Terence Tao
Member
- Jul 22, 2025
- 6
- 4
Katika Advancement ya AI zikiwepo Grok, Gemini, Chat Gpt, Deepseek, muhimu sana kujifunza programming maana unaweza kuletewa program ambazo hujui maana yake ukaenda kutengeneza kitu ambacho kikileta shida unashindwa kuelewa namna ya kutatua . Muhimu tujifunze programming ili ziturahisishie kwenye kazi zetu.
Leo tutajifunza kuhusu
Comment
Data type
Operators in python
If statement
Loops
Lists
Dictionaries
Function
Python ni programming language ambayo inatumika kufanya vitu vifuatavyo
-kutengeneza website, inatumika katika Data Science and Data Analysis (Numpy , Pandas), Machine Learning and Artificial Intelligence , Desktop GUI Application ( Tkinter, PyQt ) , Game Development ( PyGame ), Computer vision and Image processing , Internet of Things n.k
Unaposave file lako andika jina unalotaka mwisho unaweka .py, unatakiwa uinstall python kwenye pc yako pia unaweza kutumia VS code kurun python au kama hutaki waweza kutumia online software mfano Replit , Google Colab ukaandika program zako huko na kuzirun n.k
Haya ni maneno ambayo ukiandika hayafinyiwi kazi katika program yako , Yawepo au yasiwepo hamna chochote kinachotokea . Ili umuhimu wake inamsaidia anayeandika program kuelezea Zaidi kuhusu code anazokuwa anaandika. Na pia atakayekuja kuzisoma hizo code ataelewa maana ya code zako.
Comment katika tunakuwa tunatumia alama ya # mwazoni mwa code yako . Baada ya # hata kama mbele ukiandika kikabila haina shida yoyote. kila ukianza mstari mwingine usisahau kutumia #
Data type .
-Data katika python zipo katika makundi mbali mbali ambazo ni
namba nzima tunaziita integers mfano 10, 30 ,56, 178 ,976 , -87 n.k
herufi tunaziita Characters mfano ‘a’ , ‘b’ , ‘c’ ,’d’ n.k
Kuna String ambazo hii ni muunganika wa Characters mfano “mkoa”, “chama”, “wanyama” n.k
desimali tunaziita decimal numbers au float au double mfano ni 4.5, 34.98, 837.86 n.k.
Boolean Type inakuwa ina dhamani mbili ya “True” au “False”
Zingine ni lists , dictionaries ambazo tutaiona Leo . n.k
UZURI MMOJA WAPO WA PYTHON HAUNA HAJA YA KUSEMA DATA TYPE NI IPI .
VARIABLE IN PYTHON
Data type ambazo tumezisema zinakuwa zinatunzwa ndani ya Variable. Mfano tulivyokuwa primary tulikuwa tuna let dhamani ya x=7, hapa x inakuwa ni variable inabeba dhamani ya 7. Tukiwa tunatumia string au charater Tunaweka Single Quote ( hii alama ' ') au Double quotes( hii alama " " ) ni wewe mwenyewe utakavyo amaua .
Code examples
x=10
miaka=40
mkoa=”dar”
distance=90.98
score=’A’
hapa x, miaka , mkoa , distance , score ni variable
NOTE:
Kwenye hizo code hapo juu hatuja sema aina za data ambazo tunakuwa tunadili nazo .
print()
Majibu.
Ili tuchukue data kutoka kwa mtumiaji wa program tunakuwa tunatumia neno input() , ndani ya mabano tunaweza kuweka ujumbe ambao mtu atakuwa anauona pindi atakapo kuwa anatumia program .
Code
Maelezo:
Mtumiaji akiweka umri wake tunaweza kuutunza huo umri kwenye variable mfano miaka . Na code ikabadilika na kuwa .
Code
Swali : Nataka variable yangu ambayo ni miaka iwe ni string au integers kwasababu kuna muda nataka niitumie kama namba na kuna muda nataka niitumie pamoja na maneno mengine
Maelezo
Ukitaka utumia variable miaka kama namba au integer ili uweze kufanya operation zingine inakuhitaji uweke neno int mwanzo wa neno input, au kama unataka miaka iwe ni string utaweka neno str kabla ya neno input.
Code
Or
Code
Operators in python.
Tukitaka kufanya mahesabu kama vile kujumlisha, kutoa , kugawanya , kuzidisha , . Tunakuwa tunatumia Arithmetic Operators.
Tukitaka kuangalia kama data ni kubwa kwa “ greater than” dhamani flani, au ndogo “ less than” , au “greater or equal to” au “less or equal to” ,au data flani ni sawa sawa na data nyingine .Tunakuwa tunatumia Relational Operator
Kuna Logical operator
Hii tunaitumia sana kuangalia logic za data .
Kuna Assignment operator
Kama tunataka variable mshahara iwe ni mshahara wako tunaandika
Code:
Tukiprint mshahara tutapata 300000, tukitaka kuongeza mshahara kwa kiasi cha 20,000
Tunaandika.
code
320000
Maelezo
Tukitaka kupunguza mshahara kwa kiasi cha 20000 basi tutaandika
Code
If statement ni moja kati ya program ya muhimu sana , Maisha yetu asilimia kubwa tunaishi na if statement , Mfano Kama ikifika mwakani ntanunua kiwanja, kama nikifikisha miaka kadhaa ntaacha kufanya kazi Fulani, Kama nikiwa na elfu moja ntapata MB kadhaa , kama nikiwa na hela kadhaa ntafanya jambo fulani , N.k. vyote hivo vipo ndani ya if statement . Unaweza kuwa na machaguzi Zaidi ya moja .
Chini ya if statement na elif tukuwa tunafanaya indentation , tuacha nafasi kwenye lines zinazofuata chini. Au unabonyeza tab kwenye pc yako
Namna tunavyoandika if statement au syntax yake:
if ------:
#your Code
elif ------:
#yourCode
elif------:
#yourCode
else:
#yourCode
Mfano 1:
Unachukua umri wa mtu na kudisplay either anaruhusiwa kuendelea mbele na au haruhisiwi kutokana na umri wake
Simple Code:
print(“ karibu katika mfumo wetu”)
miaka=int(input(“ weka miaka yako”))
if miaka>=18:
print(“unaruhisiwa kuendelea mbele”)
else:
Print(“ umri wako bado”)
Mfano 2:
Kuchagua kifurushi cha siku au wiki au mwezi
Loop inatumika kurun code mara kadhaa. Tukitaka kuonyesha vitu mara kadhaa tunakuwa tunatumia loop. Mfano unapoenda kutoa pesa bank , ATM inavyohesabu hela mara kadhaa ile ni Loop, Saa inapokuwa inaccount seconds , minutes n.k hiyo ni Loop. Mwalimu anapokuwa anahesabu idadi ya wanafunzi wake hiyo ni Loop. Unapokuwa unaangalia video kadhaa kwenye mitandao ya kijamii hiyo ni loop N.k.
Kuna while loop , for Loop katika python
Syntax yake
While conditions:
#code
Note,
Baadaya ya neno while loop na condictions kunakuwa na vidoti viwili.
Chini ya while loop tunafanya indentation kwa maana tunaacha nafasi au unaweza kubonyeza tap. Lakini mara nyingi inakuwa automatic tu.
Mfano 1:
Tunataka kuonyesha namba kuanzia namba 1 mpaka 10 , Cha kwanza lazima tuwe na variable au “neno” ambalo litatunza namba moja ( Code: namba=1) , baada ya hapo tutakuwa na condition kuangalia kama namba yetu haijazidi kumi (Code : while namba<=10: ) , then tutakuwa tunaongeza dhamani ya namba kwa moja ( moja+=1)
Mfano wa Code:
Kwenye mfano wa hapo juu tuweza kuamua kuruka namba zionekane 1, 4 ,7, 10 . kinachobadilika ni kwenye namba+=1 tunaweka namba+=3
Simple Code:
Break statement
Break statement inatumika endapo tunataka loop yetu iishie sehemu flani .
Mfano 3
Kudisplay number 1 mpaka 10 lakini ikifika namba saba program isiendelee.
Njia
Tunaweka inavalue ya mwanzo kuwa moja ( number=1), Tunaweka value ya mwisho ndani ya while loop ( while<=10) , baada ya hapo tunasema ikifika number 7 program isiendelee ( if number==7 break) , tunakuwa tunaruka number yetu kwa dhamani ya moja (number+=1)
Simple code
Mfano 4: Kumuomba user aweke neno la sili asipo weka “password123” isimruhusu kuendelea mbele.
Simple code .
For statement.
Tunaweza kuwa na list ya vitu , Mfano List ya magari, majina ya watu, List ya matunda , List ya mikoa . Tunaweza kutumia for Loop kuonyesha list zote .
Mfano 1:
List ya mikoa kwa mfano Dar , Mbeya, Arusha , Dodoma, Tanga, Mwanza . ( Code: mikoa = [ ‘Dar’, ‘Mbeya’, ‘Arusha’,’Dodoma’,’Mwanza’] ) hapa tunakuwa tumetengeneza list teyali, Sasa tunatumia for loop kuonyesha mikoa yote ( Code: for x in mikoa: ) , x inakuwa inachukua mkoa moja baada ya mwingine ,x=’Dar’ next x=’Mbeya’ next x=’Arusha’ n.k. mpaka list zote ziishe alafu tunaweza kuzionyesha (Code : print(x) )
Simple code
Mfano 2:
Tunaweza kutumia for loop ndani yake pia tukaweka for loop ,Tunakuwa tunaita nested loop.
-unaweza kuwa na aina za simu Samsung,Iphone, Pixel ( Code: simu= [‘Samsung’, ‘Iphone’, ‘pixel’] tukawa na mikoa tuliyoiona juu ,mikoa kwa mfano Dar , Mbeya, Arusha , Dodoma, Tanga, Mwanza . ( Code: mikoa = [ ‘Dar’, ‘Mbeya’, ‘Arusha’,’Dodoma’,’Mwanza’] ). Sasa tunaweza kudisplay kila mkoa ukaonyesha aina za simu zinazopatikana. (Code: for x in mikoa: ) ikafuatia for loop nyingine ( Code: for y in simu: ) baada ya hapo tukadisplay mikoa ikafuata aina za simu
Simple code
Mfano 3
Kuunganisha pamoja for loop na if statement .
Kutengeneza list ya namba (Code: namba=[1,2,3,4,5,6,7,8] ) , katika hizi number tutazidisplay kwa kutumia for loop ( Code : for x in namba) baada ya hapo tutaangalia kama number inagawanyika kwa 2 ( Code : if x%2 == 0 ) , tutaonyesha kuwa hiyo number ni even number
Simple Code
Mfano 4:
Kudisplay numbers 1 to 9 kwa kutumia range()
Lists
Inakuwa na mchanganyiko wa namba, maneno , vitu mbali mbali kama object. Tunaweza kuongeza vitu ndani ya List , tunaweza kufuta vitu ndani ya list , tunaweza kucount idadi ya vitu ndani ya List.
Mfano .
List ya nchi , ( Code: nchi=[“Tanzania”,”Kenya”,”Uganda”]) , tukitaka kuziona tunaandika( code: print(nchi))
Simple code
Tukitakana kuziona kwa kutumia for loop , ( code: for x in nchi) baada ya hapo tunazidisplay
Tukitaka kuongeza mfano nchi nyingine tunakuwa tunatumia neno append ( code: nchi.append(“Uganda”). Hii tunakuwe tunaweka neno moja tu ndani yake
nchi=[“Tanzania”,”Kenya”,”Uganda”]
Itaendelea...
Leo tutajifunza kuhusu
Comment
Data type
Operators in python
If statement
Loops
Lists
Dictionaries
Function
Python ni programming language ambayo inatumika kufanya vitu vifuatavyo
-kutengeneza website, inatumika katika Data Science and Data Analysis (Numpy , Pandas), Machine Learning and Artificial Intelligence , Desktop GUI Application ( Tkinter, PyQt ) , Game Development ( PyGame ), Computer vision and Image processing , Internet of Things n.k
Unaposave file lako andika jina unalotaka mwisho unaweka .py, unatakiwa uinstall python kwenye pc yako pia unaweza kutumia VS code kurun python au kama hutaki waweza kutumia online software mfano Replit , Google Colab ukaandika program zako huko na kuzirun n.k
[COLOR=rgb(184, 49, 47)]Comment katika python[/COLOR]
Haya ni maneno ambayo ukiandika hayafinyiwi kazi katika program yako , Yawepo au yasiwepo hamna chochote kinachotokea . Ili umuhimu wake inamsaidia anayeandika program kuelezea Zaidi kuhusu code anazokuwa anaandika. Na pia atakayekuja kuzisoma hizo code ataelewa maana ya code zako.Comment katika tunakuwa tunatumia alama ya # mwazoni mwa code yako . Baada ya # hata kama mbele ukiandika kikabila haina shida yoyote. kila ukianza mstari mwingine usisahau kutumia #
Data type .
-Data katika python zipo katika makundi mbali mbali ambazo ni
namba nzima tunaziita integers mfano 10, 30 ,56, 178 ,976 , -87 n.k
herufi tunaziita Characters mfano ‘a’ , ‘b’ , ‘c’ ,’d’ n.k
Kuna String ambazo hii ni muunganika wa Characters mfano “mkoa”, “chama”, “wanyama” n.k
desimali tunaziita decimal numbers au float au double mfano ni 4.5, 34.98, 837.86 n.k.
Boolean Type inakuwa ina dhamani mbili ya “True” au “False”
Zingine ni lists , dictionaries ambazo tutaiona Leo . n.k
UZURI MMOJA WAPO WA PYTHON HAUNA HAJA YA KUSEMA DATA TYPE NI IPI .
VARIABLE IN PYTHON
Data type ambazo tumezisema zinakuwa zinatunzwa ndani ya Variable. Mfano tulivyokuwa primary tulikuwa tuna let dhamani ya x=7, hapa x inakuwa ni variable inabeba dhamani ya 7. Tukiwa tunatumia string au charater Tunaweka Single Quote ( hii alama ' ') au Double quotes( hii alama " " ) ni wewe mwenyewe utakavyo amaua .
Code examples
x=10
miaka=40
mkoa=”dar”
distance=90.98
score=’A’
hapa x, miaka , mkoa , distance , score ni variable
NOTE:
Kwenye hizo code hapo juu hatuja sema aina za data ambazo tunakuwa tunadili nazo .
Ukitaka uonyeshe maneno kwenye Screen katika python
Ukitaka uone data zako au maneno yaonekane katika screen kwa python unakuwa unatumia neno print ikifatiwa na mabano .Hili ni neno ambalo tutalitumia sana katika python.print()
Getting value from the user
Swali: Nawezakaje kuchukua data kutoka katika mtumiaje wa program yangu?Majibu.
Ili tuchukue data kutoka kwa mtumiaji wa program tunakuwa tunatumia neno input() , ndani ya mabano tunaweza kuweka ujumbe ambao mtu atakuwa anauona pindi atakapo kuwa anatumia program .
Code
>>input(“ weka umri wako”)
Maelezo:
Mtumiaji akiweka umri wake tunaweza kuutunza huo umri kwenye variable mfano miaka . Na code ikabadilika na kuwa .
Code
>>miaka=input(“weka umri wako ”)
Swali : Nataka variable yangu ambayo ni miaka iwe ni string au integers kwasababu kuna muda nataka niitumie kama namba na kuna muda nataka niitumie pamoja na maneno mengine
Maelezo
Ukitaka utumia variable miaka kama namba au integer ili uweze kufanya operation zingine inakuhitaji uweke neno int mwanzo wa neno input, au kama unataka miaka iwe ni string utaweka neno str kabla ya neno input.
Code
>>miaka= int(input(“ weka umri wako”))
Or
Code
>>miaka =str(input(“ weka umri wako”))
Operators in python.
Tukitaka kufanya mahesabu kama vile kujumlisha, kutoa , kugawanya , kuzidisha , . Tunakuwa tunatumia Arithmetic Operators.
| Arithmetic operators | +, -, *, /, % |
Tukitaka kuangalia kama data ni kubwa kwa “ greater than” dhamani flani, au ndogo “ less than” , au “greater or equal to” au “less or equal to” ,au data flani ni sawa sawa na data nyingine .Tunakuwa tunatumia Relational Operator
| Relational Operator | <, >, <=, >=,= =, ! = |
Kuna Logical operator
Hii tunaitumia sana kuangalia logic za data .
| Logical operator | AND, OR, NOT |
Kuna Assignment operator
| Assignment operator | =, +=, -=, *=, %= |
Kama tunataka variable mshahara iwe ni mshahara wako tunaandika
Code:
Maelezo:>mshahara=300000
Tukiprint mshahara tutapata 300000, tukitaka kuongeza mshahara kwa kiasi cha 20,000
Tunaandika.
code
au>>mshahara=mshahara+20000
>> mshahara+=20000
Output>>print(mshahara)
320000
Maelezo
Tukitaka kupunguza mshahara kwa kiasi cha 20000 basi tutaandika
Code
>>mshahara-=20000 au
>>mshahara= mshahara-20000
If statement ni moja kati ya program ya muhimu sana , Maisha yetu asilimia kubwa tunaishi na if statement , Mfano Kama ikifika mwakani ntanunua kiwanja, kama nikifikisha miaka kadhaa ntaacha kufanya kazi Fulani, Kama nikiwa na elfu moja ntapata MB kadhaa , kama nikiwa na hela kadhaa ntafanya jambo fulani , N.k. vyote hivo vipo ndani ya if statement . Unaweza kuwa na machaguzi Zaidi ya moja .
Chini ya if statement na elif tukuwa tunafanaya indentation , tuacha nafasi kwenye lines zinazofuata chini. Au unabonyeza tab kwenye pc yako
Namna tunavyoandika if statement au syntax yake:
if ------:
#your Code
elif ------:
#yourCode
elif------:
#yourCode
else:
#yourCode
Mfano 1:
Unachukua umri wa mtu na kudisplay either anaruhusiwa kuendelea mbele na au haruhisiwi kutokana na umri wake
Simple Code:
print(“ karibu katika mfumo wetu”)
miaka=int(input(“ weka miaka yako”))
if miaka>=18:
print(“unaruhisiwa kuendelea mbele”)
else:
Print(“ umri wako bado”)
Mfano 2:
Kuchagua kifurushi cha siku au wiki au mwezi
| Loop in python |
Kuna while loop , for Loop katika python
| While loop |
Syntax yake
While conditions:
#code
Note,
Baadaya ya neno while loop na condictions kunakuwa na vidoti viwili.
Chini ya while loop tunafanya indentation kwa maana tunaacha nafasi au unaweza kubonyeza tap. Lakini mara nyingi inakuwa automatic tu.
Mfano 1:
Tunataka kuonyesha namba kuanzia namba 1 mpaka 10 , Cha kwanza lazima tuwe na variable au “neno” ambalo litatunza namba moja ( Code: namba=1) , baada ya hapo tutakuwa na condition kuangalia kama namba yetu haijazidi kumi (Code : while namba<=10: ) , then tutakuwa tunaongeza dhamani ya namba kwa moja ( moja+=1)
Mfano wa Code:
Kwenye mfano wa hapo juu tuweza kuamua kuruka namba zionekane 1, 4 ,7, 10 . kinachobadilika ni kwenye namba+=1 tunaweka namba+=3
Simple Code:
- Tunaweza kutumia if statement ndani ya while Loop . Kwa mfano tunataka kudisplay even numbers . Even numbers ni namba zinazokawanyika kwa mbili pasina ya baki. ( code yake inakuwa: namba%2= =0) . Modulus (%) inakuwa inaangalia baki . sawa sawa mbili inakuwa na maana ya je baada ya kugawanya baki inakuwa sawa sawa na 0 . Ikiwa ni kweli basi code za chini yake zinafanyiwa kazi .
Break statement
Break statement inatumika endapo tunataka loop yetu iishie sehemu flani .
Mfano 3
Kudisplay number 1 mpaka 10 lakini ikifika namba saba program isiendelee.
Njia
Tunaweka inavalue ya mwanzo kuwa moja ( number=1), Tunaweka value ya mwisho ndani ya while loop ( while<=10) , baada ya hapo tunasema ikifika number 7 program isiendelee ( if number==7 break) , tunakuwa tunaruka number yetu kwa dhamani ya moja (number+=1)
Simple code
Mfano 4: Kumuomba user aweke neno la sili asipo weka “password123” isimruhusu kuendelea mbele.
Simple code .
FOR LOOP |
For statement.
Tunaweza kuwa na list ya vitu , Mfano List ya magari, majina ya watu, List ya matunda , List ya mikoa . Tunaweza kutumia for Loop kuonyesha list zote .
Mfano 1:
List ya mikoa kwa mfano Dar , Mbeya, Arusha , Dodoma, Tanga, Mwanza . ( Code: mikoa = [ ‘Dar’, ‘Mbeya’, ‘Arusha’,’Dodoma’,’Mwanza’] ) hapa tunakuwa tumetengeneza list teyali, Sasa tunatumia for loop kuonyesha mikoa yote ( Code: for x in mikoa: ) , x inakuwa inachukua mkoa moja baada ya mwingine ,x=’Dar’ next x=’Mbeya’ next x=’Arusha’ n.k. mpaka list zote ziishe alafu tunaweza kuzionyesha (Code : print(x) )
Simple code
Mfano 2:
Tunaweza kutumia for loop ndani yake pia tukaweka for loop ,Tunakuwa tunaita nested loop.
-unaweza kuwa na aina za simu Samsung,Iphone, Pixel ( Code: simu= [‘Samsung’, ‘Iphone’, ‘pixel’] tukawa na mikoa tuliyoiona juu ,mikoa kwa mfano Dar , Mbeya, Arusha , Dodoma, Tanga, Mwanza . ( Code: mikoa = [ ‘Dar’, ‘Mbeya’, ‘Arusha’,’Dodoma’,’Mwanza’] ). Sasa tunaweza kudisplay kila mkoa ukaonyesha aina za simu zinazopatikana. (Code: for x in mikoa: ) ikafuatia for loop nyingine ( Code: for y in simu: ) baada ya hapo tukadisplay mikoa ikafuata aina za simu
Simple code
Mfano 3
Kuunganisha pamoja for loop na if statement .
Kutengeneza list ya namba (Code: namba=[1,2,3,4,5,6,7,8] ) , katika hizi number tutazidisplay kwa kutumia for loop ( Code : for x in namba) baada ya hapo tutaangalia kama number inagawanyika kwa 2 ( Code : if x%2 == 0 ) , tutaonyesha kuwa hiyo number ni even number
Simple Code
Mfano 4:
Kudisplay numbers 1 to 9 kwa kutumia range()
Lists
Inakuwa na mchanganyiko wa namba, maneno , vitu mbali mbali kama object. Tunaweza kuongeza vitu ndani ya List , tunaweza kufuta vitu ndani ya list , tunaweza kucount idadi ya vitu ndani ya List.
Mfano .
List ya nchi , ( Code: nchi=[“Tanzania”,”Kenya”,”Uganda”]) , tukitaka kuziona tunaandika( code: print(nchi))
Simple code
Tukitakana kuziona kwa kutumia for loop , ( code: for x in nchi) baada ya hapo tunazidisplay
Tukitaka kuongeza mfano nchi nyingine tunakuwa tunatumia neno append ( code: nchi.append(“Uganda”). Hii tunakuwe tunaweka neno moja tu ndani yake
nchi=[“Tanzania”,”Kenya”,”Uganda”]
| Operation | Maelezo | Majibu |
| nchi.append(“Rwanda”) | Inaongeza nchi ya Rwanda kwenye list | print(nchi) ['Tanzania', 'Kenya', 'Uganda', 'Rwanda'] |
| nchi.clear() | Inafuta kila kitu kilichopo kwenye list za nchi | print(nchi) [] |
| nchi.sort() | Inapanga list kutokana na alphabetical order | print(nchi) ['Kenya', 'Tanzania', 'Uganda'] |
| nchi.reverse() | Cha mwisho kwenye list kinakuwa cha kwanza na cha kwanza kinakuwa cha mwisho | print(nchi) ['Uganda', 'Kenya', 'Tanzania'] |
| nchi.pop() | Inaondona dhamani ya mwisho kwenye list | print(nchi) ['Tanzania', 'Kenya'] |
Itaendelea...