Jifunze hapa: Namna nilivyoanza mpaka nilipofikia. Unaweza kupata kitu

umefanya kosa kubwa sana kutozingatia masomo. utakuja kujutia siku moja. sijui unasoma kozi gani, ila kuna kozi ambazo kama hautakuwa vizuri kichwani huwezi kuzifanyia kazi mtaani na wenzio uliowaacha kipesa watakuja kukuovertake kama umesimama siku moja. nakupa pole.
Kuna watu wana GPA za chini wapo sehemu nzuri tena wanatucheka tu. Mkuu komaa fanya ujasiamali wako utasonga hata mtu hakikupita usijali maisha sio mashindano
 
Ila hujatuambia huo uliwekwa ndani hosteli au ghetto na kama ghetto la Ukubwa gani, sio mambo ya hekaya

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyumba ninayokaa inavyumba vinne,na sebule pamoja na Dining hall.Kwahiyo nafasi yakuweka mchele ipo kubwaa sanaa.Na mwenye nyumba kwa kukubali juhudi zangu kuna kisehumu kaniambia nijenge nifanye kitu nilichomueleza.Unakaribishwa sana ni mbezi ya kimara sehemu moja panapoitwa Luguluni.Wengine huwa mnaamini kwa kuona,ingawa wapo wengi humu waliofika mpaka mahali napoishi.
 
Nimejifunza kwajinsi watu walivyo pata inspirational kwa ujumbe huu itabidi na mm niwe muwazi wa mafaniko yangu kwa kutoa post One Day, huenda watu watajifunza na kuamka.. Soon nitaiandaa nakuipost hapa watu waone nilivyo toka kwenye maisha duni mpaka sasa namiliki Account ya 84Milion, Nyumba ya 120milion na biashara ya dhamani kubwa zaidi ya 400mlioni. Kwa mihangaiko tangu nikiwa Chuon Udsm 2008-2011 na mpaka leo hii.. 2017.
Stay tuned guys.

Sent using Jamii Forums mobile app
Najua tu kuna watu wanatamani hii msg ingeambatana na thread ya .."natafuta mke"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mkuu...mungu azid kusimama na wew katk mapambano yko ya maisha utafanikiwa zaid..kuna meng nimejifunza toka kwako
 
Habari wakuu.

Mimi binafsi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo flani hapa mjini.Na nasoma course ya uhandisi.Nilipofika jijini kwa mara ya kwanza tangu nazaliwa ilikuwa 2014 mwezi wa kumi tare 9.Nilipotoka mkoani nikija mjini nilikuwa nashauku kubwa nikijua kuwa tayali nimeshatoka kimaisha.

Nilipofika mjini nilikuta baadhi ya watu wanaosoma walioko juu yangu(chuoni) wakisema ajira kupata nivigumu pindi umalizapo chuo.Labda mpaka uwe na lefa,na mimi nikiangalia home kwetu mimi ndio wakwanza kufika chuoni na maisha nimagumu.Nikawaza sana kuwa story nilizokuwa naambiwa pindi nikiwa advance zilikuwa za uongo.Nikasema kama ajira ni ngumu na nyumbani wanajua tayari mtu akishafika chuo katoka kimaisha,nikawaza namna gani nifanye ili nami nitoke kimaisha.

Kwa bahati nzuri nilipata mkopo,nikasema mimi kitakachonitoa pesa ya kujikimu boom.Nakumbuka kipindi kile 2014/2015 boom ilikuwa kama laki nne na 70.Kila baada ya miezi miwili,lakini wakijumlisha book and stationary laki mbili jumla boom la kwanza(mwanzo wa semister) inakuwa kama laki sita.Tukasaini boom bahati nzuri nikapewa hiyo laki sita na 70.Nikasema sasa ngoja nisichelewe nianze na hii hii.

Baada ya hapo nakumbuka nilichukua laki tatu na elfu 37 nikaenda kaliakoo nikawa nanunua viatu vya watoto na wanawake,nikawa nasafilisha kupitia salumu transport.Mzigo ulikuwa ukifika kule kuna mdada mmoja alikuwa ananiuzia baada ya hapo mzigo ukiisha nampa kidogo hela ya kutumia.Bahati nzuri huyu mdada alikuwa muaminifu sana,kiasi kwamba alikuwa zaidi ya chinga nikituma mzigo wiki tatu haziishi mzigo umeisha.

Nakumbuka mara ya kwanza nilipata faida kama laki na nusu,nilipompa ela kidogo akakataa akadai tukuze mtaji kwanza ntaanza kumlipa nikianza kuchukua mzigo wa Million moja.Kwa bahati mbaya baada yakumaliza mzigo wa pili yule dada akawa ameugua nikashindwa kuendelea na ile biashara.Nilihuzunika sana nikasema kweli ng'ombe wa maskini hazai.Nilivokaa muda kidogo nikiwa nawaza ile pesa niifanyie nini,nikakumbuka kuna jamaa yangu yupo kitaa kule kule mkoani. Nikaongea nae akakubali niwe nanunua mzigo namuagizia lakini sharti tutakuwa tunagawana faida nusu kwa nusu ikabidi nikubali.Baada yakumpelekea mzigo ulikaa muda kidogo kama mwezi mmoja na wiki mbili ndio ukaisha,trend yake nikaona sio nzuri nikaona nisipokuwa makini biashara inaweza isitoke vile navyotaka.Nikaona bora niwe naagiza asali kutoka Tabora nakuja kuuza DSM.Kutafuta soka lake nikalikosa ikanibidi nipige chini mambo ya biashara.Nikaona kufanya biashara nikupoteza muda kama huisimamii mwenyewe,nilivokaa kidogo nikasema lakini hamna ngoja niendelee kupambana.Ikanibidi ninunue mpunga niweke ndani kama wa laki tano hivi.Hiyo ilikuwa 2015 nakauweka ule mpunga ulivopabda bei nakuuza,nikapata faida kama ya laki tatu jumla nikawa kama na laki nane.

Niliamua ile pesa kuifungulia akaunti yake na nikasema sasa hii pesa lazima initoe.Nakumbuka ilikuwa mwaka jana mwezi wa nne nikaja nawazo humu lakuomba ushauli namna gani nimeanza kufanya biashara ya mchele.

Nilipata mawazo mengi na baadhi ya member walikuwa wakinipigia simu niwapelekea mchele.Nikipima nikipeleka mtu anazima simu,narudi na mzigo wangu.Lakini wapo pia waaminifu ambao walikuwa wakihitaji mchele nawapelekea nawapo wengine walifika kuona mpaka mahali napoishi.Nilijitahidi kupambana kadri ya uwezo wangu maana nakumbuka niliamua kununua mchele kama wa laki tano nikawa natembeza nyumba kwa nyumba,pia nikawa nawauzia baadhi ya mama ntilie mahali napoishi.

Changamoto kubwa niliyokumbana nayo ilikuwa muda mwingine naenda kupokea mchele saa nane usiku halafu nakaa mpaka saa kumi na moja nikisubili bodaboda waamke wanibebee mzigo wangu.Hakika ilikuwa changamoto kubwa.

Nikili kabisa kimasomo nilishuka sana mpaka nakumbuka nilipata supplementary 3 katika course wake 8.Halafu masomo mengine nikiangukia makalai.Lakini nilipambana nikasema sintokata tamaa lazima biashara initoe.Kipindi hiki nazungusha mchele nilitafuta na jama yangu mmoja kutoka mkoani,akaja ndio tukawa tunazunguka nae.Nilitembelea hostel zote za wanavyuo wanaojipikia nikiwauzia mchele.Hii biashara ilikuwa nzuri sana na faida niliiona.Nakumbuka kuna member mmoja humu aliniita sehemu nimpelekee mchele baada yakumpelekea alinipiga tafu fedha kidogo yakuongezea mtaji.Ikafikia kipindi nikawa naagiza mchele mpka wa millioni tatu.Mambo yakaenda baadhi ya watu wakanishauri nitafute frem.Nikaona nikitafuta fremu ntalazimika kulipa kodi jambo ambalo nilikuwa naona ni zuri lakini bado mtaji wangu mdogo.

Baada ya hapo nilipambana nikasema ngoja niache chuo nitafute fedha,wengine wakanishauri nisiache niendelee maana kilichonileta mjini ni shule kwanza sio biashara.Nikasema sawa lakini kiukweli shule niliipa asilimia 25.Asilimia 70 nilikuwa naitumia nje ya chuo kusaka pesa.Mpaka sasa biashara hii naweza kusema imenitoa kimaisha.Kwa nini nasema imenitoa kimaisha?.iko hivi

Baada yakupambana sana mpaka fedha kufikia million sita,kuna sehemu mama mmoja alikiwa na kiwanja nikamuomba nitumie kiwanja chake nijenge banda la mpira.Niliamua nitoe shilingi millioni nne na nusu nijenge banda la mpira niwe naonyesha.Kwa sababu maeneo haya nayoishi niliona watu wanaenda kuangalia mpira mbali,nahuyo anaeonyesha alikuwa analalamikiwa na watu na pia alitoza 1000 kwa kila mechi.Hapa millioni nne na nusu haikutosha nilikopwa million 2.5 Jumla banda zima lilikosti 7.0M

Baada ya kuanza ujenzi wa banda la mpira niliamua kumwambia jamaa yangu mmoja hivi awe analeta mchele namuuzia lengo likiwa nisipoteze wateja wangu.

Kuanzia tare 6 mechi ya ufunguzi wa ligi ya england nilianza kuonyesha mpira namuitikio haukuwa mbaya.Baanda langu nikubwa kidogo linauwezo wakuchukua kama watu 200. Nakumbuka hiyo tare 6 mwezi huu waliingia kama watu 132.Nakiingilio ni shillingi 700 kwa kila kichwa

700*132=92400.

Mechi iliyofuata ya ufunguzi uefa cup waliingia watu 243.

243*700=170100.

Baada yahapo nilisubili ligi kuu ianze kwa bahati nzuri wakiingia watu wachache ni watu 100 kwa zile timu nne kubwa,ambapo walipocheza man u,chelsea,arsenal,na liverpool kwa wikend nilipata kama laki tatu.

Hapo wakuu sijapigia mahesabu mechi ya barcelona na madrid pamoja na mechi za bongo,ambapo simba day nilipata kam elfu 82.Pia yanga walipocheza ruvu shuting nilipata kama elfu 50.

Sasa ukiangalia trend ikienda vizuri kwa mwezi ntakuwa napata kama 1.2M kwa lingi ya engaland.Bado ligi ya bongo ambayo sijaipigia mahesabu kwa sababu haijaanza nikafanya tathmini.kwa maana hiyo hata kama ligi ya bongo itaniingizia laki nne kwa mwezi sio mbaya.Nachofanya kwa sasa nalipa madeni kwanza wakuu .Lakini trend hii sio mbaya.

Mchele bado nauza wa mshikaji wangu ingawa huwa ananipa fedha kidogo ya udalali.Nafanya hayo yote nikiwa bado nipo chuo lengo langu kuu nataka mwakani ntakapomaliza chuo niwe na uwezo wakuingiza at least million 5 kwa mwezi.Kuna project nyingine nataka nifanye ambayo nahakika itaniingizia million 3/4 kwa mwezi na hii lazima ikamilike kabla sijamaliza chuo,mwakani mwezi 7.

ujumbe.
Anza kidogo kwa hicho hicho ulichonacho fursa nyingine utaziona ukiwa ndani ya safari yako.
hongera sana mku that's hustling.

ila ulipoingia kwenye biashara ya kuonyesha mpira hujatupa changamoto zake au haina changamoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenifurahisha hapo pa kwenda kwa mteja kisha anazima simu.
Online busness ni ngumu sana ila ukishatengeneza mtandao mambo yanaenda vizuri tu.
Hongera sana
 
Back
Top Bottom