jibu la Adhana hili hapa

jibu la Adhana hili hapa

MartinCoder

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2018
Posts
700
Reaction score
630
HISTORIA YA ADHANA

Katika mji wa Makka, idadi ya Waislam ilikuwa ndogo. Walikuwa Wanaweza kufanya Jama'ah (mkusanyiko) bila hata kuitana. Wakati Mtume (Muhammad sala na amani ziwe juu yake) alipofika /alipohamia Madina, idadi ya Waislamu ilianza kuongezeka.

Mtume aliamua kujenga Masjid kwa ajili ya Salah za mara kwa mara. Katika mwaka wa pili wa Hijrah (baada ya kuhama kutoka Makka kwenda Madina), idadi ya Waislamu iliongezeka. Watu walikuwa wakitangaza kwa sauti kubwa maneno yafuatayo, "'As-Salat ul-Jami'ah, salah ya jama'ah iko tayari." Wale waliokuwa wakisikia wito huo walikuwa wanakuja kujiunga na Salah. Waislamu waliona kuna haja ya kutafuta njia nyingine ya kuwajulisha watu kuja kuswali. Mtume aliwaomba maswahaba wake ushauri kuhusu jambo hilo.

Baadhi ya maswahaba walipendekeza kuwa Waislamu wafanye kama Mayahudi,yaani wapige pembe kutangaza wakati wa Salah (muslims should blow a horn to announce the time for the Salah). maswahaba Wengine walipendekeza kuwa Waislamu wapige kengele kama Wakristo wanavyofanya katika makanisa yao. maswahaba Wachache walipendekeza kuwa Waislamu wafanye kama waabudu moto,yaani wawashe moto kuwaita watu kuja kwenye salah.

Mtume hakulidhika na mawazo yote yaliyotolewa na maswahaba. Alisubiri kusikia wazo bora au kupokea mwongozo kutoka kwa Allah (Mwenyezi Mungu).

Siku moja, Swahaba mmoja ,jina lake Abdullah ibn Zaid , alikuja kwa Mtume na akasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niliota ndoto nzuri jana usiku."

"Mtume akamuuliza ni ndoto gani hiyo uliota? Abdullah ibn Zaid akajibu, "Nilimuona mtu kwenye ndoto amevaa mavazi ya kijani, akaja na kunifundisha maneno yanayotakiwa kusemwa katika 'Adhana’ =(calling for salah) na alinishauri kuwaita watu kuja katika salah kwa kutumia maneno haya.' Kisha akaanza kusema maneno aliyofundishwa: (ALLAH AKBAR ALLAHU AKBAR X2 ,ASH-HADU ALLAA-ILAHA ILLA LLAHU X2 ……………………)akasema maneno yote ya adhana mpaka mwisho kama yanavyosikika hivi leo.

Maneno hayo yalikuwa mazuri na yenye maana. Mtume alitambua kuwa ndoto ya 'Abdullah ilikuwa ya kweli, Na Alimuomba 'Abdullah kumfundisha swahaba aitwaye BILALI maneno ya Adhana' sababu BILALI alikuwa na sauti kubwa na nzuri.

BILALI (radhi za Allah ziwe juu yake) alisimama na akasoma 'Adhana'. Sauti ya BILALI ilisambaa karibia mji wote wa Madina. Watu walikuja mbio kwenda kwenye Msikiti wa mtume kwa ajili ya salah.

Swahaba mwingine aitwaye UMAR(Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa mmoja wa watu waliokuja na kusema, "Ewe Mtume wa Allah na mimi malaika alinifundisha maneno sawa na hayo (i.e maneno aliooteshwa swahaba wa kwanza, ZAID)katika ndoto yangu jana usiku."

Mtume Muhammad (sala na salamu ziwe juu yake) alikubali hii ‘ADHANA’ kama wito rasmi kwa Salah. Bilali akawa Mu'adhdhin (mtoa adhana) wa kwanza wa Uislam.


HIYO NDO HISTORIA YA ADHANA : SO SIO JAMBO LA KUBUNI ; NI WAHYI (UFUNUO) ULIOLETWA KWA NJIA YA NDOTO NA KUPITISHWA KWA MASWAHABA WA MTUME (I.E WALIOOTESHWA NI MASWAHABA)
 
mikoa mingi China hakuna hiyo kitu.na waislam wanasali on time
 
Kumbe wahyi uliwashukuia hata Maswahaba. Mi nilidhani ilikuwa exclusive kwa Bwana Mtume tu.
 
KUna watu hata MASWAHABA wa mtume hawawafahamu, yaani vurugu tupu.
 
Tatizo ninaloliona mimi ni pale mtaa mmoja unapokuwa na misikiti mitano na wote wanashindana kuadhini.
Wangekuwa walau wanachagua msikiti mmoja tu ndo uadhini na waamin wanaenda nyumba za ibada.
Pia kuna waadhini wastaarabu bana, sauti ya taratibu na haina bugdha, tatizo ni wale wanaotoa sauti mithiri ya wale jamaa wengine wa wokovu wanapoweka spika zao na kuhubiri kwa sauti kama ugomvi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom