaha aligongwa na gari lililokuwa likienda kwa kasi. Alikuwa akivuka barabara bila tahadhari, labda kwa sababu ya kile nilichosema.

"Mazishi yake ni Jumamosi na umealikwa pia, mwalimu" Aisha aliendelea.

Wakati nilikuwa nimesimama nilijaribu kuudhibiti mshtuko niliokuwa nao, Aisha alisema huku akilia, "Mwalimu, umemuua rafiki yangu".

Alikuwa sahihi! Ninapaswa kuwa muuaji! Wasichana wengine darasani walikuwa tayari wanalia! Sikujua niseme nini, ikiwa ni kuomba msamaha kwa rafiki wa Furaha au kwa roho ya Furaha.

Niliwasilisha barua yangu ya kujiuzulu siku iliyofuata ikiwa na maneno haya: Wapendwa Wahadhiri na Walimu, tafadhali acheni kutukana wanafunzi wenu. Wako shuleni ili kujifunza kutoka kwenu. Ingekuwa tayari wanajua, wasingekuwa shuleni!

Tafadhali fikiria kile unachosema kwa watu wengine. Je! Maneno yako yanaleta uhai au kifo kwa wasikilizaji?

ZINGATIO: HADITHI HII NI LAZIMA ISOMWE NA HAIWAHUSU WALIMU TU BALI SISI WOTE TUNAPOKUWA TUNAWASILIANA NA BINADAMU WENZETU: WATEJA, WANAFUNZI, WAZAZI, WENZIO, MARAFIKI NA KADHARIKA

Yatupasa tuwe waangalifu sana juu ya jinsi tunavyosemezana.

Asante.
Hiki kisa nilishasikiaga miaka mingiii huko nyumaa ni stories stories inayoelezwa ili kutuweka saaa binadam
 
Back
Top Bottom