Jiepushe kurudiana na mpenzi wako wa zamani ni hatari sana kwako

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
18,730
29,262
Mapenzi/Mahusiano ni kama chuo/darasa, unapata mengi ya kujifunza toka
kwa mwenzako uliyenaye kwenye huo uhusiano. Mnaweza achana kwa makubaliano mazuri au kwa vurugu na dharau pamoja na kejeli kibao.

Hutokea mara nyingi mmoja wenu akarudi kama rafiki mwema aliyebadilika na kuhitaji nafasi ya pili ya mahusiano/mapenzi tafadhali usikurupuke kuingia katika mtego huo.

Unaweza kuhatarisha afya yako bila kujua.Baadhi ya wanaorejea na kuomba mrudiane wanakuwa na agenda za siri kama hizi

1- Kule alikoenda aliyempata kashindwa kufikia vigezo vya ubora ulivyonavyo wewe ndo maana karudi mazingira yamemrudisha kwako vinginevyo asingerudi, sio upendo.


2- Anaweza kuwa na kinyongo moyoni nawewe kwa namna uliyomuacha sasa anataka kulipa kisasi kwa gharama yoyote,sio lazima atoe uhai wako katika hili.

3- Maisha yamemshinda yamekuwa ni kinyume na matarajio yake, angefanikiwa asingerudi, akirudi huyu lazima akufilisi akirudi kwako.


4- Wako wanaorudi kujaribu hana nia ya dhati,lolote litakalokuwa liwe,mtu wa aina hii, ataishia kukupotezea mda na raslimali zako.

5 - Wako wanaorudi huku bado wanamahusiano waliyoyaanzisha baada ya kuachana nawewe awali utashangaa mwanamke/mwanaume ana stress za mapenzi mda mwingi chanzo kumbe ni kule alikotoka bado yuko naye.


Ni hayo kwa leo, bado maamuzi ni yako kwani maswala ya mapenzi ni vigumu kumwamulia mtu, unampa ushauri kutokana na uzoefu ambao nao hauna kanuni, unatofautiana baina ya mtu na mtu.
 
Kamwe sitorudia matapishi nilijufunza kumwacha aende ,,,,,,,,, naamini ipo siku yang nitasahau maumivu niliyoyapata , nitangaaa kama dhahabu, bado nakusubir mtarajiwa wang sijui utakuja kwa njia ipi
Kabisa mdada... kama aliweza kukumiza mwanzoni... hata shindwa kukuumiza tena. Alaf watu itabid wakubali some peoples dont change
 
Kabisa mdada... kama aliweza kukumiza mwanzoni... hata shindwa kukuumiza tena. Alaf watu itabid wakubali some peoples dont change
That's true Kuna watu hawabadiliki,,,, raha yao wakuone unaumia,, ila nahis watu kama hao wako na laana za kwao hakika halaf huwa wanapenda kutuumiza sisi mabinti tuliokulia familia zenye nadhan na hofu ya Mungu, ila naamin Mungu wang sio kiziw atanipa muda utakapofika
 
Kuna watu... unawapa mpaka third chances... lakin wapi... wanarudia vituko vile vile...
Kama unampenda kweli hutochoka mapema kuvumilia,mueleweshe Binadamu wengine hua wagumu kuelewa,mfano
mbona wanawake wengine wanawafumania waume zao na sms,mara kamkuta live na mwanamke mwengine na vituko vingi lakini still ana vumilia mbona wanaume wanakua na stahmalah fupi?
 
Mapenzi ya kweli ni tofauti wengi wenu mnaosema hamwezi kurudia mlikuwa hampendani, ulijipendekeza au penzi la kushawishiwa. Mshusiano yenye mapenzi ya kweli hayafutiki mioyoni mwa wapendanao, mahusiano mengi niya uongo ongo tu.

umenena kweli mkuu, kuna mwanamke nilimpenda jamani acheni kabisa hivi sasa ni mwaka amesepa lakini bado anaishi moyoni mwangu, kila siku lazima nimkumbuke G wangu jamani.
 
umenena kweli mkuu, kuna mwanamke nilimpenda jamani acheni kabisa hivi sasa ni mwaka amesepa lakini bado anaishi moyoni mwangu, kila siku lazima nimkumbuke G wangu jamani.
Ni kweli haswa kama ulimoenda kweli.. huwa inachukua muda sana. Lakin pia ina depend.. mli tengana kwa jinsi gani...
 
Hii cjui itasound kwa kwt tulio nao kwa ss kama kwel mnapendana,am just talk by experience,nliachana na mpnz wangu ila nikiri kuwa mm ndo nlikuwa mwny makosa,ila kwa nlichomtendea nliona uwesekano mdogo wa kurudiana nae nkaamua ku move on,tukawa kila mtu hanq mawasiliano na mwenzie,imekaa mwez akaamua kunitafuta na kusema ukwel ameshndwa kuwa comfortable kwa kipnd chote hicho due uwepo wangu ameukosa,ilq niseme tu hata mimi nlikuwa naumia sanaa kumpoteza,rgt now tumerudiana tena kwa kasi ya 4g ila nnachoomba nisimkwase tena kwan yy kwel anaonesha upendo wa kwel
 
Ndio maana huwa staki mazoea na ex hata aje analia wengi wao hurudi huko yakiwashinda, au hurudi kulipiza kisasi
 
Back
Top Bottom