Kompyuta Programming ni kipengele chenye Umuhimu wa Kipekee kabisa Katika Uwanja wa masomo ya Sayansi ya Komputer, vile vile ni Msingi mkuu wa Karne Ya ishirini na Moja, Ambayo imetajwa rasmi kuwa ni karne ya sience na technolojia, Vijana wengi wanaosomea maswala ya Kompyuta katika Nyanja za ICT na COMPUTER SCIENCE hususan katika nchi zetu za Africa mashariki wameshindwa kabisa Kuzingatia Fulsa hii, nahii ni kutokana na ukweli kuwa wameshindwa kung'amua kwamba computer Programming ni Roho ya Mfumo wowote Wa computer. Katika karne Ya Ishirini na Moja katika Kila Electronic mfumo wa computer umetumika, Katika kila Biashara Mfumo wa computer umetumika. Mifumo ya computer imetumika kwenye simu, Magali, TV, Lift za kwenye majengo, mawasiliano, ulinzi, usafirishaji, elimu, tiba, burudani nk.
Utafiti binafsi kutoka ndani ya codeMafia Forum unaonesha Kuwa 60% ya wanafunzi wanaohitimu masomo ya komputa science na ICT hufanya kazi zisizo husiana kabisa na maswala ya computer, katika 40% inayosalia 35% huingia katika ajira za IT na 5% tu ndio Hufanya shughuri mbali mbali zinazohusiana na Computer Programming. Kama utafiti huu ni kweli kwa asilimia 50! Basi kufikia mwaka 2020, Tanzania itakuwa na tatizo kubwa sana la kutokuwa na maprogrammer.
Kompyuta Programming ni kitu gani? Hiki ni kitendo cha kuiwezesha Kompyuta ikufanyie Kazi maalum kulingana na mahitaji yako. uwezeshaji huu mara zote Umekuwa Ukifanyika kwa kutumia Lugha maalum ambazo ndio tunaziita Programming Languages. Na hayo maelekezo yanayokuwa yameandikwa huitwa Program.Tafsiri hii ya CodeMafia imekuwa na Maana Halisi na inayoeleweka zaidi katika Lugha ya Kiswahili ukilinganisha na ile inayotumiwa na wataalamu wengi inayosema kuwa Computer programming ni Kitendo cha kuipa Maelekezo Komputer juu ya nini ifanye na kwa wakati gani.
PROGRAMMING LANGUAGES
Ili kutanua zaidi uelewa wa mfumo wa computer unavyoweza Kutekeleza kile unachotaka fikiria mfano wa mfanya kazi wa Kinyarwanda kwenye familia ya Kiswahili. Tatizo kubwa Litakalojitokeza ni kwamba maelekezo yoyote utakayotoa kwa mfanyakazi huyo hatoweza kuyaelewa kutokana na tofauti ya lugha baina yenu na ili kuleta maelewano lazima kuwe na mtua atakaekuwa anatafsiri maneno utakayokuwa ukimwambia mfanyakazi huyo. Tatizo hili limejitokeza pia kwenye computer Programming, Kwani mfumo wa maneno ambao computer inaweza kusoma ni vigumu sana kueleweka na binadamu, hivyo ili kurahisisha Uandikaji wa Programm ilibidi zitengenezwe lugha zingine ambazo zitakuwa rahizi kusomwa na kueleweka na binadamu.kisha kutafuta jinsi ambavyo maelekezo hayo yatatafsiriwa kuingia kwenye Maana ambayo computer itaweza kusoma na kuelewa.
Hivyo basi zoezi hili likatenganisha Lugha inayoandikwa na binadamu ambayo kitaalamu huitwa Source Code na ile inayosomwa na computer kuitwa objectCode huku zikiunganishwa na kiungo muhimu kinachofanya kazi ya kufasiri Kinachojulikana kama Compiler. Katika mchakato huu kitendo cha kubadilisha maelekezo kutoka katika Source Code Kwenda kwenye Object Code Kinajulikana kama Compilie, pengine kwa lugha yetu tutakuwa hatujakosea tukisema kukompile. Haya yanafaa kuwa maelezo mafupi sana juu ya programming Languages na kwakuwa Lengo la kozii hii si kuelezea Programming Languages basi Katika Lecture Hii ya kwanza tutaishia hapa. Kuanzia miaka ya 90 mpaka sasa kutokana na mahitaji mbali mbali ya Program kumekuwa na zaidi ya programming languages 40, zikiwemo zile Ambazo zimejizolea umashuhuri mkubwa kabisa kama JAVA, C, C++, C#, PHYTHON,
OBJECTIVE-C, PHP Nazinginezo. Kama jinsi nilivyotangulia kwenye Title ya kozi hapo juu, kwenye kozi hii tutatumia JAVA kwa ajili ya kupata introduction ya kufanya Computer Programming, na kwenye Lecture Ijayo moja kwa moja tutaanza na kutumia Lugha hii.