JICHAGULIE DUNIA YAKO
_______________________________________________
Sahau kuhusu mengineyo, kinachofurahisha ni kuwa katika dunia yetu hii kila mtu ni staa...ni staa katika dunia yake; tena kila mmoja ni shujaa...lakini ni shujaa katika dunia yake; isitoshe kila mtu ni mjuaji...lakini ujuaji wake unadhihirika zaidi katika dunia yake.
Kwa kifupi kila mmoja anajidai na kutamba katika uwanja wake wa nyumbani; ndiyo dunia yake!
Kuna mwingine ni mjanja mchana, lakini usiku ni bwege wa kutupa. Tena mwingine mchana ni bwege kabisa ila usiku anacharuka na kujanjaruka kuliko popo!
Rafiki yangu mmoja anajua sana mambo yahusuyo mpira wa miguu, mkianzisha mjadala kuhusu soka hata saa nane za usiku, mishipa humsimama. Hana asichokijua kuhusu kabumbu, tena huongea kama chiriku. Lakini ukimhamisha ghafla na kuanzisha mada inayohusu siasa na uchumi wa nchi na dunia kwa ujumla, hunyong'onyea ghafla na kuanza kupiga miayo. Siyo kwamba hapendi kuongea, ila hana anachokijua kuhusu siasa za ulimwengu. Sio dunia yake.
Tena kuna watu wanajua sana mambo ya dini. Wanapenda sana kufuatilia maandiko matakatifu na kujaribu kuyaishi. Waulize chochote kuhusu maandiko watakujibu. Waeleze kuhusu shida yako watakuombea na kukufanyia kila aina ya dua huku wakikufariji kwa maneno ya Mungu. Hawaamini katika kushindwa kwa kudra za Mwenyezi. Hiyo ndiyo dunia yao waliyoamua kujichagulia.
Lakini pia wapo waliobobea kwenye imani nyeusi; ushirikina, uchawi na mambo ya kuloga. Hawa huwaambii kitu kuhusu makafara, mazindiko na kinga. Wanajua kila aina ya dawa, hadithi na visa vya kichawi. Ukikaa nao unaweza kukimbia kwa hofu, maana kwao kila kitu wanahusianisha na nguvu za giza. Ukikohoa kidogo watakushauri kupiga ramli. Nzi akikutulia mdomoni utaambiwa ni zongo! Wao hawaamini kabisa katika magonjwa. Hawaamini katika biashara bila kufukia ndumba, au kazi bila kuvaa hirizi...kutwa kucha ni kupasua nazi.. Hiyo ndiyo dunia yao, waliyojichagulia. Ni mashujaa katika eneo hilo!
Mjeda aweza kuwa shujaa kwenye uwanja wa vita lakini linapokuja suala la majeraha makubwa ya kutisha anaweza kukimbia. Daktari ndiye shujaa kwenye eneo hilo. Yeye haogopi kuangalia kidonda. Hata kama utumbo uko nje au mifupa au ubongo wa mtu umemwagika, yeye ndiye shujaa pekee mwenye uwezo wa kucheza na majeraha ya binadamu bila kinyaa wala hofu! Ndiyo dunia aliyoichagua.
Halafu kuna yule shujaa na supastaa wa kila kitu, ogopa sana!
Huyu anajua kila kitu. Mkianzisha mambo ya soka yumo. Kwenye ubishi wa dini yumo, tena na vifungu vyote anavijua. Lakini wakati huo ni fundi na mjuvi mkubwa kwenye mambo ya ushirikina. Anazijua kila ndumba na alishafanya kila aina ya zindiko. Anawajua waganga wa kienyeji kwa majina na vitengo vyao.
Lakini ukimuhamishia kwenye ulimwengu wa totoz ndo usipime. Anawajua vilivyo, na anaweza kuwachambua hata kwa vijiji wanavyotoka, tokea Mchinga, mtama mpaka Chitohori Kwa kifupi ni much- knower wa kiwango cha juu.
TUSIMALIZE MANENO
Muhimu ni kutuliza utashi wako na kuchagua dunia yako, ndicho nachotaka kusema. Amua mwenyewe aina ya ushujaa na ustaa unaoutaka. Hakuna wa kukuamulia zaidi yako mwenyewe. Dakika tisini za mchezo zikiisha usijekusema ningejua.
The world is all yours